Natafuta mwanaume wa kujenga naye familia❤

Habari wana JamiiForums,

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 35, nipo kwenye hatua ya maisha ambayo ningependa kukutana na mwanaume mwenye mtazamo wa ndoa na kujenga familia.

Ninayemtafuta ni mwanaume mwenye umri wa miaka 38–45, Mkristo, mwenye heshima, uaminifu, upendo, hekima na anayejua anachotaka katika maisha.

Kwa upande wa familia, ningependelea mwanaume km ana watoto wasiozidi wawili.

Sina haraka ya kuingia kwenye uhusiano kwa sababu ya kuwa tu kwenye uhusiano. Ningependa kwanza tufahamiane vizuri, tujenge mawasiliano yenye heshima na kuona kama tunalingana kimtazamo, kitabia na katika malengo ya maisha. Ikiwa Mungu akipenda, lengo liwe ndoa na familia yenye amani na upendo.

Mwanaume mwenye nia ya dhati na anayejiona kwenye maelezo haya, karibu tuanze kufahamiana. 😊❤️

Asanteni.
1791022027610.png
 
Ukipata mwanamke aliyemaliza mambo yake katika umri huo, ukimweka ndani anaweza kutulia

Muhimu afute akaunti zake zote za mitandao ya kijamii na umbadirishie namba ya simu

Kila la heri kwa waoaji 🙏🙏

I will marry when I want ~ ñgugí wa thingó
 
Habari wana JamiiForums,

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 35, nipo kwenye hatua ya maisha ambayo ningependa kukutana na mwanaume mwenye mtazamo wa ndoa na kujenga familia.

Ninayemtafuta ni mwanaume mwenye umri wa miaka 38–45, Mkristo, mwenye heshima, uaminifu, upendo, hekima na anayejua anachotaka katika maisha.

Kwa upande wa familia, ningependelea mwanaume km ana watoto wasiozidi wawili.

Sina haraka ya kuingia kwenye uhusiano kwa sababu ya kuwa tu kwenye uhusiano. Ningependa kwanza tufahamiane vizuri, tujenge mawasiliano yenye heshima na kuona kama tunalingana kimtazamo, kitabia na katika malengo ya maisha. Ikiwa Mungu akipenda, lengo liwe ndoa na familia yenye amani na upendo.

Mwanaume mwenye nia ya dhati na anayejiona kwenye maelezo haya, karibu tuanze kufahamiana. 😊❤️

Asanteni.
Mungu akupe wepesi ,
 
  • Thanks
Reactions: 627
Wanawake wa aina yako mara nyingi huishia tu kuchezewa na wahuni na baadaye kutupwa dampo. Kwa sababu hadi unafikia huo umri wa miaka 35 umeshakutana na wanaume wengi tu! Wazuri na wabaya. Bahati mbaya ulishindwa kufanya uchaguzi sahihi. Kwa hiyo usitegemee utapata chaguo sahihi kwa wakati huu.
Mkuu usimkatishe tamaa, anything can happen, cha msingi awe Tu makini
 
Kuna badhi ya wanaume ni malimbukeni sana. Kosa la kutoolewa mapema sio la mwanamke mwanamke ataolewa na nani mapema wakati sisi hatuoi tunazalisha tu?🤣 hata hivyo miaka hii ndoa sio issue sana muhimu uwe na maisha tu
 
Je, wewe ni mshangazi uliye jipata?

Maana wanasema bila hela huna uzuri wa aina yoyote
 
  • Thanks
Reactions: 627
Mwambie Mungu akuongoze upate mwenza alie mwema wa tabia, watu wanaweza kuigiza kama malaika ukishaingia ndani wanakiwasha, na hapo umeingia gharama, Ndugu na jamaa wanajuwa kwamba wewe ni mke wa mtu fulani, unaanzaje kujitowa huko na umri umeenda. Mtangulize Mungu wako.
 
Habari wana JamiiForums,

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 35, nipo kwenye hatua ya maisha ambayo ningependa kukutana na mwanaume mwenye mtazamo wa ndoa na kujenga familia.

Ninayemtafuta ni mwanaume mwenye umri wa miaka 38–45, Mkristo, mwenye heshima, uaminifu, upendo, hekima na anayejua anachotaka katika maisha.

Kwa upande wa familia, ningependelea mwanaume km ana watoto wasiozidi wawili.

Sina haraka ya kuingia kwenye uhusiano kwa sababu ya kuwa tu kwenye uhusiano. Ningependa kwanza tufahamiane vizuri, tujenge mawasiliano yenye heshima na kuona kama tunalingana kimtazamo, kitabia na katika malengo ya maisha. Ikiwa Mungu akipenda, lengo liwe ndoa na familia yenye amani na upendo.

Mwanaume mwenye nia ya dhati na anayejiona kwenye maelezo haya, karibu tuanze kufahamiana. 😊❤️

Asanteni.
Kwa umri huo tafadhali badilisha lengo isiwe NDOA tu, maana katika umri wako wato huko nyuma uli focus na ndoa ikashindikana maana sina uhakika kama hawakupatikana wanaume wema na wazuri kwako lakini ukweli ulio mchungu kwa sasa wanaume wanaojielewa wakisikia mwanamke anakazia habari za ndoa, ndoa, ndoa wanapata mashaka huenda kuna mambo anajaribu kuyaficha anataka kuharakisha mambo.

Pili mindset za wanawake wa ki afrika zime base kwenye ndoa kama suluhisho la matatizo yote katika maisha ya wawili, wakati wengi hajajipanga kwenda kutumikia hizo ndoa kama wake/mke na si wanawake.

Ila all the best mwanetu 😀
 
Back
Top Bottom