Putin Sina tabu naye sana lakini nawaza TU kuwa Kwa Nini asiendeleze mazungumzo ya kidiplomasia badala yake akaamua kuua ndugu zake ambao Wana asili Moja ?
Kuna wapumbavu na malofa wanaojaribu Kulinganisha uvamizi wa Marekani Kwa Libya au Irak na huo uvamizi wa Urusi Kwa Taifa la Ukrein. Ni upofu na ushabiki TU lakini Kuna tofauti kubwa sana.
Kwanza tunasahau kuwa Libya na Iraki zilikua zinatoa vitisho vya mara Kwa mara vya Kuishambulia Israel na kuifuta kwenye Ramani ya Dunia. Jambo ambalo lingeleta vita kubwa. Na pia magaidi walikua wanawashambulia sana wamarekani Kwa muda mrefu na walikua wanapata ufadhili Toka Libya na Iraki. Kuna watu watasema kuwa zilkua propaganda za Marekani ,lakini Libya na Iraki zenyewe ndizo zilikua zinajiloga Kwa kutangaza hadharani kuwaunga mkono magaidi na kuitishia Israel Kwa kufanya majaribio ya silaha zao Kwa lengo la kuifuta Israel.
Sasa bila kupendelea upande wowote ni wazi kuwa Israel isingekubali kuondolewa kwenye Ramani ya Dunia Kwa kusubiri mpaka walipuliwe au hata kufanyiwa majaribio.
Lakini Libya na Iraki kama zingefanya maendeleo yao bila kuweka vitisho kwa nchi nyingine na kuwasapoti magaidi ili wawaue wamarekani kila wanapowaona bila shaka hakuna nchi ingewashambulia na kuwaondoa Marais wao madarakani.
Hata Iddi Amini alipigwa Kwa sababu ya kuitishia kuiangamiza Tanzania na kuchukua mkoa wa Kagera na Kisha Mwanza na baadae kuweka Bendera yake Dodoma. Uchokozi na vitisho vya wazi Kwa Israel ndio uliopelekea Libya kupigwa.
Suala la Palestina ni la muda Mrefu na Israel Wana haki Kwa upande mmoja na wapo tayari kuishi na wapalestina lakini wanahofia kuuawa Kwa kuviziwa na maroketi. Kama Wapalestina wangejichanganya na kuacha siasa za itikadi Kali za kujitoa mhanga nadhani hata Israel wangeishi kama watu wa kawaida TU na maisha yangesonga lakini kama Kuna wanaowaona kama wavamizi wasio na haki itakua ni ubaguzi usioisha. Ni sawa na kuwabagua Kwa wazi wamarekani weusi miaka ya nyuma ilivyokua ni shida na uhasama Kwa miaka mingi mpaka walipoanzia kuwatambua kama wamarekani wengine ndipo kidogo uhasama ukapungua.
Libya pia ilikua inashutumiwa Kwa kuua wapinzani wake kama panya.
Iraki pia Sadamu alikua anawaua wapinzani wake kama panya Kwa kutumia mabomu ya sumu. Ukrein ilikua ni nchi isiyo na vitisho Kwa majirani au Raia wake na ndio maana hata watanzania wengi wamesoma Huko. Ilikua ni nchi Nzuri na isiyo na ubaguzi wa wazi wa kidini kama ilivyokua Libya.
Libya chini ya Gadaff ilijaribu kumsaidia Iddi Amini ili aivamie na kuiangamiza Tanzania wakati Tanzania haikua na uadui na Libya.
Laana ya Libya kujaribu kuwaangamiza watanzania kupitia Idi Amini ilimtafuna mpaka Marekani ilipoamua kuisambaratisha Nguvu ya Libya na kuiacha ikiwa inayumba mpaka Leo.
Siungi mkono uvamizia wowote unaoondoa uhuru wa watu kidemokrasia.
Ni rahisi Kwa Muafrika wa dini yoyote na kabila lolote kwenda kuishi Marekani Kwa uhuru na Kwa amani kuliko kwenda kuishi Urusi. Urusi ni makauzu.
Dunia ni Mali ya Mungu na Mtawala aliyepewa mamlaka ya kutawala kuanzia mbinguni na Mwana wa Adam. Putin anatakiwa aachane na Vita na vitisho vya kuiangamiza dunia Kwa Moto wa mionzi ya Nyuklia. HATA Mungu aliapa kuwa hata Iangamiza Dunia Kwa Moto na Kwa Maji mpaka Kiama.b