Umetoa boko TateWanawake wa aina yako mara nyingi huishia tu kuchezewa na wahuni na baadaye kutupwa dampo. Kwa sababu hadi unafikia huo umri wa miaka 35 umeshakutana na wanaume wengi tu! Wazuri na wabaya. Bahati mbaya ulishindwa kufanya uchaguzi sahihi. Kwa hiyo usitegemee utapata chaguo sahihi kwa wakati huu.
Uko sahihi watu wanaolewa na miaka 60 (nina ushuhuda kwenye hili) sembuse miaka 30'sHuenda mpaka 35 bahati yake ilikuwa bado. Mama yangu mdogo aliolewa akiwa 40 ila hakuwa na mtoto. Wapo mpaka dadika hii na mume wake yeye yupo 78 sasa
Sawa. Utuambie sasa kama una mtoto/watoto, au huna. Kwa maana umeongelea habari za watoto wawili wa mwanaume pekee. Kuficha ficha mambo siyo vizuriHii umeitoa wapi? Kuna amri au sheria inayosema ukifika umri fulan hupaswi kuoa au kuolewa , Mtu anaolewa au kuoa akiwa na huo utayar na sio umri fulani
Upo mkweli!Uko sahihi watu wanaolewa na miaka 60 (nina ushuhuda kwenye hili) sembuse miaka 30's
Wenye bastola aka mguu wa Kuku pia tuje?Habari wana JamiiForums,
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 35, nipo kwenye hatua ya maisha ambayo ningependa kukutana na mwanaume mwenye mtazamo wa ndoa na kujenga familia.
Ninayemtafuta ni mwanaume mwenye umri wa miaka 38–45, Mkristo, mwenye heshima, uaminifu, upendo, hekima na anayejua anachotaka katika maisha.
Kwa upande wa familia, ningependelea mwanaume km ana watoto wasiozidi wawili.
Sina haraka ya kuingia kwenye uhusiano kwa sababu ya kuwa tu kwenye uhusiano. Ningependa kwanza tufahamiane vizuri, tujenge mawasiliano yenye heshima na kuona kama tunalingana kimtazamo, kitabia na katika malengo ya maisha. Ikiwa Mungu akipenda, lengo liwe ndoa na familia yenye amani na upendo.
Mwanaume mwenye nia ya dhati na anayejiona kwenye maelezo haya, karibu tuanze kufahamiana. 😊❤️
Asanteni.