Nashindwa kuamini hiki ninachokisoma kuhusu haya makato ya LUKU

Nashindwa kuamini hiki ninachokisoma kuhusu haya makato ya LUKU

Mimi nimenunua umeme wa 50,000 sasa hivi, ujumbe wangu huu hapa

Cost 39,344.27
VAT 18% 7,081.96
EWURA 1% 393.44
REA 3% 1,180.33
Debt Collected 2,000.00
TOTAL 50,000.00 20/08/21 22:19

Yaani nimepata umeme wa 39,344 tu, elfu 10,656 ni jumla ya makato,,,, makato ya kununua umeme ni makubwa zaidi kama tozo ya kutuma hela....... hapo ukumbuke, nimenunua kwa simu, tigopesa wamenikata 1,000 ya zaidi....... hii nchi inajitafutia laana, hela ya dhuluma haijengagi hata siku moja
Ngoja wajidai ni wazalendo wao watemebelee veiti,walale kwa 5* hotel.wakafanyiwe masaje na watt wa kiarabu. Watt wao wakisoma uk USA German,feza ,ist wa mwigulu yupo feza wa kwako yupo za bure.
Ndege kila siku Dom dar
 
Ni bora utumie milioni kadhaa ufunge umeme wa nguvu ya jua (solar energy) ili kuachana na ujinga huu...

Ni kodi kweli na tunapaswa kulipa....

Lakini shida iko kwenye ugumu wa implementation yake kiasi cha kila mtu kulazimika kuilipa hata kama hana nyumba eti tu kwa sababu anamnunulia rafiki yake umeme...!!
 
Aise hii sio nchi yangu nayoijuwa hii nimepigwa aisee kwanza mwenye namba za M power anisaidie afu tuone tunaendaje Bujumbura
 
Mtajijua nyinyi na serikali yenu ya kijani ,uzuri hayo matozo yenu yasiyo na kichwa wala miguu yana option! mtu akizidiwa hatumi fedha anapeleka kwa basi na vile vile kuna option ya solar kukimbia hiyo elfu 12 yao ya kodi.
Kuna kodi ya kisima cha maji ukichimba kwako, na hiyo solar wataweka kodi tu Hawa walafi
 
Tatizo la waafrika ni ubinafsi na hatutaendelea hadi dunia inaisha hakuna kiongozi aliopo kwaajili ya raia wake hivi kama nchi haina hela kwanini tunaendelea na zigo la wabunge wasio na tija wanaolipwa mamilioni ya hela kwanini wasipunguzwe kila mkoa ubaki na mbunge mmoja tuuuuuuu???
hii nchi JPM ndio alikuwa anaiweza peke yake. nakumbuka libya, baada ya kufa gadafi cha mito wanakiona sasa
 
Ndugu zangu, Ukisikia nchi imeingia uchumi wa kati ujue kuwa hali ya wananchi itakuwa taaban bin mauti.
Angalia Ethiopia. Wananchi kila Siku wanatoroka nchi yao kuelekea kusini mwa Africa, wengine wanafia maporini kukwepa kukamatwa.
Hata sisi tukae mkao wa kuwa wahamiaji haramu. Ukichimba kisima nyumbani kwako, watu wa maji watafika na kukuwekea mita ya maji.eti maji ni Mali ya serekali. Hayo yanafanyika Ethiopia, nchi yenye madege zaidi ya hamsini yanaenda Ulaya.
 
Huyo jamaa ni boya tu, yule Mzee aliefariki alikuwa na madhaifu yake ila sidhani kama angewahi kuruhusu huu upumbavu kwenye serikali yake.

Ninachoamini huu ni kwanzo tu,kuna mabaya mengi yanakuja mbele ya Safari.
Achen Magufuli apumzikee
 
Mmmh wewe unapataje unit 50.6 kwa 20K?

Mimi huwa napata units 30.6

Elf50 napata 140 unit inamaa nikilipa 25 nitapata 70 nikinunua 20 nitapata unit 50 kwa nini wewe unapata 30?
 
Nchi hii imefika pabaya. Mabeyo na watu wake waingilie kati. Yaani hata umeme tunapangiwa tununue wa shilingi ngapi! Kwani mnatupa hela vile?
Habari za jioni wateja wetu.
Kuanzia leo sheria ya kulipa kodi ya jengo kupitia manunuzi ya umeme imeanza kutekelezwa.
Kwa hiyo mteja akinunua umeme atakatwa shs 2000 ikiwa ni kodi ya Jengo inayodaiwa na Tra.kodi hii ilitakiwa kuanza tarehe 01.07.2021 lakini imeanza leo.
Hivyo mteja akinunua umeme kuanzila leo atakatwa shs 2000 ambayo ni kodi ya jengo ya miezi miwili ya (Julai na Agasti.)
Tunawashauri wateja wetu wanunue umeme wa kuanzia 3000 ili walipie kodi ya jengo 2000 na shs 1000 wapate umeme.
Imetolewa na:
Ofisi ya uhusiano na huduma kwa wateja
TANESCO
20.08.2021


Copy and paste
 
Back
Top Bottom