Nashauri awamu ya sita agombee Rais Mstaafu Ndg. Jakaya Kikwete

Kiukweli Kikwete arudi tu, samahani lakini mwamba ni ×1000 kuliko aliyepo. Huwa tunawaacha wanawake ila ukigundua ulifanya makosa unamrudia na unatulia kabisa.

Nadhani pia na yeye atakuwa amejifunza kitu, kiufupi Kikwete anatakiwa awe Raisi wa milele. Sisi Watanzania hii nchi ni yetu sote , watu maisha magumu alafu mtu amekomaa na madaraja, hapana kabisa.
 
Habari Kama hizi Lissu akiona anajisikiaje? Au yeye hastahili kuwa Rais?
 
Wewe huna akili na sidhani kama hata una uelewa. Kikwete ni adui wa pesa za tanzania. Kama unampenda sana mwalike kwako unywe naye kahawa au mfanye rais wa familia yako.

Kikwete aliiharibu sana hii nchi na siwezi hata kumfikiria yeye kuwa waziri acha urais. Thank god haitowezekana tena na pengine ni kuanza kufanya maombi asije tokea rais kama kikwete tena tanzania hii.
 
Rais ajae ni Majaliwa Kassim Majaliwa na Waziri wake Mkuu atakua Freeman Mbowe. Save this
Mbowe hawezi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa namna yeyote ile. Akiwa yupo upinzani au akiwa yupo CCM, haiwezekani.
 

Wataka chai? Karibu na tende
 
Hussein Ali Mwinyi ni turufu sahihi, ila kwa tunavyoteseka hivi huyu mpole tutampelekesha balaa.
 
Watanzania tumekosa akili kiasi hichi
Hamuwazi balaa alilofanya huyu bwana bado mnataka balaa lingine tena

Hakuna anayewaza Sasa kwamba ndiyo muda wa kutafuta katiba mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…