Nashauri safari za mabasi kutembea saa 24 zisitishwe, vifo vitamaliza watu

Kwa hiyo hii Ajali ni usiku?

View: https://www.instagram.com/p/C0OGVinM_E5/?igshid=NmJiYWZiY2E0Mg==
 
Ni ushamba tu ajali zipo mda wote usiku na mchana safari za usiku zimefungua nchi kibiashara kwa mfano kwa sasa ninaweza kutoka dar jioni nikaingia Mbeya asubuhi na nikageuza kibiashara imekuwa nafuu kubwa sana
 
Mtu wa kwanza wa kukali usalama barabarani ni abiria mwenyewe, toa taarifa unapoona ukiukaji wa uendeshaji wa vyombo vya usafiri barabarani, hata iwe mchana.
 
Mkuu hoja iambatane na ushahidi. Ungeambatanisha ushahidi wa ajali kama mbili tatu za usiku hoja ingekuwa na mashiko.
 
Usiku kuzuri aiseee watu tunakula sana kimasihara!
 
No research, no right to speak.
Ufanyike utafiti kabla ya uamuzi wowote.
Ikionekana ajali za magari yanayosafiri mchana ni nyingi kuliko yanayosafiri usiku, utapendekeza magari yazuiwe kusafiri mchana?
Hoja isiwe kuzuia.
Hoja iwe kupata suluhisho
 

Ajali hata mchana zinatokea tena mbaya zaidi sio hoja katika hili na je magari yote yanayotembea usiku yanapata ajali?

Nashauri huduma za usafiri ziendelee kufanyika 24hrs chamsingi udhibiti uongezeke.
 
True 💯 ! Naunga mkono hoja !
 
Haya kwa bongo bado muda utaongea
Muda utaongea !
Safari za usiku za mabasi ni sawa na kupeleka watu kuzimu !!
Madereva wengi ni reckless tena mchana na Askari na tochi zao wapo barabarani ! Je usiku itakuwaje na wanajua hakuna tochi za Askari ??!!

Watamaliza watu ! Nawashauri abiria msipande mabasi ya usiku !!
 
Kila ajali Tunasemaga hiyo ni kazi ya Mungu !!
Hata kama Dereva alikuwa mzembe !
 
ajali ya singida imetokea asubuhi,
ajali ya lindi asubuhi.
hsyo ya usiku ajali we ni ipi
Imetokea asubuhi lakini hapo utakuta dereva hakulala usiku alikuwa anaendesha. Ajali kutokea mchana mara nyingi madereva wananaendesha usiku so wanachoka mchana wanasinzia
 
Imetokea asubuhi lakini hapo utakuta dereva hakulala usiku alikuwa anaendesha. Ajali kutokea mchana mara nyingi madereva wananaendesha usiku so wanachoka mchana wanasinzia
Na ndivyo ilivyo !!
 
Kila ajali Tunasemaga hiyo ni kazi ya Mungu !!
Hata kama Dereva alikuwa mzembe !
Hilo ndio tatizo kubwa la kutokuwa na akili za kuwaza
Yaani kama Rushwa haitaisha na ajali hazitaisha
Mtu anakamatwa yuko speed anatoa za brashi anaenda kuuwa mbele
Wasomi wanakariri shuleni
Ila sheria za barabarani wanashindwa kukariri
 
Hakika wewe unaandika tu mradi umeandika. Serikali ilifanya tathmini lini? Au hujui maana ya thathmini? Mimi siko hapa kupinga mabasi kusafiri usiku ila napinga uongo unasema hapa. Ni hivi: mabasi hayajaanza siku nyingi kusafiri usiku, hivyo cha kuzingatia ni kuchukuwa na kufanya tathmini mara kwa mara eg kila baada ya mwaka ili kujua kama kusafiri usiku kunasababisha ajali nyingi zaidi.
 
Kusafiri mchana tulikuwa tunapoteza muda sana! Sasa hivi nina uwezo wa kutoka nitokako muda wa saa 2 usiku Dar nafika kesho yake saa 4 asubuhi! Hizi safari ni ukombozi kwa watu wanaujua kupangilia safari zao!
 
Unafikri traffic wamelala? Tuache ujuaji!
 
Na hizi pombe zilizojaa za kupima wwkishajidunga wanajiona Barabarani ni kama wao peke Yao!


Mabasi ya Tanzania imekuwa kama Gaza ni mwendo wa kuchinja tu!
 
Lifanyiwe service hata kama muda wa service bado?
Hebu nunua lako likienda tripu moja ulifanyie service baada ya mwaka uje jukwaani hapa useme umepata faida kiasi gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…