Nashauri safari za mabasi kutembea saa 24 zisitishwe, vifo vitamaliza watu

na kwasasa usiku kuna abiria wengi sana,kama umewahi safiri usiku utakua shahidi.
Kweli Mkuu! Juzi nilikua nataka kusafiri na gari ya saa 10 jioni (newforce) wakaniambia seats zilizokuwepo. Nikawaambia niwekee namba 11 nitalipa kwa mpesa. Mtandao ulinisumbua kidogo jamaa wakanipigia simu kuwa zimebaki za nyuma. Ikabidi nichukue ya saa 2 usiku.
 

Labda alimaanisha halijafanyiwa hata usafi ..
 
Mie nafkir kuwe na Certification maalumu ya kubeba abiria usiku.

Kwa kuzingatia vipimo mbalimbali ikiwemo cha afya na matumizi ya pombe.
 
Suluhisho ni kupanua barabara sasa sio kuwafanya watu wasifanye kazi usiku.
kama ni lazima kufanya kazi usiku bila kuzingatia mazingira yanini kuingia gharama kupanua barabara??

tunaitwa ulimwengu wa 3 sababu bado hatujajua kipi ni sahihi kipi si,kama tuna usokwe kwa mbali bado.

ndio maana hata tbs iko radhi kupitisha bidhaa viwango hafifu kwa sababu watu wanatumia na maisha yanakwenda.
 
Hatujitambui mkuu
 
Nazn ni usimamizi na utaratbu ufuatwe lakn sio kufuta safr za usiku
 
Acha kelele zako,
Leta takwimu zinazoonyesha basi za abiria kusafiri mchana ni salama zaidi kuliko usiku.
Leta idadi ya ajali zilizotokea usiku dhidi ya zile za mchana. Vinginevyo wewe na wenzako wa aina yako ni wa kupuuzwa tu.
una ujinga mwingi kaa nao uendele kukudhuru peke yako.

nikupe data kwa sababu unabisha au?
nakupa homework nawewe usipende kutafuniwa utaendelea kudumaa kichwa,ingia kwenye utafiti utaelewa kwanini hatukubaliani.
 
Watu wenye lodge na migahawa wanapambania ugali wao.....
kwahiyo mkuu una risk maisha kisa kukwepa kula njian na kulala guest[emoji1787][emoji1787][emoji1787].

hii nchi kweli ni chanel ya vituko huko mbinguni.
 
Aliyeanzisha hii mada amewasilisha maoni yake ambayo ninayaheshimu lakini sikubaliani nayo.
Nasafiri saana kwenda ARUSHA na Moshi kibiashara nikiwa nimebeba time sensesitve items kama madawa nakadhalika na usafiri wangu mkubwa ni magari ya BM COACH,mwendo wao nyakati za usiku ni mzuri saana kuliko mchana na abiria wanagombania tiketi za usiku
 
Ujinga.Ajali zimeanza Leo Tzn hapa?

Wakati safari ni mchana tuu Ajali zilikuwa hazipo?
 
Naunga mkono hoja, zifutwe tunaangamia!
 
Mleta mada upo sahihi safari za usiku Zinaleta adhari nyingi kuliko mchana Hata hizo ajali za alfajiri au mchana ni sababu ya kusafiri usiku .

Dereva hapumziki vya kutosha usiku na unakuta kampuni nyingine wabahili kuweka madereva Wawili .
Mfano hai nilisafiri na Dar Lux mwanza - Dar kidogo tupate ajali dereva ametoka Dar Mpaka mwanza akageuza kurudi Dar akachoka akampatia gari rafiki yake asiyejua njia matokeo tukaparamia tuta wakati mvua inanyesha na huko njiani tulikosakosa malori mengi yapo full mzuka na mataa full Kama Treni .
 
ajali ya singida imetokea asubuhi,
ajali ya lindi asubuhi.
hsyo ya usiku ajali we ni ipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…