Nashauri safari za mabasi kutembea saa 24 zisitishwe, vifo vitamaliza watu

Watanzania wanaendeshwa na hisia kuliko akili
 
Acha kelele zako,
Leta takwimu zinazoonyesha basi za abiria kusafiri mchana ni salama zaidi kuliko usiku.
Leta idadi ya ajali zilizotokea usiku dhidi ya zile za mchana. Vinginevyo wewe na wenzako wa aina yako ni wa kupuuzwa tu.
 
Changamoto ni vihiyo na wajinga kuwa wengi katika jamii na vivyo hivyo kwenye mamlaka za usimamizi na utoaji leseni.
Matajiri wenye magari kwa sababu ya ujinga wa jumla wanawakabidhi vijana wapuuzi waliopitishwa na mamlaka bila weledi, magari ya thamani kubwa na maisha ya abiria.
Watu wengi huangamia kwa kukosa maarifa na weledi katika taifa kwa ujumla.
 
hamna shida amkeni tu,ila msisahau barabara zenu ni vichochoro,hata taa hakuna.

wenzenu wanaamka huku wanawajibika,nyinyi mnaamka huku mnapiga siasa tu.
Suluhisho ni kupanua barabara sasa sio kuwafanya watu wasifanye kazi usiku.
 
Kama hakuna data zinazoonesha ajali za usiku ni nyingi kuliko za mchana basi, hii hoja haina mashiko.

Tupende kutafuta data kwanza. Huu ni uchumi,kazi za watu.
Huwezi amini usiku abiria ni wengi sana
 
Kama unapotokea kuna vibaka sana basi panda gari za saa mbili asubuhi, sio lazima kusafiri na linaloanza safari saa kumi usiku.
 
mtu anatoa ushauri safari zisitishwe wanatokea wanywa mbege, ulanzi na konyagi huko kelele nyingi hatutaki wewe acha sijui nzuri sijui fwee fwee,
kwa nini miaka yote safari hua zinazuiwa? na wanaruhusu tena,
hata mimi nashauri uthibiti uongezeke hakuna asiyejua hawa madereva wa masafa ukiacha speed kali wanaendesha hovyo kweli kweli peke yao ndo wanawahi wanakoenda

na wahuni wamepandisha nauli hivi wafute kabisa safari za usiku nyambafu.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Tujifunze kuleta mawazo ya kuboresha, sio kufungia na kusitisha tu. Labda pia uje na takwimu za ku-support hoja yako

Mchana mabasi yanasafiri mangapi? Ajali zake ziko ngapi? Vifo vingapi? halafu fananisha na usiku pia.

Halafu tutazame pia faida na hasara kwa uchumi, risk ni sehemu ya maisha.
 
Haina uhusiano na kusafiri usiku. Miaka yote ajali zinatokea gari zinasafiri mchana mbona hushauri nazo zisitishwe?
 
na kwasasa usiku kuna abiria wengi sana,kama umewahi safiri usiku utakua shahidi.
 
Kuna ukweli usiku ni muda wa kulala hata kama ulipumzika vipi, kuendesha labda yawe mayahudi mawili anaetoa gari ikifika saa nane usiku anampa mwingune aliyepumzika kwa kujiegesha pale chini.


Kingine gari za isamilo ni mbovu mno hazifanyiwi service mapema kuna moja juzi nilikuwa inatoka mwanza yaanj nilikuwa inasimama barabarani inafanyiwa service wanamwaga oil mule abiria wanasubiri tu zaidi ya mara moja
 
Hapo umetoa elimu sahihi katika uwanja usio sahihi.

Jf ya sasa imejaa wabishi wasiokuwa na uelewa.
 
Nakubaliana nawe kwenye ishu ya kujikagua hasa breki na matairi kabla ya kugeuka baada ya kusafiri safari ndefu..ila safari za usiku ni salama kabisa kwa sababu magari yanaenda kwa ratiba ya muda mfano gari linaloenda mwanza linapangiwa mda wa kufika dodoma, singida,nzega, shinyanga nk sasa hapo akiwahi sana kabla ya muda kuna sheria zinafuatwa...wanaheshimu muda siku hizi. Kuhusu kupata ajali zaidi usiku labda kama unatakwimu halisi toka polisi ila ajali hata mchana zipo nyingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…