Nashauri Rais Samia ambadilishie kituo cha kazi Paul Makonda. Arusha inatosha, aende mahali pengine

Mwambieni Mbunge ajue mipaka yake na awe na adabu kwa wakubwa. Makonda ana zaidi ya Wabunge sita chini yake, kwa nini wakulia lia awe Gambo tuu? Mwambieni atulie, imeandikwa, ukiua kwa Upanga utakufa kwa Upanga. Gambo asome alama za nyakati, siasa za sasa hazimtaki. Hata kama asingekuwepo Makonda, Gambo asingepita kura za maoni CCM.
 

Chawa wa Gambo wache watoane macho hakuna anaye wataka . Mtu ambaye anapendwa Arusha ni Lema wengine wanategemea serikali . Wote wajinga jinga
 
Ubunge ni Cv kubwa kuliko mkuu wa Mkoa..

Kuna wabunge baada ya kushindwa uchaguzi walipozwa kwa kupewa u-Dc au kupewa u-Rc.

Ukimpa leo mbunge yeyote wa Ccm options, ama aendelee na ubunge au ateuliwe kuwa mkuu wa mkoa...lazima atachagua kuendelea na ubunge.

Hata Makonda aliuweka rehani ukuu wa mkoa, akaenda kugombea ubunge kigamboni...

Makonda ni Rc msumbufu sana.
Ni vile tu hajakutana na mbunge mjuaji.
Gambo sijui nae vp tu.....Mbunge wa chama tawala unapelekeshwaje kizembe hivyo..si amtie kofi tu.
 
Huyu Makona alitakiwa akutane na mbunge mjeuri sampuli za Ole sendeka, Msukuma, Kigwangala, au hata li-Gwajima.

Wakuu wa mikoa wana shughuli chache sana kimiongozo..
Kulazimisha kutrend ndio kunamfanya Makonda afanye shughuli za watu wengine...

Mbunge yupo, Madiwani wapo, Wakurugenzi wapo, Meya yupo, Ras yupo, Das vilevile.....
Makonda anataka yote afanye yeye.

Ipo tofauti kati ya mkuu wa Mkoa na Gavana wa eneo.
Makonda amejigeuza kuwa Gavana.
Hicho cheo hatuna Tanzania.
Gavana yupo mmoja tu wa B.O.T tu nae hana mkoa wala Jimbo.

Na kwanini ang'ang'anie Arusha mjini tu,
Kwani Hazipo wilaya nyingine.
 
Milioni 400 ya bodaboda imeliwa 2016. Msimamizi akiwa Mrisho Gambo. Inaonekana CCM wanajua na kujuana nani kaiba pesa wapi. Wanakaysha ila wakizinguana ndio wanafukua makaburi.

Kutakuwa na upigaji kama huu sehemu nyingi tu.
 
Hao wote ni wahuni. Makonda ni mhuni na kibaka, Gambo nae ni mhuni na kibaka. Ni vibaka toka enzi na enzi.
Ndo wamekutana sasa !
Ngoja tuone nani msomi wa Kweli kuliko mwingine na nani ni wa mujini na nani wa pande za Bush
Ila sidhani kama atajitunisha tena
wanasemaga unaweza kulihamisha Jabali lililopo baharini lakini huwezi kuihamisha tabia ya mtu πŸ™„ !
Ngoja tuone !
 
Arusha tu ?!!
Labda ndipo kwenye njuluku mingi maokoto mingi !
 
Hapo kuna Mbunge wa Arusha mjini na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mjini.
 
Tatizo la huyu jamaa ni hilo kujijenga mwenyewe na kupuuza wengine na kudharau wengine,kipindi cha Magu aliwadharau mpaka mawaziri.Nafkri kuna kitu hakiko sawa,na atajitambua kwa kuchelewa.
 
Poleni chawa wa Makonda na Gambo. Ubunge tu ndio unafanya mpigane hivyo au kuna sababu nyingine?
 
Katika watu wapo na tamaa ya madaraka tz hii Makonda ni mmoja wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…