Nashauri safari za mabasi kutembea saa 24 zisitishwe, vifo vitamaliza watu

Kweli kabisa. Mimi nasafiri karibu kila weekend. Wanaenda vizuri tu.
 
Lifanyiwe service hata kama muda wa service bado?
Hebu nunua lako likienda tripu moja ulifanyie service baada ya mwaka uje jukwaani hapa useme umepata faida kiasi gani
Amekariri tu, hajui
 
Una takwimu zozote mkuu za kuthibitisha hilo? Tangu yameanza kusafiri usiku kumetokea ajali ngapi na wangapi wamepoteza maisha mpaka useme tutaisha?
 
Zimpopa kaza fuvu
 
Lile basi la magereza liligonga treni ilikuwa saa 8 usiku au?
 
Usafiri wa usiku uendeleee, hatuwezi stopisha safari za usiku kisa ajali mbili
 
Magari yaruhusiwe, wanaoweza kusafiri wasafiri,
Ambao hawawezi walale nyumbani watasafiri mchana,
Wanaokaa karib na stend watasafiri usiku, wengine mtasafiri asubuhi
 
Umesoma nilichoandika au umedandia tu? Nionyeshe sehemu niliyosema traffic wamelala!
Huko kusema serikali haijafanya tathmini ndiko napingana nako! Hivi unafikri mpaka serikali inasema sasa mabasi wafanye safari za usiku wamekurupuka tu? Ndiyo maana nikauliza unafikri traffic wamelala?
 
Watanzania tujisahihishe. Kila mtu ajitahidi kufuata sheria. Ni upumbavu wa hali ya juu kusikia basi limegonga treni. Madereva wa kitanzania wana ushenzi mwingi wa kutokuwa makini barabarani. Hata madereva wa malori wa kitanzania wanalaumiwa sana kusababisha ajali barabarani kati ya Nakonde - Kapiri Mposhi, Zambia.
 
Shida ni nini?
Mabasi?
Malori?
Madereva?
Polisi?
Service?

Safari za usiku zinaleta freedom kwenye matumizi ya muda!
Na kwa sasa hawatorudi nyuma
 
Ni mabasi mangapi yamepata ajali usiku ?

Mabasi ya Newforce yaliyofungiwa wakati ule hakuna hata moja katika mabasi yaliyopata ajali lililoanguka usiku
 
Tatizo tupo kwenye kila kitu ni shortcuts.
Uchaguzi shortcuts!
Matibabu shortcuts
Biashara shortcuts
Leseni shortcuts
Sheria shortcuts

NB: safari za usiku ziendelee
 
Shida ni nini?
Mabasi?
Malori?
Madereva?
Polisi?
Service?

Safari za usiku zinaleta freedom kwenye matumizi ya muda!
Na kwa sasa hawatorudi nyuma
Maswali ya msingi sana!
Na Mimi nikaongeza kuwa kama mchana hakuna ajali basi tugeuze usiku Mchana kwa kuweka Taa za barabarani njia zote.
 
Huko kusema serikali haijafanya tathmini ndiko napingana nako! Hivi unafikri mpaka serikali inasema sasa mabasi wafanye safari za usiku wamekurupuka tu? Ndiyo maana nikauliza unafikri traffic wamelala?
Haikufanya tathmini yoyote. Ni kukurupuka ndiyo. Ila kunaweza kuwa kukurupuka kusiko na madhara.... muda ndiyo utaamua. Labda nikuulize- trafiki wanazuia ajali kwa kiwango gani? Mbona mchana wanakuwa wamejaa kila amahali lakini bado ajali zinatokea?
 
If that is the case hata tungepiga marufuku kutengeneza visu sababu vinaweza kutumika pia kuleta madhara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…