Natabiri jaribio lolote la kubadilisha Katiba na ukomo wa Rais litaibua mazito

Uganda haina utamaduni wa marais kuheshimu term limits.

Tanzania tangu aondoke Nyerere marais wote wameheshimu term limits.

Na hata Magufuli amesema hatazidisha muhula wake.

Sasa huu mchecheto wa kusema Magufuli ataongeza muda unatokea wapi?
 
Magufuli ameshasema hataongeza muda wakubaki madarakani baada ya 2025 acha hofu.
 
Lengo la JIWE ni kuendelea kutawala baada ya 2025 ,ndio maana anajenga IKULU dodoma ili akaendelee kujinafasi huko,wewe unadhani anamjengea RAIS wa 2025-2030? Sarakasi zote za Biashara ya utumwa lengo ni kuondoa wapiga kelele pindi akianza kuchezea katiba.

Kwa mwendo wake wa KUKUSANYA MABILIONI through manunuzi nakwambia mpaka 2024 wapinzani wengi watakuwa washafanya BIASHARA ya UTUMWA....Sugu washaanza kumtia jamba jamba ya kumbomolea HOTEL yake ,lengo wamfilisi ili aunge mkono JUHUDI.
 
Katiba itabadilishwa na kutakua shwari Kama ilivyokua ktk uchaguzi huu. Siku Magu anaapishwa nchi nzima ilikua busy na mapokezi ya bi Zari na Diamond.

Kwa aina ya raia wa nchi hii Magu atatawala hadi mola wake atakapomtwaa.
Ninakubaliana nawe kwa asili mia kubwa.
 
Kwa Tanzania hii nayoifahamu? Ambapo hata lissu na mbowe wana kadi za ccm! Hebu kuwa siliazi kidogo.
 
Yupo wapi Ben saa nane??Siku hizi na wewe umekuwa wa kulia lia
Vipi mkuu? Umepotea Sana jukwaani kwema lakini?

Hizo tuhuma za kumpoteza Saanane mtoa mada amekuwa akizikanusha sana, kwanini hamuamini utetezi wake?
 
Hata kama humuamini Magufuli, unatakiwa kutomuamini kimantiki.

Ama sivyo, unaweza kubakia unajadili speculations za ajabu.

Kwa mfano.

Je, ni sawa kujadili kwamba Magufuli ataiuza ardhi ya nchi yote iwe koloni la China, kwa sababu tu Magufuli haaminiki?

Where do you draw the line?

Magufuli kashasema hataongeza muda, mnataka afanye nini zaidi muamini hataongeza muda?
 
Wakuu, hivi ikifika 2025 halafu Magufuli akajistaafia zake mtasemaje?

Mtaomba msamaha kwa kumsingizia makosa ambayo hajayafanya?

Tuwekane sawa, maana hizi nyuzi zinadumu na zinaweza kufika 2025.
 
Ningeomba sana akusome uliyemjibu na akuelewe ulichomjibu.

Ahsante sana kwa kuliandika hili kiurahisi hivi ili lieleweke na yeyote akusomae.
 
Aah wapi!! Mipango kama ipo ya kuongeza muda ipo, kama haipo hata zikipigwa kilele haipo. Siasa na utawala wa taifa ni mikakati sio mihemko kama ya kina wasanii au mwanamziki yoyote, na hii mada inasemwa semwa sababu kuna wanufaika wanataka iwe hivyo, na kutokea inawezekana hatakama muhusika kasema hataki.
Kuna tofauti kubwa kati ya kuongoza na kuwa celebrity. Mfano wa Mziki wa jaakiss sijui kiss haufit kwenye mazingira haya ya siasa na utawala.
 
Mkuu haujaelewaa hoja yake? Anamaanisha kwamba Raisi atakuwa SAMIA (mwanamke),baada ya Mungu kutovumilia ushenzi wa huyu aliepo Sasa( Sasa sijui akiongea nae[emoji848]).Bawacha hawana hoja ya msingi, ukute yeye ndo atatangulia [emoji23][emoji23]

nimemwelewa sana,anajifanya ana uchungu usioelezeka[emoji23][emoji23].
 
Hilo shairi la Jadakiss ni fasihi, sasa kama huelewi fasihi, kuelewa ni vigumu.

Hapa kuna mambo mawili.

1.Speculation/ ubashiri
2. Fact

Kwenye speculation na ubashiri hakuna mpaka, unaweza kutunga lolote.

Unaweza kusema 2025 tutagundua Magufuli ni mumiani aliyetoka sayari ya Zuhura.

Hakuna anayeweza kupinga hili kwa fact, kama ambavyo huwezi kuthibitisha kwa fact.

Kwa sababu hatujafika 2025.

Halafu kuna facts.

Tuna facts gani za kuonesha Magufuli ataendelea na urais baada ya 2025?

Magufuli amesema hilo? Hapana. Alichosema ni kukanusha hilo.

Magufuli ameanzisha mchakato huo? Hakuna ushahidi wowote.

Sasa mchecheto huu kuhusiana na hadithi zisizo na msingi unatokea wapi?
 
Ulais kazi nzito ngumu niombeeni kwa mngu nisijawe kiburi, sitoongeza muda wa kutawara
 
Ok, mm sipo vizuri kwenye mambo ya fasihi za muziki hivyo sawa.
Mchecheto upo unaweza kuwa na sababu kuu mbili.. Kwanza ni kuweka presha kama kuna kusudio la kuongeza muda, au kupima upepo juu ya kusudio la kuongeza muda.
 
Fahamu tu kuhusu haya machache.
1. Hakuna Dikteta aliyebadilisha katiba ili kuongezewa muda akawa analiongea hilo suala kabla. Mara zote hukana au kukaa kimya wakati vuguvugu likishika kasi. Wanaolisema huwa ni wapambe wa watawala.

2. Suala hili limekuwa likipigiwa debe na viongozi waandamizi na wateule wa Magufuli kwa muda mrefu sasa, na hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua za kinidhamu na Magufuli mwenyewe wala na CCM.

3. Jambo linalosemwa semwa na watu tofauti tofauti kwa nyakati tofauti kuwa linapangwa kutokea, maana huo mpango upo au huenda ukawepo tu nyuma ya pazia. Watu husema kile wanachokiona, kukisikia au kukihisi.
 
Wakuu, hivi ikifika 2025 halafu Magufuli akajistaafia zake mtasemaje?

Mtaomba msamaha kwa kumsingizia makosa ambayo hajayafanya?

Tuwekane sawa, maana hizi nyuzi zinadumu na zinaweza kufika 2025.
Mkuu tunapenda iwe hivyo lakini kwa plan za JIWE sidhani ila ikitokea 2025 akastaafu itakuwa ajabu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…