Nataka kufanya DNA test ya watoto wa kaka kupitia mimi je inawezekana?

Watoto wametoka kufiwa baba yao, halafu tena familia inataka kuanza kuwahangaisha😭

Kama baba yao hakuona haja ya kuwapima hao watoto DNA, kwa nini wao watake kuwapima? Shida ni nini?

Kimsingi jamaa aongeze nyama ili apewe ushauri unaoeleweka, ila kwa content aliyotoa, bado hakuna sababu ya msingi ya kupima hao watoto DNA.
Ndio maana jamaa anataka kuwapima watoto DNA huenda hata Baba yao bado yupo hai.
 
Thamini sana familia yako na mke wako ukiwa hai angalau wajivunie walikuwa na baba na anawapenda na kuwajali hawa ndugu sio wa kuwaamini sana ukishakufa ndio mambo kama haya hutokea mara hawa watoto sio kama damu yetu mara vile mishowe watatelekezwa wawe ombaomba.

Mimi nawaonea huruma hao watoto tu isee
Kama mama alijifanya majanja akawa anachepuka wacha avune alichopanda.

Tunahendekeza ujinga Africa kwa sababu Mtu anafanya mambo kwa kujua hawezi kuwajibika nayo.

Watu wameamka. Mambo ya kumlaza mtu usiku kucha anabembeleza Mtoto sio wake yanafika mwisho.
 
Mwaka jana nimefiwa na kaka yngu na ameacha watoto 4 watatu wako primary ila kuna jambo kidgo limenipa hofu kama inawezekana ili nijiridhishe.

Kifupi hawa watoto wote kwa sasa hivi mimi ndio mlezi wao kwa kila kitu, ni sehemu ya familia yangu na mama yao ilibidi tumbakishe nyumbani kwajili ya kusaidia ulezi sababu jamaa bado ni wadogo.

Nisiende mbali sana nataka kufanya DNA kwahawa watoto kupitia mimi au babu yao je! Inawezekana?
Inaelekea unataka kudhulumu hao watoto mali ya baba yao hakuna kingine hapo. Baba yao aliwatambua wewe ni nani uwakatae. Mungu anakuona
 
Mleta mada ameelemewa na mzigo wa kulea watoto 4 pamoja na Mama yao mpaka akili ikawaza kua isije ikawa analea watoto ambao sio wa Kaka yake,

Mpaka hapo nampongeza sana kwa kujitwisha hilo jukumu na kwa moyo huo,
Kupima DNA ni sahihi,kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe,unaweza kuhangaika nao halafu wakisha kua wakubwa wanakuja kuonyeshwa Baba yao mzazi,halafu yanakufika yale yale yaliyomfika Baba yake Diamond.
 
Kwanini marehemu asiwapime kwenye uhai wake?
Je wewe alikuachia usia na kukuambia wapime?
Na je kama sio wa kwenu utawapeleka wapi?
Mkuu najua umasikini ni mbaya sana
Lakini kama una uwezo wa kuwalea walee tu maana hukuwazaa wewe
Aliewakubali kafa
Au tumuulize mjane
 
Ndivyo inavyokuwa.....Mtoto ambaye hujamzaaa bora umlee ukijua unajitolea tu.

La usije ukale ukijua ni wako. Siku utakapojua ukweli unakufa siku hiyo hiyo.

Watu wawe responsible kwa matendo yao.
 
Kwanini marehemu asiwapime kwenye uhai wake?
Je wewe alikuachia usia na kukuambia wapime?
Na je kama sio wa kwenu utawapeleka wapi?
Mkuu najua umasikini ni mbaya sana
Lakini kama una uwezo wa kuwalea walee tu maana hukuwazaa wewe
Aliewakubali kafa
Au tumuulize mjane
Mbona mnaingilia Mambo ya Kifamilia?
 
Mwaka jana nimefiwa na kaka yngu na ameacha watoto 4 watatu wako primary ila kuna jambo kidgo limenipa hofu kama inawezekana ili nijiridhishe.

Kifupi hawa watoto wote kwa sasa hivi mimi ndio mlezi wao kwa kila kitu, ni sehemu ya familia yangu na mama yao ilibidi tumbakishe nyumbani kwajili ya kusaidia ulezi sababu jamaa bado ni wadogo.

Nisiende mbali sana nataka kufanya DNA kwahawa watoto kupitia mimi au babu yao je! Inawezekana?
Unauthibitisho wa hilo jambo limelokufanya utake DNA test?

Nikuhakikishie, hata ukipima majibu yatatoka kwamba watoto wote ni damu yenu.
 
Kwanini marehemu asiwapime kwenye uhai wake?
Je wewe alikuachia usia na kukuambia wapime?
Na je kama sio wa kwenu utawapeleka wapi?
Mkuu najua umasikini ni mbaya sana
Lakini kama una uwezo wa kuwalea walee tu maana hukuwazaa wewe
Aliewakubali kafa
Au tumuulize mjane
  1. Kwanza hapa hatuna uhakika kama marehemu aliwapima au hakuwapima hao watoto wakati wa uhai wake
  2. Sasa hivi mleta mada ndio responsible wa malezi ya hao watoto pamoja na Mama yao,so anao uamuzi wa kujiridhisha,isije ikawa anachukua majukumu ya mtu mwingine,
  3. Akisha jua kua hao watoto sio wa kwao,uamuzi utakua ni wake,aidha awapeleke wakalelewe na Baba yao au awalee kwa kujitolea tu huku akiwa na uhakika kua hao watoto sio damu yao
Ifike mahali watu wawe responsible kwa matendo yao na sio tu kutanguliza huruma tu,kwanza ingewekwa sheria kabisa,kabla ya mtoto kupewe Birth certificate ni lazima apimwe DNA ili huko mbeleni isije kutokea sintofahamu kama hii,kuna tofauti ya kumlea mtoto kwa kujitolea na kumlea mtoto huku ukijua kua ni damu yenu na kumbe sio damu yenu.
 
Ila #3 Baba kaishatangulia mbele
Lakini ni maamuzi ya mtu na mtu
Na ni ushauri mzuri kama umeshuku kwamba mke alikuwa mama huruma
 
Watoto wametoka kufiwa na baba yao, halafu tena familia inataka kuanza kuwahangaisha😭

Kama baba yao hakuona haja ya kuwapima hao watoto DNA, kwa nini wao watake kuwapima? Shida ni nini?

Kimsingi jamaa aongeze nyama ili apewe ushauri unaoeleweka, ila kwa content aliyotoa, bado hakuna sababu ya msingi ya kupima hao watoto DNA.
Katika masuala ya msingi huwa hatuleti huruma huruma hizi huruma na kuleta ubinadamu madhara yake makubwa mbeleni.. Nyie mnaokuja na comment zenu za aina hii mnakera sana.. nini maana ya uvumbuzi wa VIpimo vya DNA? unalea mtoto ukijua ni wa ndugu yako kumbe wa jamaa mwingine bora ifahamike sio damu yake au damu yake

Usirudi Nyuma.. Nenda kushughulikie DNA
 
Kwa namna moja au nyingine najaribu kumuelewa mtoa mada......unajua haya mambo yanakuwa mepesi kuyatolea majibu ikiwa hujakutana nayo..........

Wanasema Siri ya ndani ya mtungi aijuaye kata.......hatujui kayaona mazingira gani yaliyoipa mashaka nafsi yake.........

Kama hayo mazingira uliyoyaona yameendana na dhana yako kwa asilimia kadhaa basi wewe kamwe hutakuwa na amani nafsini mwako.........

Hata ukisema ulipuuzie lakini daima litaganda moyoni mwako.......

Mwisho wa siku wewe ndio mwenye maamuzi ya mwisho ya kubeba hayo machungu......
 
  1. Kwanza hapa hatuna uhakika kama marehemu aliwapima au hakuwapima hao watoto wakati wa uhai wake
  2. Sasa hivi mleta mada ndio responsible wa malezi ya hao watoto pamoja na Mama yao,so anao uamuzi wa kujiridhisha,isije ikawa anachukua majukumu ya mtu mwingine,
  3. Akisha jua kua hao watoto sio wa kwao,uamuzi utakua ni wake,aidha awapeleke wakalelewe na Baba yao au awalee kwa kujitolea tu huku akiwa na uhakika kua hao watoto sio damu yao
Ifike mahali watu wawe responsible kwa matendo yao na sio tu kutanguliza huruma tu,kwanza ingewekwa sheria kabisa,kabla ya mtoto kupewe Birth certificate ni lazima apimwe DNA ili huko mbeleni isije kutokea sintofahamu kama hii,kuna tofauti ya kumlea mtoto kwa kujitolea na kumlea mtoto huku ukijua kua ni damu yenu na kumbe sio damu yenu.
Uko sahihi katika hili...... lakini hoja yako inakinzana na mitazamo ya kiimani........

Unaanzaje kumuambia aliyekuja kumuangalia mwanae aliyezaliwa kuwa anatakiwa apimwe DNA kuthibitisha nasaba yake na mtoto....???

Majibu yoyote yatakavyokuwa lakini lazima yataacha nyufa kwenye mioyo ya wanandoa.......hakuna tena atakayemuamini mwenzie.....
 
Back
Top Bottom