Nasikia ushawishi wa kutaka kujiua

Nasikia ushawishi wa kutaka kujiua

Mimi namshuru Mungu kwa wema wake kupitia Kristo Yesu. Ndani ya miaka miwili nimepitia shinikizo kubwa la kiuchumi. Unaomba mbingu zimenyamaza kimya kimya kabisa. Milango yote ni kama imefungwa. Mlango niliouona upo wazi ni wa msamaha kutoka Kwa Mungu peke yake.
Nilifika mahali nikamwambia Yesu ungenipa nafasi ya kuchagua kuja dunia au kutokuja nisingechagua kuja. Namshukuru japo bado hajaifungua milango ila Nina amani na pia naamini ataifungua. Japo nimechoka ila nilimwahidi sitajiua na Kwa msaada wake nipo njema mpaka sasa hivi.
Usikate tamaa, omba toba na msaada. Damu yake itatusaidia tu.
 
Sauti inakuja kichwani jiue....!!!

Sielewi ila napambana nayo kweli. Biashara zikigoma inaniambia jiue. Mahusiano yakigoma inaniambia jiue.

Maisha yakibana jiue.....
Matarajio yakifutika jiue....
Makwazo yakitokea jiue...

NA HII SAUTI IKISHINDA BASI MTU HUJIUA KWELI BILA SABABU YOYOTE YA MSINGI KIROHO NA KIMWILI.

Mimi nawakilisha vijana wengi ambao kutokana na changamoto za maisha na matokeo yake, tunasumbuliwa na sauti za ushawishi wa kujiua.

Machoni pa watu tupo very smart na hali zetu za kiuchumi sio mbaya. Ila rohoni tuna mizigo ya maumivu na hatuwezi kuonyesha in public sababu jamii haituruhusu vijana wa kiume kuonyesha changamoto zetu hadharani.

Sasa hapa ndipo sauti za kujiua zinapoanza kutuandama. Mimi ni muwazi nimesema ila vijana wengi hawasemi wanaishia kujiua.

Na ndio maana siku hizi kuna wimbi la vijana wengi kujikatisha uhai wao.
Mkuu hiyo hali ni kawaida haswa unapopitia katika hzuni kuu ya msongo wa mawazo.

Kama vijana tumepitia hiyo hali ya kuona kwamba hakuna kitu ambacho kinakupa furaha tena,unajikuta mawazo tele.

Katika hali hiyo unaona hakuna kitu kitakupa furaha tena,yani unaona dunia inaboa tu hakuna jipya na hakuna kitu utafanya ukawa excited tena.

Binafsi nilishapitia hiyo hali asee inatisha,nilipopitia hali hiyo ndipo nikaacha kuwalaumu watu wanaojiuwa kwa sababu kuna majanga yanakukuta huoni wa kumuambia.

Ila habari njema mkuu ni kwamba matatizo yote yatapita ni jambo la muda tu.

Na matatizo mengi tunayakuza sisi wenyewe yawe makubwa lakini kimsingi ni matatizo ya kawaida tu ila tunayakuza kutokana na expectation zetu.

Ndio maana mtu ukijiuwa utaandika sababu ya kujiuwa ni fulani,lakini watu wako wakisoma ujumbe ule watasema khaaa jamani si angesema tuu mbona hii sababu ni ya kawaida huwapata watu wengi ? Lskini wakati huo wewe uliyejiua umeona hiyo ni sababu kubwa sana.

Mara nyingi sana tunatamani kujiua kwa sababu tunawahofia watu ambao hata hawana mpango na sisi.

Mfano mtu vidio yake ya ngono imevuja anataka kujiua kwa kuwahofia watu watamuonaje,bila kujua kwamba watu watakudiscuss siku mbili tu alafu baadae itakuwa ni kawaida na kila mamoja atasahau within a week,ila wakati huo wewe umeshafanya maamuzi ya kudumu ya kujiua.

Hivyo mtoa mada kaa chini tafakari uangalie na ujiulize kwamba ni kweli haya matatizo ambayo yananifanya niwaze kujiua ni makubwa kiasi cha kuona kwamba solution ni kujiuwa ?

Kuna namna fulani ya kutafakari ambayo kama haujaexperience hali hii unaweza usijue ila mtoa mada kaa tena tafakari kwamba hivi haya matatizo ni mskubwa hivi ?

Nakukaribisha inbox ysngu kama utahitaji msaada zaidi.
 
lil bow wow kuna muda alihojiwa akasema ilifika kipindi alitamani kujiua ili apate kuona inavyokuwa maana alihisi starehe zote za dunia hii amemaliza
Kwahio muda mwingine pepo kama hilo linaweza kukujia tu bila ya wewe kufahamu ni kwann
Kama una silaha ya moto kaa nayo mbali au irudishe maana ipo siku isiyo na jina utajaribu kichwani
 
Wabongo tunashindwa kuelewa umuhimu wa afya ya akili

imani potofu na dini vinatumpumbaza
Kabisa kuwa na hofu ya Mungu au kusema mtu mcha Mungu sio ndo kupata tiketi ya kuepuka mawazo ya kujiua.Wapo watu waliopata kumcha na kumhofu Mungu waliushindwa huu mtihani wa kutaka kujiua.wameenda zao ardhi imewafukia.
Tafiti zinaonyesha asilimia kubwa ya watu waliojiua hawakuwai kufikiri kama siju moja watafikia uamuzi wa kujiua.
Maisha haya si ya kujiamini sanaaaaaa
 
Ukijazwa Roho mtakatifu hutahisi huo upweke, utaona bubujiko la furaha kubwa ndani yako na utakua na amani tele, ukitaka kujazwa Roho mtakatifu wa kweli tafuta kanisa takatifu, moja lipo kisukuru, tegeta na chamazi, kwa maelekezo zaidi ni PM nikuunganishe na mchungaji
Mwambie ukweli umsaidie mwenzio kwamba Roho mtakatifu atafanyika faraja na nguvu kwake(atamtia nguvu ktk mapito yake lakini sio kwamba 100% hatahisi upweke/maumivu, anayeyapitia haya ni binadamu pia hawezi kukwepa kuhisi uchungu/maumivu/huzuni TOFAUTI akiwa na Roho mtakatifu anamsaidia kushinda matokeo mabaya ya mapito yake(kumbuka Yesu ilifika point akaomba kwa Babake kikombe kimuepuka [emoji17]na hapo ilikuwa enzi hizo sembuse nyakati hizi za hatari na vurugu nyingi
 
The same as Wanaojiua wanavyokua wanahisi!!!
Hebu acha upuuzi na kutupotezea muda hapa kutaka sympathy za kipuuzi.

Eti "kujiua", eti "wanaojiua wanavyokua wanahisi" umejuaje kama hujawahi kujiua, jinga kabisa, na kama kwenye hio dp ni ww basi mama ako alipata hasara.

Watu tunaumwa maugonjwa mazito lkn tunakomaa kuishi, halafi lipuuzo limoja linataka kujiua huku JF
 
Kuokoka ni kujiongezea majukumu mazito Sana!!kupambana na kiumbe asieonekana wakati yeye anakuona!!!

Aiseh mi nimekuwepo kwenye hiyo game muda mrefu nikaona I have to neutralize aiseh!

Life can't be serious like that my friend!!



Hili nalo neno mkuu...but life seem empty despite i hv almost everything
Eze
 
Sauti inakuja kichwani jiue....!!!

Sielewi ila napambana nayo kweli. Biashara zikigoma inaniambia jiue. Mahusiano yakigoma inaniambia jiue.

Maisha yakibana jiue.....
Matarajio yakifutika jiue....
Makwazo yakitokea jiue...

NA HII SAUTI IKISHINDA BASI MTU HUJIUA KWELI BILA SABABU YOYOTE YA MSINGI KIROHO NA KIMWILI.

Mimi nawakilisha vijana wengi ambao kutokana na changamoto za maisha na matokeo yake, tunasumbuliwa na sauti za ushawishi wa kujiua.

Machoni pa watu tupo very smart na hali zetu za kiuchumi sio mbaya. Ila rohoni tuna mizigo ya maumivu na hatuwezi kuonyesha in public sababu jamii haituruhusu vijana wa kiume kuonyesha changamoto zetu hadharani.

Sasa hapa ndipo sauti za kujiua zinapoanza kutuandama. Mimi ni muwazi nimesema ila vijana wengi hawasemi wanaishia kujiua.

Na ndio maana siku hizi kuna wimbi la vijana wengi kujikatisha uhai wao.
Omba dhidi ya sauti hizo Kwa jina La Yesu mambo yatakuwa shwari.
 
Kwasasa pesa pekee haitoshi mkuu!

Pesa inaweza kununua vinvyonunulika lakini sio vile visivyonunulika mkuu!!

Pesa haiwezi nunua upendo mkuu!!

Vile ukimtazama mkeo machoni ukaiona belongingness inaridhisha na kuleta faraja sana,kwamba you have a place deep in her!furaha ilioje mkuu!!?

Lakin Sasa ukimtazama unaona maswali kuhusu bills,shuku,na kisirani aiseh,we are just machines I say!!

Pesa sio ridhiko Tena mkuu!!

Source-trust me brooo!
Mkuu upo sahii kabisa
 
Back
Top Bottom