Nasikitika kusema kwamba, Katiba Mpya tunayoitafuta kwa nguvu nyingi haiwezi kutusaidia

Mwisho wa siku solution bado ni moja. Elimu bado ni jambo la msingi. Kwa sababu. Imagine watanzania wote million 55 wakawa na uelewa wa intelijensia ya siasa na elimu ya juu. Hivi nani ataweza kumdamganya nani. Hapa ndo utashuhudia mabadiliko makubwa. Ila kwa style iliyopo. Wajinga bado ni mtaji mkubwa wa wanasiasa. Wakiisha wajinga kila mtu anarudi kwenye umaskini. Kwa sababu hakuna mtu anae elimika anakubali kufanywa mtumwa " educated mind cant be enslaved"
Hii nguvu tunayotumia kupambana na wanyonyaji ni kwa sababu watu wengi hawawezi ku organize na kufikiria kitu kimoja kwa sababu ya elimu. Na wanasiasa wanapenda situation iwe hivo ili wafaidike.
 
Angalau basi kuwe na tume huru ya uchaguzi, hilo nalo lina gharimu nini nchi! Kwani Serikali haijui kuwa tume iliyopo sio huru chini ya mfumo wa vyama vingi?!
 
Umewasilisha mawazo yangu kwa namna ingine kabisa yani kama ulikuepo akilini mwangu.

Ndio maana mimi nilisema katika moja ya uzi wangu...

Thread 'Mifumo imara bila watu waadilifu sio suluhisho, jenga watu kwanza' Mifumo imara bila watu waadilifu sio suluhisho, jenga watu kwanza
 
Angalau basi kuwe na tume huru ya uchaguzi, hilo nalo lina gharimu nini nchi! Kwani Serikali haijui kuwa tume iliyopo sio huru chini ya mfumo wa vyama vingi?!
Ili tume iwe huru inatakiwa iwe na sifa gani ?
 
Watanzania hawajui kuandamana, hawajui kudai haki yao, wao wanaamini tu kwamba, Mungu ndiyo kila kitu.

Hivi kwa nini kweli tunahangaishana kudai katiba?
Ndoma huko kwa mswati,watu wanamtoa kwa nguvu

Ova
 
Katiba ya sasa inaruhusu maandamano na mikutano ya siasa, si ndiyo jamani?

Mbona mambo yakienda kombo, watu hawaandamani nchini?

Mbona wanasiasa wa upinzani hawafanyi mikutano ya kisiasa ya nje wakati katiba inaruhusu?

Ukipata majibu ya hayo maswali, ndo utagundua, chanzo cha matatizo ya Watanzania ni katiba au hilo jibu la maswali ya hapo juu!
 
Hahaha.

Naunga mkono hoja kwamba tatizo sio katiba.

Tatizo ni watu.

Kwa sababu kuna mengi ambayo wapinzani wanakubali kikatiba lakini hayafanywi.
 

Inawezekana ukawa na ushauri wa msingi kuwa cdm wanyamaze. Tuje kwenye uhalisia, je ni mara moja au 2 umewahi kusikia mtu akifanya madai stahiki ya kundi lao na kuambiwa kuwa anatumika? Makundi ya dhahiri ndani ya nchi hii ni wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara, je makundi haya umewahi kuyaona yakimudu kutetea maslahi yao, zaidi ya kuwataka wanasiasa wawatetee?

Hayo niliyokutajia ni makundi ya wazi kabisa ambayo ndio wanaoendesha nchi hii. Je makundi haya yana umoja wowote wa wazi, au wana platform ya pamoja ya kuongelea mambo ya utawala wa nchi hii, zaidi ya kila kundi kuongelea maslahi yao, ambayo hata hayo maslahi ya makundi yao huyapata kwa shida? Je kuna dalili yoyote ya makundi hayo kudai katiba ya nchi? Je kwa hili hii ya wanasiasa kudai katiba mpya, makundi hayo yanaonyesha kuwa hayaitaki katiba mpya? Tusitake kupotoshwa na ccm kuwa katiba mpya iachwe idaiwe na makundi ambayo, hata madai yao yanasubiri wanasiasa ndio wawasaidie kuyadai.
 

Hayo makundi wasio mashabiki wa cdm unayajuaje? Ni lini hayo makundi yataanza kuidai hiyo katiba mpya? Katiba hii ya mwaka 1977 hayo makundi yote ndio yaliidai mpaka ikatengenezwa? Acha upotoshaji usio na msingi wowote.
 

Uko sahihi kabisa kwenye hii nadharia yako, hiyo elimu kuhusu katiba nani anapaswa kuitoa? Ni lini unategemea watu watoe hiyo elimu ya katiba na wapi, zaidi ya hawa hawa wanasiasa? Na je, kuna mtu yoyote amekukataza ww ama wanaoamini kwenye hii nadharia yako kutoa elimu ya katiba? Ama hii kutoa elimu ya katiba ni dhana yako, lakini unataka watu wengine ndio waitekeleze?
 

Katika kitu kinapaswa kutoacha kupigiwa kelele ni haya madai ya katiba mpya. Hakuna hata kushiriki uchaguzi wowote mpaka katiba mpya yenye kutenda haki ipatikane. Inatakiwa hata hao viongozi watakaochaguliwa bila katiba mpya kususiwa, mfano sasa hivi watu hawajitokezi kwa wingi tena kupiga kura, maana hawana imani tena na mwenendo wa uchaguzi. Kwahiyo tunatakiwa tuende mbali zaidi hadi kususia hao viongozi ikibidi hata kuwazomea.
 
Wakina mbowe wanataka katiba mpya itakayo waingiza madarakani.
CCm wanataka katiba hii hii itakayo waacha madarakani? Huu ujinga wa kuona katiba kama nyaraka ya uchaguzi mtauacha lini?
 
Shida yetu kuu iko hapo chief, hata tukipata katiba nzuri kiasi gani, kama hatuna ujasiri wa kukabiliana na wavunja katiba, Tunapoteza muda tu

Ni hivi boss, tunaitaka hiyo katiba mpya ambayo pia itaendelea kuvunjwa. Lakini iko siku watu watasimama kudai katiba hiyo itekelezwe. Kwasasa tuipate hiyo unayoamini haitatekelezwa, kisha kutakuwa na kizazi cha kuhakikisha katiba hiyo inatekelezwa.
 
Kwa maswali yako Chief, hapa tatizo siyo katiba, Tatizo ni Sisi watanzania
 
Ngoja leo tusikilize hoja za madai ya katiba,pengine tunaweza tukapata pa kuanzia
 
Na huu ndo unatakiwa kuwa msimamo wa taifa katiba ni hitaji la nchi sio hisani ya kiongozi fulani kuamua kitu hata nicha kijinga basi Kiko sawa hapana
Nadhani pia, utaratibu wa upatika aji wa katiba ukifanikiwa, kuwekwe kipengele kingine kitakachoondoa sauti ya Raisi kwamba, Wananchi watakapoona Katiba yao inamapungufu na wanataka katiba iundwe upya tena, kusihitajike sauti ya Raisi kuamua iandikwe au la, Ni kuachwe kipengele cha kupiga kura kuanzishwa katiba nyingine, wananchi watapiga kura, na hizo kura zikifikia kiwango kitakachoruhusiwa kuandikwa katiba zikitimia, mtu yeyote asiseme eti achwe ajenge sjui nini ndio aone katiba kama itaandikwa
 
Naunga mkono hili wazo japo bado nataka katiba mpya. Kama tumeshindwa kumuwajibisha kiongozi anaevunja katiba ya zamani basi hata mpya ikija itavunjwa tu na hakuna kitakachotokea
Nani wa kuwawajibishwa hao wanaivunja katiba sasa?

Watu wengi mnashindwa kulijibu hili swali ndio maana hamuoni umuhimu wa katiba mpya.
 
Ukifanikiwa kutenganisha mihimili ya nchi hakuna ujinga utaendelea.

Kwa katiba ya sasa Raisi anachagua majaji.

Sasa unategemea nini hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…