Hii lugha ya CHADEMA kupewa serikali inatokea wapi? Unajua chama cha siasa kinapataje dhamana ya kuongoza nchi na kuunda serikali? Tunasema Tanzania ni nchi ya kidemokrasia. Basi wananchi ndio wenye mamlaka ya kuchagua viongozi wao kupitia uchaguzi huru na wa haki. Kwa namna hiyo chama kinachopata kura nyingi zaidi za uRais ndicho huunda serikali.
Si ajabu ukiwa CCM huwezi kufahamu hilo baada ya miaka mingi ya kujitwalia madaraka kwa nguvu ya vyombo vya dola kinyume na kura halali za wananchi. Ndio maana mnaamini katika kupeana serikali !
Yote uliyoandika yatawekwa sawa na katiba makini ya taifa. CHADEMA wanapigania kuandaliwa kwa katiba mpya itakayohakikisha uongozi wa nchi unazingatia misingi ya demokrasia, utawala bora, utawala wa katiba na sheria, utawali wa haki. Katiba hiyo ndiyo itakayodhibiti utendaji wa viongozi wanaokuwa madarakani.
Kwa akili yako unafikiri ni kiongozi aliyeko madarakani ndiye atakayemua kila kitu: akae madarakani muda gani, amteue nani na kumfukuza nani kwa mapenzi yake, auze rasilimali za nchi kama anavyopenda. Hayo ni mambo ya CCM inayong'ang'ania Rais ndiyo aendelee kuwa na madaraka ya kuteua kila mtendaji na kutumia rasilimali za nchi kama anavyotaka.
Huo ni uchambuzi mfu. Halafu haya mambo ya kupeana tuwaachie waKenya. Hata wao siku hizi hawafanyi hivyo kwenye siasa labda kwenye mambo ya mitaani. Kinachotakiwa Tanzania ni uchaguzi huru na wa haki ili wananchi waamue wenyewe kama CHADEMA wanafaa au hawafai kuongoza nchi. Tunatakiwa kuachana na huu ujinga wa kufikiria nani anafaa au hafai kuongoza. Hiyo ni kazi ya wananchi kuamua.