Nasikitika kusema kwamba, Katiba Mpya tunayoitafuta kwa nguvu nyingi haiwezi kutusaidia

Kwa hiyo inatakiwa Katiba itakayohama kunufaisha ccm ianze kunufaisha chadema?πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ Acheni upumbavu
Ha ha ha,ndo ushangae sasa,,,ukweli ni kuwa wenye majority ndo watapitisha katiba,hata hiyo katiba ikisema kiongozi wa nchi awe Putin wa Russia,,,
Democracy ni dhana pana mno
 
Nyie ndio mliungana na WAKOLONI " Uhuru Hauwezi kutusaidia" mpaka ilipofika 1961 tukaupata kwa kupewa kama zawadi .
 
Mwelevu maana yake nini wewe kisimi? sasa mtu hata kuandika hujui unataka kubishana na mimi, kiufupi una akili ya kukuwezesha kunya tuu, am done with you ***** sana.
Nitakufuatilia mpaka mwisho, niuone ufundi wa matusi yako
 
Kichwa cha habari kina tosha, haina haja ya kusoma ulicho andika, yatosha kusema wewe ni mpumbavu wa kutupwa.

Kama umetumwa kuteste mitambo, waambie waliokutuma kwamba, mpaka wavuta bange wa vijiweni wanaujua umuhimu wa KATIBA MPYA hivyo hilo jambo mutalichelewesha tu, lakini mutatupatia.
 
Hoja ni nzuri ila kwa mtazamo wangu hakuna katiba yoyote Duniani ambayo hujilinda au kijitete yenyewe. Je katiba ni nini ni mkataba baina ya mtawala na mtawaliwa. Kwa ukweli huu basi mtu yeyote atakaevunja mkataba huu anaweza kuhoji kwa njia mbalimbali. Kwa upande wa serikali itakupeleka mahakamani na utafungwa. Kwa mwananchi njia zipo nyingi ikiwemo ya kwenda mahakamani, kuandamana na kupiga kelele. Na kelele hizi ndizo unazosikia, njia moja ikishindikana wananchi watatafuta njia njingine hadi wafike mwisho hadi kutokutii serikali iliyo madarakani kama Arab springs. Hiki kilio sio cha kufumbia macho au kukitolea utatuzi wenye kebehi kwani wananchi watatufanya nini ni hatari. Majeshi hayataweza kuzuia nguvu ya umma, serikali isitoe kisingizio cha kujenga uchumi this is cheap politics zenye dalili za kudharau mwananchi ni hatari sana.
 
Nimekuelewa sana mkuu
 
Baada sasa ya kusoma ninaouita ujinga wako, twende nikuambie kitu.

Sio wa Tanzania wote ni wafuatiliaji wa hiyo Siasa yenu, hayo mambo uliyo ya orodhesha hapo hayana tija yeyote kwenye KATIBA MPYA.

Mfano mimi, tangu nimetimiza umri wa kuchagua kiongozi nimeshiriki mala moja tu 2005, baada ya hapo sikuwahi chagua kiongozi yeyote yule.

Lakini nina ham na swala la uraia wa nchi mbili, sababu nina watoto nchi jirani natamani wanangu waruhusiwe kuwa na Uraia pacha.

Natamani niione Tanzania yenye serkali moja tu, sio kama ilivyo sasa, mara Zanzibar ina Rais Tanzania kuna Rais, wakati Tanganyika sio haina Rais tu bali haipo kabisa.

Na hauwezi amini kila mtu ana mambo yake ambayo yanamfanya ahitaji KATIBA MPYA.
 
Mkuu, katiba ni imebeba masuala mengi mhimu, utaanzaje kuita ujinga kwenye suala ambalo wewe haligusii sehemu yako na wakati wewe sehemu yako ya umhimu wa katiba ni kuona inaruhusu uraia pacha pekee?

Umeshindwa kabisa kuelewa kwamba, hiyo ni sehemu ndoogo sana kati ya vitu vingi vitakavyingia kwenye katiba?

Hata hivyo, mashaka ya huu uzi ni kwa namna ipi itakuwa rahisi kuisimamia katiba na kuwajibishwa wale wote watakakuwa wakivunja katiba

Nimesema hivyo kwa sababu kuu moja tu, Karibu vipindi vingi vya uongozi vilivyopita vimewahi kuvunja katiba, lakini ni nani anayewashughurikia hao wavunja katiba, hawaonekani, isipokuwa wanakuwepo tu Mitandaoni wakiandamana

ni miaka karibu sita sasa, mikutano ya siasa imezuwiwa kinyume kabisa cha katiba yetu,

Tuna bunge lisilo halali kwa madai ya chama cha Chadema, kwamba, wapo wabunge wanaojiita ninwabunge wa kuteuliwa kutokea chadema ili hali chama hakuwatambui, huko ni kuvunja katiba ya nchi, maana katiba yetu inamtambua mbunge anayetokana na chama pekee

Hata hivyo, hakuna aliyesima kupinga na kwa kuonyesha kukasirishwa na Jambo hilo, na hakuna aliyeonyesha kumwajibisha mvunja katiba

Na kwa kuwa, Katiba haiwezi kuandamana, haiwezi kuwashitaki wavunja katiba, haiwezi kujisimamia, Je sasa, ni nani atakayekuwa jasiri wa kuandamana, au kuwapeleka mahakamani wavunja katiba, nakumbuka, sisi watanzania kwenye mambo ya kuandamana kudai haki zetu ni sawa na Mtu na C -19, mtu yuko tayari kumwona kipngozi wake akifanya atakavyo na yeye kushangilia na kupiga vigelegele hata anaponyang'anywa watoto wake ila sio kuandamana,

unalisemeaje hili mkuu
 
Suala la kuwashtaki wanaovunja katiba linaweza kutimimia tu endapo mihimili itatenganishwa. Hasa kama mhimili wa mahakama utakuwa huru.

Likitimia hilo hakutakuwa na huu upumbavu unaoendelea sasa.
 
Hawawajibishwi kwa sababu ya mhimili mmoja uliojichimbia chini.

Mihimili yote mitatu ikiwa independent huu ujinga hautakaa utokee.
 
Mkuu, jifunze kuvumilia ujinga wa wenzako kama na wao wanavyovumila upumbavu wako!
 
Naunga mkono hili wazo japo bado nataka katiba mpya. Kama tumeshindwa kumuwajibisha kiongozi anaevunja katiba ya zamani basi hata mpya ikija itavunjwa tu na hakuna kitakachotokea
 
Naunga mkono hili wazo japo bado nataka katiba mpya. Kama tumeshindwa kumuwajibisha kiongozi anaevunja katiba ya zamani basi hata mpya ikija itavunjwa tu na hakuna kitakachotokea
tuko pa1 mkuu
 
Huu mchakato uko hijacked na haohao waliokumbatia nchi. On your way ku focus kwenye elimu. Kuna watu watakuja kuwaharibia plan. They know elimu ndo solution. But they choose to ignore
 
Tatizo sio katiba. Hata katiba itungwe na malaika. Viongozi wakiamua kuwa play wanawaplay tu. Cha msingi ni kutafuta njia ya kumbananisha kiongozi akivunja katiba. Hili jambo liko very complicated na linahitaji ufikiriaji wa hali ya juu na kwa kina. Pia linahitaji mwanafalsafa ambaye si mlafi wa hela itakayoweza kumbadilisha mawazo.
 
Shida yetu kuu iko hapo chief, hata tukipata katiba nzuri kiasi gani, kama hatuna ujasiri wa kukabiliana na wavunja katiba, Tunapoteza muda tu
 
Naunga mkono hili wazo japo bado nataka katiba mpya. Kama tumeshindwa kumuwajibisha kiongozi anaevunja katiba ya zamani basi hata mpya ikija itavunjwa tu na hakuna kitakachotokea
Ya zamani imetushinda kuwajibisha viongozi wakikosea. Mpya tutaweza kweli? Cha msingi issue sio katiba. Issue ni tutaweka mfumo gani ambao utafanya kila mtu awajibike na sheria. Lakini mwisho wa siku hata kama tukipata hiyo katiba. Bado kuna swala moja ambalo ni gumu kutatulika "rushwa" kiongozi anaweza kucheza faulo. Lakini marefa( bunge na mahakama) wakapewa rushwa na wakavunga hawajaiona faulo, hata kama wananchi wakiona faulo. Bado kiongozi na timu yake ya jeshi na mahakama wanalindwa na jeshi. So mwisho wa siku wananchi mtabaki kulia tu.
Ndo maana nasema. Cha msingi hii kitu inahitaji ma genius na wana falsafa kuijadili na kutengeneza mfumo utakao kua permanent
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…