Napendekeza mfumo wa ‘Randomizer’ kwenye usajili wa ‘plate number’ za magari nchini

Nadhani yote haya nimeshayafafanua kwenye uzi.
 
Mi nina C imekaza na wala sifikirii kuiuza kwa sasa na hata nikitaka uza nitauza bei nayotaka mimi.

Wananchi wengi wananunua gari kwa kuangalia number plate ila mtindo huo hau guarantee mtu kupata gari zuri hata kidogo.
Well said... Nimenunua namba C five yrs ago bado iko bomba sana kuliko wenye namba D walioagiza..
 
Kuna magari TxxxAAA mazima na mwonekano mpya kuliko hayo D jambo kubwa ni service na utunzaji
 
Ndiyo maana sasa hivi hutakiwi kuagiza gari lililokua zaidi ya miaka kumi...
 
Sina uhakika na wanachofanya mataifa mengine yanayofanana na sisi, lakini ninachoona mimi wazo lako litawaongezea matapeli uwanja mpana zaidi wa kupiga pesa za wanunuaji wasiokuwa makini.
Hata Japan, Huwa wanaweka Grade Points, Kama ni Repaired, Normal Used, Accident and etc, wanawekaga kwa mtindo wa 4.5,5.0,3.0,2.0 etc
 
Ile sehemu ya kwanza hapana, acha tu ukweli utawale kama gari ya zamani acha ijulikane kuwa imesajiliwa zamani

Hiyo sehemu ya car restoration hiyo ndo real deal, hapo umepatia sana. Huyo mtengenezaji azitengeneze na azibrandi hivyo kama refurbished car watu watanunua tu.

Sema shida moja inayotukwamisha ni trust, tukiweza kuaminiana na kuweka pembeni utimilizaji wa matakwa binafsi kwa gharama kwa wengine ndio tutatoboa.
 
filii sipichi iko kazini
Ni upumbavu tu mkuu ndio unasumbua baadhi ya watu! Eti gari zuri kuliko hata hilo la kutoka Japan, tunatengeneza gari sisi? Si hata hilo nalo limetoka Japan? Bure kazi hili jamaa!
 
Ni upumbavu tu mkuu ndio unasumbua baadhi ya watu! Eti gari zuri kuliko hata hilo la kutoka Japan, tunatengeneza gari sisi? Si hata hilo nalo limetoka Japan? Bure kazi hili jamaa!
Kwani gari si zinafanyiwa restoration na kuzirudisha kwenye upya karibia sawa na wa kiwandani, kwanini isiwe nzuri kuliko used ya Japana ambayo haijafanyiwa restoration? Legeza ubongo
 
Labda ungetoa ushauri ushuru wa magari upunguzwe gari sio anasa, ant dumping principal ishapitwa na wakati, gari ikichoka inakatwa screpa
 
Plate number ni number inayoandikwa kwenye plate, na number plate ni plate inayoandikwa number. Sasa chagua wewe ipi ni sahihi
Siku zote nasikia "a car with registration number T XYZ 123" hiyo nyingine sijawahi kuisikia kwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…