Sasa mimi sijaelewa hebu nifafanulie. Yaani kuna njemba ina ndevu unaisikia inakupumulia kisogoni au huwa inakuwaje?!
Maana isije ikawa ni mkeo anakukumbatia usiku ila wewe kwenye ndoto unapata hisia umekumbatiwa na mwanaume mwenzako.
Ila swali la msingi zaidi, mimi siamini sana katika maswala ya ushirikina au popo bawa stuffs..... Upande wa pili naamini ni illusions tu zinakuwa zimetawala kichwa chako. Na illusions ni matokeo ya fikra iliyopo ndani ya subconscious yako.
Sasa swali ni kwamba je, wewe fikra za kubambiwa au hiyo nightmare ya kubambiwa inatokana na tukio gani katika maisha yako kihistoria?!
Its probably one of your personal wars unazopigana ndani ya nafsi.
Hakuna historia ya mtu mzima wakati wa utoto wako kutaka kukufanyia molestation ukiwa mdogo na sasa ile worst memory inakurejea?!
Sababu kuna watoto unakuta chini ya umri wa miaka 10 kuna ndugu bazazi alikuwa akilala nae usiku alikuwa anamchezea sehemu za siri au kumfanyia vitendo vya kingono, kwa mtoto hayo mambo kama aidha alihisi au aligundua anafanyiwa ila sababu ya utoto alishindwa kuelewa nini kinaendelea then akiwa mkubwa ile fikra au kumbukumbu ya lile tukio huwa inakuja tena na kutaka kufanyiwa clarification yaani ufafanuzi wa nini kilikuwa kinatokea na iwe fikra mtambuka na sio fikra tu isiyo na maana.
Hebu jaribu kukumbuka, enzi za utoto wako, someone hakukuwahi kukufanyia vitendo vyenye sexual intent ndani yake?! Jaribu kukumbuka ndugu, jamaa, rafiki yaani mtu yoyote wa utotoni ambaye kwasasa ukikumbuka tukio mojawapo unashindwa kuelewa lilikuwa ni tukio la aina gani ila kwako kwa sasa ni tukio la mashaka sana.
Hebu kumbuka, jaribu sana kukiuliza kichwa chako kinakukumbusha nini kilichowahi kukukuta.