Narudia tena, tusije kurudia kufanya kosa kama la 2015. Nchi ilikuwa inaenda kufa

Narudia tena, tusije kurudia kufanya kosa kama la 2015. Nchi ilikuwa inaenda kufa

CAG kutaja hayo madudu halafu mafisadi yenyewe hayajafanywa chochote imetusaidia nini sana sana imetuonyesha ushujaa wa mafisadi jinsi walivyopiga hela nchi haiendelei kwa sababu ya wajinga kama nyie
Katiba na kanuni za nchi,hutoa muda gani report ya CAG kupitiwa na kutolewa maamuzi baada ya kukabidhiwa kwa Rais?.
Kama haujui,basi jitafakari ili usiendelee kuihaibisha familia yako.
 
Makini sana bro
Tusilete mtu wa kuzuia wezi wa pesa za serikali .Tusifanye makosa ya kuleta mtu atakayezuia majambazi,wapiga dili.Bro upo vizur yaan unataka mtu ambaye anaruhusu nchi inaibiwa hovyo.
 
A short lived frenzy and hysteria...Some Say
A Good riddance...Some say Too
A homicidal maniac....His common nomenclature

But I say this, with all his pitfalls, President Magufuli successfully put to light a grotesque and diabolical nefarious cabal that has stealthily sucked our nation's resources like leeches. The people whom we never knew existed. Most of traitors are now known by their names and monikers. For this, he earned my deepest respect
Wewe wasema
 
Hivi mfano Yusuf Manji unaweza sema aliteseka na wakati alihamishia biashara zake South Africa?Vipi wewe mtoto wa mkulima ambaye baba yako alikuwa analima Mbaazi na kumuuzia huyo Manji kwa tsh 2000 kwa kilo,na baada ya kuondoka Manji,Mbaazi zikashuka bei mpaka tsh 150 kwa kilo?

Uelekeo wa upepo ni muhimu zaid.
 
Kila kitu kilikuwa kinaenda ovyo kana kwamba tunaongozwa na darasa la sabau au nursery kabisa.

Hebu fikiria yafuatayo:

1. Uhuru wa habari ulikuwa umezimwa kama mshumaa ikabaki ni kumsifia tu mpaka kikaanziaha kipindi Cha kishindo Cha awamu ya tano.

2. CAG alivyoibua madudu tu akatumbuliwa fasta.

3. Wawekezaji wanakimbia daily wa nje na ndani nchi ikabaki biashara ni ngumu na ukumbuke watu walikuwa wanapoteza ajira daily ndo ikazalisha mass unemployment tunayoiona Leo.

4. Ukiamka tu asubuhi hujui kama utarudi nyumbani salama mana wasiojulikana walikuwa wametanda kila Kona na tunaogopana hasa.

5. Madudu ya yule bwana ni mengi mno natumia kuandika kitabu ili iwe fundisho kwa wengine
Mh🤔 ngoja wale jamaa waje!!
 
Tanzania tuna mfumo wa kipumbavu sana ambapo mambo ya msingi huamuliwa kwa utashi wa MTU
Wazimbabwe kwenye mfumo wa kipumbavu wa Robert Mugabe, wakijifirahisha kwa misemo ya kibaguzi ya Mugabe dhidi ya Wazungu huku Uchumi wa nchi yao ukiporomoka na kufa Kabisa! Propagandist Dictator Robert Mugabe amekufa na kuwaachia Wazimbabwe urithi wa kumuabudu Mugabe ambaye kaua Uchumi wa nchi yao.

Ajabu ya sisi Watanzania pia tuliishi kwenye mfumo wa kipumbavu wa Mwendazake wa kuwachukia Wazungungu, kuishangilia serikali isipoboresha mishahara ya Wafanyakazi, kuona ni jambo jema serikali kuwafukiza kazi wafanyakazi kwa uonevu kwa kigezo cha cheti cha form four, kuona ni jambo la kawaida Polisi kujaa Barabarani kupora hela za Madereva kwa kisingizio cha kubrashi viatu vyao, Kuona ni jambo la kawaida Wakuu wa Wilaya (Sabaya nk) kunda magenge ya kihalifu kupora hela za Wafanyabiashara kwa kisingizio cha Taskforce, kuona ni jambo la kheri JW watukufu wetu kutumwa na mtutu wa bunduki kwenye maduka ya kubadiri hela na kuyapora kwa amri ya Mwendazake, kuona wafanyabiashara wakipachikiwa Kodi kubwa na kusingiziwa Kesi za uhujumu Uchumi, kuona wakulima wanaanzishiwa vikundi vya AMUKOS ambavyo vitakopa mazao ya wakulima na kushindwa kuwalipa tena kwa Bei ndogo, kuona kuvunja mikataba na wawekezaji na kushitakiwa na kuwalipa ni sifa, kuona serikali inaua ajira za Serikali na za Sekita binafsi, na kuwambia vijana Wetu wajiajiri ni jambo jema, kuona Sekita binafsi inauwawa Kodi na Tozo zinazodaiwa kwa mtindo wa taskforce. Kuona vizuizi vya Barabarani ni vingi utadhani nchi iko vitamin, kuona ni Mwendazake pekee ndo mwenye uwezo wa kugundua ufisadi na kuutangaza Vyombo vya habari vikigundua vikatangaza vinafungiwa nk nk nk.
 
Kuunganisha vituo vya habari kwa lazima kila ifikapo saa 2 usiku.
Lazima waungane na Tibisii na taarifa ya kwanza ni yeye bichwa[emoji16], alisema akifa yeye haoni wa kuiendeleza nchi.
Viroba na mito ilifanya kazi kumaliza ndugu zetu, shetani yule asifufuke hata siku ya kiama
 
A short lived frenzy and hysteria...Some Say
A Good riddance...Some say Too
A homicidal maniac....His common nomenclature

But I say this, with all his pitfalls, President Magufuli successfully put to light a grotesque and diabolical nefarious cabal that has stealthily sucked our nation's resources like leeches. The people whom we never knew existed. Most of traitors are now known by their names and monikers. For this, he earned my deepest respect.
Mitandao ya mafisadi papa wa CCM imekuwa wazi miaka yote. JPM haku-shed any new light on the scourge. Hujuma za hao mafisadi hazijawahi kuwa za kificho sana. Dili zao kubwa kama EPA, ndege, rada, Tegeta escrow, Richmond, n.k. zimekuwa nyimbo za taifa nchini. Hata wahusika wanafahamika. Lakini ndio hivyo tena: wamekamata dola hakuna mwenye ubavu wa kuwashughulikia. They are untouchables to this day.

Hakuna kipya Magufuli alichofanya kuhusu mafisadi wakuu wa CCM. Hakuna cha mahakama ya mafisadi wala nini. Sana sana alivibana vifisadi uchwara kwenye ofisi za umma na kufyekelea mbali posho, maslahi ikiwa ni pamoja na baadhi ya stahiki za wafanyakazi huko chini. Kule juu mitandao ya mafisadi wakuu wa CCM iliendelea kupumua tartiib kusubiri “zamu” kama jadi. (Sijui angejiongezea miaka wangefanyaje?!)

BADALA YAKE na yeye akaweka mtandao wake ulioendeleza ufisadi mkubwa tena kwa jeuri na kibri ya hali ya juu. Katiba, sheria, mifumo vikawekwa kando kabisa. Hakukuwa hata na pretense ya utawala bora (mwamba hakuwa na haya kama waliomtangulia). Vyombo vya habari vikapigwa pini. (Hii ni kuzima mwanga). Viongozi wa mikoa na wilaya wakawa wakikumbushwa wajue aliyeshika maslahi yao na mhimili uliojichimbia chini zaidi! Mbinu na vikundi vya kigaidi vikawa mobilized kushughulikia wapinzani, wakosoaji na wasiomnyenyekea mtawala. Ikawa a reign of terror, literally!

Mleta mada ana hoja nzito kwa watanzania walioamua kusimama kwenye KWELI.
 
Mitandao ya mafisadi papa wa CCM imekuwa wazi miaka yote. JPM haku-shed any new light on the scourge. Hujuma za hao mafisadi hazijawahi kuwa za kificho sana. Dili zao kubwa kama EPA, ndege, rada, Tegeta escrow, Richmond, n.k. zimekuwa nyimbo za taifa nchini. Hata wahusika wanafahamika. Lakini ndio hivyo tena: wamekamata dola hakuna mwenye ubavu wa kuwashughulikia.
Now, this is what I call a hive mindset and over-sensationalism of Tanzanian intelligentsia.

Kama unadhani ufisadi wa CCM ni EPA, BAE-Radar, Tegeta ESCROW, RICHMOND, MEREMETA na DOWANS basi itabidi tukufunge kurunzi la NASA. Tanzania hii kuna watu ambao ni hatari kwa nchi na hata nchi jirani. The Panama Papers zilivyovuja kuna mambo yalikuwa ya hatari mno mle na watanzania walikuwepo, lakini nashangaa wewe hujayagusia hapa kabisa. Wewe umekomaa na ufisadi wa vigogo wa CCM tu ambao uko kwenye magazeti hujagusa yale ya gizani.

The Panama Papers zinasema kuna watanzania wamezaliwa na kukulia mkoa wa Iringa lakini wana ukwasi wa kutisha kiasi cha kumwaga mabilioni ya pesa kwenye vyama vya siasa na makundi ya wahalifu kule nchi za Afrika ya kati na Afrika Magharibi. The trademarks of these people are just appalling, and makes scandals like EPA na ESCROW look like peanuts. If you carefully read the Panama Papers you'll discover that the Richmond CCM thugs are nothing but kindergarten babies compared to these international mafia.

They are untouchables to this day.
Saying some people are "still untouchable" is a misnomer for phrases "blatant denial", and "sensationalism", which are major drawbacks for acumen and intellectual objectivity.

Hakuna kipya Magufuli alichofanya kuhusu mafisadi wakuu wa CCM. Hakuna cha mahakama ya mafisadi wala nini. Sana sana alivibana vifisadi uchwara kwenye ofisi za umma na kufyekelea mbali posho, maslahi ikiwa ni pamoja na baadhi ya stahiki za wafanyakazi huko chini. Kule juu mitandao ya mafisadi wakuu wa CCM iliendelea kupumua tartiib kusubiri “zamu” kama jadi. (Sijui angejiongezea miaka wangefanyaje?!)
Hili la CCM kuguswa nadhani wandani wa chama kama Mzee wetu Jakaya Kikwete, Raisi Samia, Mzee Kinana, Mzee Lowassa, Mzee Makamba, Mzee Mangula, Mzee Membe, Mzee Rostam, na Marehemu Mzee Mkapa (May his soul rest in peace), ndiyo wanaweza kutoa majibu sahihi kwamba CCM iliguswa au haikuguswa.

BADALA YAKE na yeye akaweka mtandao wake ulioendeleza ufisadi mkubwa tena kwa jeuri na kibri ya hali ya juu. Katiba, sheria, mifumo vikawekwa kando kabisa. Hakukuwa hata na pretense ya utawala bora (mwamba hakuwa na haya kama waliomtangulia). Vyombo vya habari vikapigwa pini. (Hii ni kuzima mwanga). Viongozi wa mikoa na wilaya wakawa wakikumbushwa wajue aliyeshika maslahi yao na mhimili uliojichimbia chini zaidi! Mbinu na vikundi vya kigaidi vikawa mobilized kushughulikia wapinzani, wakosoaji na wasiomnyenyekea mtawala. Ikawa a reign of terror litera
Now, was Magufuli a saint ? No, he wasn't, and I never said he was.
He was a dark figure. Not, only dark, but pitch-black dark.. Nevertheless, he was Darkness in God's servitude.

As a historian and political realist, I have come to understand that Darkness is an integral part of human development.
See! similar cases were evident in America, England, China, Scandinavia, Russia, Singapore, so Tanzania is no different.

Ukweli mchungu ambao wengi wenu humu mliojaa hisia mnashindwa kuukubali hadi kushindwa kuangalia mambo kwa mapana yake ni kwamba vita ya Raisi Magufuli imewanufaisha CCM, CHADEMA, TISS, JWTZ, Raisi Samia na watanzania wote kwa ujumla. Kuna baadhi ya watu hapa nchini kama wasingeondolewa na Raisi Magufuli, hata upinzani wangechukua nchi sidhani kama hata wao wangeweza kuwagusa.

Huu ndiyo ukweli mchungu ambao hata watu kwenye vyombo vya usalama wanaufahamu lakini kwasababu ya chuki na hisia hawawezi kuukubali hadharani. This is understandable on their side, President Magufuli was an excessive lose canon. Moja kati ya majasusi waandamizi nchini, Mzee Mizengo Pinda akiwa waziri mkuu aliwahi kutamka hadharani bungeni kwamba tukiwagusa mafisadi uchumi wa nchi utayumba. Huu ndiyo utamaduni ambao ulijengeka hadi pale alipokuja Raisi Magufuli.

Raisi Samia angemkuta Yusuph Manji yule wa kipindi cha Jakaya Kikwete, sidhani hata kama angediriki kuwatuma vijana wake wa TISS kwenda kumkamata pale uwanja wa ndege wa Nyerere na kumshughulikia. Mtu ambaye kawaweka majaji na wanasheria wa serikali mfukoni, anakopesha makada wa CCM, ameshika tenda kubwa za jeshi, anawahongwa mashehe na kuna vijana wa TISS ni wafanyakazi wake unadhani hata CHADEMA wangechukua nchi wangemfanya kitu ?

Hivi watu kama Patel, Harbinder, Rugemalila unadhani unaweza kuwashinda kwa kwenda nao mahakamani ? Hata huko Marekani mnakopenda kukusifia walishughulika na mafisadi katika njia hizihizi ambazo TISS na Magufuli walizitumia. Ukifuatilia mambo ambayo EDGAR J HOOVER aliyafanya miaka ya 1920's dhidi ya Wakomunisti wa Marekani waliokuwa wanataka kusababisha vurugu, miaka ya 1930's dhidi ya magenge ya wahalifu kama kina John Dilinger, unaweza kubaki mdomo wazi tu. Sema shida yenu kubwa ni kwamba hamuwezi kuungalia ukweli usoni.

Mleta mada ana hoja nzito kwa watanzania walioamua kusimama kwenye KWELI.
Hoja ya mleta mada ni nzito mno, na hakuna muungwana anayeweza kuipinga hata kidogo. Hata binafsi siwezi kuipinga kwasababu nafahamu kilichokuwa kinaendelea hapa nchini kwa kukiona siyo kusimuliwa au kulishwa maneno na mitandao. Hivyo nafahamu ukweli ni upi na wongo ni upi.

Ukweli ni kwamba mtu wa hulka ya Raisi Magufuli alitakiwa aishie nafasi ya utendaji kama uwaziri mkuu na siyo kuachiwa uraisi wa nchi kama Tanzania. Ila akapewa madaraka kwasababu mifumo ya nchi haikuwakubali Lowassa na Membe. So he was a compromise candidate na kulikuwa hakuna mbadala zaidi yake. Lakini pia historia yake ya utendaji ilimbeba sana. Japo wengi tunaomfahamu tokea yuko ujenzi na tabia zake za kibabe tulikuwa tunacheki tu tunasema hawa hawajui wanachokitaka.

Ukweli mwingine ni kwamba Tanzania inabidi ijifunze, hasa watawala wa CCM kwamba Raisi Magufuli alikuwa ni zao la mfumo mbovu wa kushindwa kuandaa viongozi na makundi mabaya ya kukomoana na ulaji yaliyojengwa na Raisi Kikwete na genge lake tokea miaka ya 90's. Hivyo watanzania mnaolalamika mngekuwa waungwana sana kama lawama zingeenda pia kwa watu waliomuweka Raisi Magufuli ilhali wakijua tabia zake ngumu tangu akiwa waziri.

Ukweli mwingine mgumu kuumeza ni kwamba, Raisi Magufuli anapendwa sana na watanzania wa kawaida ambao wewe na mimi tunawaita "Uneducated" and "unsophisticated". Sisi tuliotembea sehemu kubwa ya Tanzania, mjini na vijijini tumekuja kuukubali huu ukweli hata kama hapo mwanzo tulipingana sana na sera za Magufuli. Mpaka sasa naendelea kujifunza vitu vipya na nazidi kubadilika mawazo kuhusu Magufuli, japo baadhi ya sera zake mbovu ntaendelea kuzichukia na kuzilaani.

A Champion of the common folk, is an accolade I cannot deny him. I choose to give the devil his dues.

Uwongo kuhusu Rasi Magufuli ni huu: Kwamba kila aliyeguswa na Raisi Magufuli alikuwa ni mtakatifu na alionewa wivu kwasababu Raisi Magufuli alikuwa ni mtu wa visasi na mwenye kukurupuka. Kwamba Raisi Magufuli alikuwa anawonea wivu wakina Shubash Patel, Sumaiyah, Dewji, Rostam Aziz, Gulam brothers, Manji, Harbinder, Rugemalira na kwamba hawa walikuwa ni malaika ambao hawana dhambi dhidi ya hili taifa. Huu ni upuuzi mkubwa mno, kwasababu mafaili kuhusu hawa watu TISS walianza kuyapeleka ikulu tokea awamu ya tatu lakini yakapigwa kapuni.

Tena kama ulikuwa hujui mafaili haya yalipelekwa kwenye uchaguzi wa CCM mwaka 2005 ili kumfanya Jakaya asiwe Raisi kwasababu alikuwa na mtandao mbaya. Lakini hata Mzee Mkapa na ubabe wake alishindwa kufanya lolote lile kwasababu alikuwa anaogopa kugusu baadhi ya mambo nchi isichafuke.

Uwongo mwingine wa mwisho ambao wengi mnaoupenda ni huu: Utawala wa Raisi Magufuli was a one man's show. Kitu ambacho wengi hamkifahamu ni kwamba Tanzania mbali na madhaifu yake mengi ina mifumo ya kiusalama yenye nguvu kubwa mno. Tanzania is not a ramshackle kleptocracy. Kama Raisi Magufuli angekuwa peke yake basi hata mwaka mmoja asingemaliza salama. Nyuma ya pazia Raisi Magufuli alikuwa anaungwa mkono na genge la MIZEE YA COLD-WAR, ile mijasusi ya tokea kipindi cha Nyerere ambayo haitaki kukubali kwamba vita baridi imeisha na dunia imebadilika.

Kuna wazee wazito ndiyo walikuwa wanampa Magufuli taarifa hadi akaweza kufahamu apige wapi na kufanikiwa kuwakata baadhi ya watu mikia. Hivi unadhani kwa akili ya kawaida tu, Raisi Magufuli anageweza kuwashinda wakina Mkapa na Kikwete kirahisi-rahisi tu ? Kuna wazee nawafahamu wa kichagga, Kihehe, kibena, Kinyakyusa ndani ya mfumo ambao walikuwa wanafurahishwa mno na uongozi wa Raisi Magufuli hadi kumuunga mkono kwenye kumkomesha Jakaya ambaye wengi kizazi cha Nyerere huamini kwamba hakutakiwa kuwa Raisi mwaka 2005 na ndiye kansa ya nchi.

Mwisho kabisa: Nakubali watanzania waliumizwa, lakini tatizo siyo Magufuli peke yake. Kumwangushia jumba lote la lawama na kushindwa kufahamu kwamba kuna maelfu nyuma ya pazia waliouwezesha utawala wake ni ujinga wa kupindukia. Ndiyo maana hata Hitler alipoondoka kulikuwa na The Denazification Project kuwaondoa wafuasi wake watiifu ndani ya Ujerumani. Ila pia kusema kwamba miaka yote mitano hakuna jema ambalo Raisi Magufuli amefanya ni ubazazi ambao mimi binafsi niliyefanikiwa kwenda shule na kuelinika, pamoja na kuifahamu hii nchi vizuri siwezi kukubali kulishwa na mtu yoyote, nimeona kwa macho yangu na kusikia kwa masikio yangu.
 
A short lived frenzy and hysteria...Some Say
A Good riddance...Some say Too
A homicidal maniac....His common nomenclature

But I say this, with all his pitfalls, President Magufuli successfully put to light a grotesque and diabolical nefarious cabal that has stealthily sucked our nation's resources like leeches. The people whom we never knew existed. Most of traitors are now known by their names and monikers. For this, he earned my deepest respect.
Taratibu Mkuu! Umetumia Kiingereza cha juu mno! Una undugu na Shakespeare nini?
 
Kila kitu kilikuwa kinaenda ovyo kana kwamba tunaongozwa na darasa la sabau au nursery kabisa.

Hebu fikiria yafuatayo:

1. Uhuru wa habari ulikuwa umezimwa kama mshumaa ikabaki ni kumsifia tu mpaka kikaanziaha kipindi Cha kishindo Cha awamu ya tano.

2. CAG alivyoibua madudu tu akatumbuliwa fasta.

3. Wawekezaji wanakimbia daily wa nje na ndani nchi ikabaki biashara ni ngumu na ukumbuke watu walikuwa wanapoteza ajira daily ndo ikazalisha mass unemployment tunayoiona Leo.

4. Ukiamka tu asubuhi hujui kama utarudi nyumbani salama mana wasiojulikana walikuwa wametanda kila Kona na tunaogopana hasa.

5. Madudu ya yule bwana ni mengi mno natumia kuandika kitabu ili iwe fundisho kwa wengine
Acha uongo wewe. Inawezekana mwenyewe ulitumbuliwa au ulikimbia ofisi kwa cheti feki. Usifikiri ni zamani wakati watu karibu wote tulikuepo. Sasa hivi wanamchi wanalinganisha samia na magufuli wamebakia kulia tu.
 
Back
Top Bottom