Sauti inakuja kichwani jiue....!!!
Sielewi ila napambana nayo kweli. Biashara zikigoma inaniambia jiue. Mahusiano yakigoma inaniambia jiue.
Maisha yakibana jiue.....
Matarajio yakifutika jiue....
Makwazo yakitokea jiue...
NA HII SAUTI IKISHINDA BASI MTU HUJIUA KWELI BILA SABABU YOYOTE YA MSINGI KIROHO NA KIMWILI.
Mimi nawakilisha vijana wengi ambao kutokana na changamoto za maisha na matokeo yake, tunasumbuliwa na sauti za ushawishi wa kujiua.
Machoni pa watu tupo very smart na hali zetu za kiuchumi sio mbaya. Ila rohoni tuna mizigo ya maumivu na hatuwezi kuonyesha in public sababu jamii haituruhusu vijana wa kiume kuonyesha changamoto zetu hadharani.
Sasa hapa ndipo sauti za kujiua zinapoanza kutuandama. Mimi ni muwazi nimesema ila vijana wengi hawasemi wanaishia kujiua.
Na ndio maana siku hizi kuna wimbi la vijana wengi kujikatisha uhai wao.
Mkuu hiyo hali ni kawaida haswa unapopitia katika hzuni kuu ya msongo wa mawazo.
Kama vijana tumepitia hiyo hali ya kuona kwamba hakuna kitu ambacho kinakupa furaha tena,unajikuta mawazo tele.
Katika hali hiyo unaona hakuna kitu kitakupa furaha tena,yani unaona dunia inaboa tu hakuna jipya na hakuna kitu utafanya ukawa excited tena.
Binafsi nilishapitia hiyo hali asee inatisha,nilipopitia hali hiyo ndipo nikaacha kuwalaumu watu wanaojiuwa kwa sababu kuna majanga yanakukuta huoni wa kumuambia.
Ila habari njema mkuu ni kwamba matatizo yote yatapita ni jambo la muda tu.
Na matatizo mengi tunayakuza sisi wenyewe yawe makubwa lakini kimsingi ni matatizo ya kawaida tu ila tunayakuza kutokana na expectation zetu.
Ndio maana mtu ukijiuwa utaandika sababu ya kujiuwa ni fulani,lakini watu wako wakisoma ujumbe ule watasema khaaa jamani si angesema tuu mbona hii sababu ni ya kawaida huwapata watu wengi ? Lskini wakati huo wewe uliyejiua umeona hiyo ni sababu kubwa sana.
Mara nyingi sana tunatamani kujiua kwa sababu tunawahofia watu ambao hata hawana mpango na sisi.
Mfano mtu vidio yake ya ngono imevuja anataka kujiua kwa kuwahofia watu watamuonaje,bila kujua kwamba watu watakudiscuss siku mbili tu alafu baadae itakuwa ni kawaida na kila mamoja atasahau within a week,ila wakati huo wewe umeshafanya maamuzi ya kudumu ya kujiua.
Hivyo mtoa mada kaa chini tafakari uangalie na ujiulize kwamba ni kweli haya matatizo ambayo yananifanya niwaze kujiua ni makubwa kiasi cha kuona kwamba solution ni kujiuwa ?
Kuna namna fulani ya kutafakari ambayo kama haujaexperience hali hii unaweza usijue ila mtoa mada kaa tena tafakari kwamba hivi haya matatizo ni mskubwa hivi ?
Nakukaribisha inbox ysngu kama utahitaji msaada zaidi.