Kwa kuwa nimeona uko interested na teknolojia za upigaji picha na kurekodi video za vyombo vya angani basi kasome vizuri hii kitu imaitwa tracking gimbal system inahusu jinsi camera za vyombo vya angani hufanya kazi
View attachment 3568932
Katika wote waliojibu Atleast umekuja na majibu makubwa sana na nilitegemea mtu aje ajibu kuhusu Gimbal..
chukua Bia nitalipa..
na niseme tu nakushukuru kwa hii picha ya
Tracking Gimbal System, na kwa bahati nzuri kabla ya kupost hoja yangu ilibidi nipitie vitu vingi sana mpaka gimbal system yote na niliangalia pia how wanaweza kupiga picha clear ndo nikakutana na hii system ya kamera kubaki imeelekezwa (point) kwenye kitu kimoja hata kama chombo kinayumba au kusogea.
Lakini, hii teknolojia
haimalizi tatizo la mzunguko wa Dunia.
1. Gimbal Inafuatilia (Track), Lakini Haizuii Mwendo wa Ndani (Internal Motion)Gimbal inaweza kuifanya picha ya Dunia isitikisike (stability), lakini haiwezi kuzuia mzunguko wa kile unachokipiga picha.
- Mfano: Ikiwa nitatumia 'Gimbal' kumpiga picha mtu anayezunguka kwenye kiti (rotating chair), Gimbal itahakikisha mtu huyo yuko katikati ya picha, lakini bado nitaona mtu huyo akizunguka.
au ngoja niseme kitu yaani Ikiwa Dunia inazunguka kwa km 1,600/hr, Gimbal inapaswa kuifanya Dunia iwe katikati ya picha, lakini bado tunapaswa kuona mabara yakipita (moving targets). Kwanini bara la Afrika limeganda palepale kwa siku kadhaa? Gimbal ina uwezo wa kusimamisha mzunguko wa sayari nzima kwenye lensi?
2. Gimbal inasawazisha mtikisiko wa chombo, lakini chombo cha Artemis kiko kwenye safari ya kuelekea Mwezini (Linear distance). Unapozidi kwenda mbali, pembe ya kuona (angle of view) inabadilika. Ikiwa Dunia inajizungusha, 'Gimbal' ingelazimika kuzunguka yenyewe kwa kasi kufuata bara la Afrika kadiri linavyoelekea upande mwingine wa usiku. Inakuwaje 'Gimbal' iweze kung'ang'ania bara moja tu wakati sayari nzima inatakiwa kuwa inageuka?
3. ok sawa tutakubali kuwa 'Gimbal' na mzunguko wa Dunia vimesawazishwa (ambalo kifizikia ni gumu), bado tuna tatizo la
Mawingu. Mawingu hayafuati 'Gimbal'. Mawingu yanapaswa kusogea na kubadilika sura (morphing) kutokana na upepo. Kwenye video ya Artemis, hata mawingu yanaonekana yameganda. Je, Gimbal ina 'lock' mpaka mawingu?"