Nataka kufanya DNA test ya watoto wa kaka kupitia mimi je inawezekana?

Nataka kufanya DNA test ya watoto wa kaka kupitia mimi je inawezekana?

Mimi nitajibu maswali yako tu.

Je, inawezekana? Jibu ni Ndiyo.

Kisha nakurudishia swali, una uhakika wewe na kaka yako ni watoto wa baba mmoja? Huna.

Kitakachotoa majibu sahihi ni DNA za marehemu kaka yako na watoto. Je, unaweza kupata DNA za marehemu, jibu ni NDIYO.

Hayo mengine yabaki juu yako.

Wewe ndio umejibu swali inavyotakiwa.
Hawa wengine naona wanaendeshwa na mihemko
 
DNA anaweza kufanya mtu yeyote lakini kwa scenario yako lazima ukubaliane na matokeo tena ujiandae kwelikweli sababu kadhaa;

1. Yawezekana kakako alitunza watoto sio wake na hakuwa anafahamu sijui kama wewe upo tayari kwa haya majibu.
2. Yawezekana watoto ni wa kaka yako lakini wewe sio kaka yako kwa maana mama hako alimpiga baba yako either wewe au kakako huyo sio baba yenu maana DNA inatoka kwa baba.

Sasa je upo tayari kwa haya matokeo? Kama upo tayari basi tafuta Wakili atakuelekeza cha kufanya na gharama za huduma nzima kwa Mkemia Mkuu na Legal fees za Wakili.
 
Hamjamuelewa tu mleta mada. Halaf mna shauri mpaka mnapitiliza.
Kauliza swali dogo tu, inawezekana au haiwezekani.

Kitandawil alicholenga kukitegua indirectly hapa ni je kama mimi na kaka yangu ni baba mmoja means tuna DNA zinafanana, je watoto wetu nao DNA zitafanana na either of us???

Swali lake (japo hajataka kuliweka hivyo) ni kwamba ,kwenye family tree ya familia au ukoo flan DNA ya great great grand father aliye source ya hiyo family itakua ni sawa na DNA za watoto wooote walio zaliwa na watoto wa kiume wa hiyo koo???

Kwa maana nyingine, ukiondoa watoto wa waliozaliwa na watoto wa kike wa ukoo au family fulan, je ukoo mzima unaweza kuwa na DNA moja tu determined by muanzilishi wa huo ukoo au family??

Mleta mada mimi nimeku study na kukuelewa kuwa hii wewe ndio concern yako, ndio maana hukuishia kuji reffer wewe tu bali ukamuingiza na babu mtu.

Nawasilisha bwana Wakuperuzi .
Uko sahihi mkuu Ivan Stepanov wakati mwingine unaweza kuwa hujaeleweka au ni kawaida ya jf kukutna na majibu tofauti eidha kwa makusudi au kwa wachangiaji kutokukuelewa ila pmj na hayo kuna baadhi ya michango nimeipenda na nimeamua kuifanyia kazi
 
Mwaka jana nimefiwa na kaka yngu na ameacha watoto 4 watatu wako primary ila kuna jambo kidgo limenipa hofu kama inawezekana ili nijiridhishe.

Kifupi hawa watoto wote kwa sasa hivi mimi ndio mlezi wao kwa kila kitu, ni sehemu ya familia yangu na mama yao ilibidi tumbakishe nyumbani kwajili ya kusaidia ulezi sababu jamaa bado ni wadogo.

Nisiende mbali sana nataka kufanya DNA kwahawa watoto kupitia mimi au babu yao je! Inawezekana?
huwezi
 
Moja kwa moja inaonyesha una tamaa na mjane wa kaka yako,umemtongoza kakukataa umeanza gubu,punguza huo ushetani
Hi moja kwa moja inaonyesha hauna mahusiano mazuri na ndugu wa mume wako..Cha msingi achana na hayo mawazo uliyoambukizwa ishi nao vizuri acha ubinafsi na uroho

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kwnz ungeanza kupima DNA yako wewe na hyo marehemu kaka yako,,
Huenda ikawa hata nyie sio ndugu halali wa damu.

Wacha kusumbuwa watoto yatima.
 
Inawezekana, kama mnashare mama na baba watoto watakuwa na robo ya DNA yako... Kama mnashare mama tu watakuwa na nusu ya robo
 
Alafu unakuta ya na brother wake sio damu moja.... izi mambo ni za kuridhi oooohhj
Yeah, unakuta mtu na kaka yake siyo damu moja... Mama alifanya maujanja Enzi zako... Sasa sijui atafukuza watoto au ataendelea kulea.
 
Mwaka jana nimefiwa na kaka yngu na ameacha watoto 4 watatu wako primary ila kuna jambo kidgo limenipa hofu kama inawezekana ili nijiridhishe.

Kifupi hawa watoto wote kwa sasa hivi mimi ndio mlezi wao kwa kila kitu, ni sehemu ya familia yangu na mama yao ilibidi tumbakishe nyumbani kwajili ya kusaidia ulezi sababu jamaa bado ni wadogo.

Nisiende mbali sana nataka kufanya DNA kwahawa watoto kupitia mimi au babu yao je! Inawezekana?
Unataka kugundua nini haswa? Paternity issue? Huwa kama ni paternity despute DNA inakuwa na maana kama unafanya comparison kati ya baba wawili au zaidi.

Unaweza kupata majibu flani lakini kwa hali yako kama utawapima watoto wote pengine ili kujua kama wote ni wa baba mmoja na ukiweka DNA yako inaweza kusaidia kutoa clue fulani ila wewe na marehemu kaka yako muwe wote ni watoto wa baba mmoja na mama mmoja.
 
Mwaka jana nimefiwa na kaka yngu na ameacha watoto 4 watatu wako primary ila kuna jambo kidgo limenipa hofu kama inawezekana ili nijiridhishe.

Kifupi hawa watoto wote kwa sasa hivi mimi ndio mlezi wao kwa kila kitu, ni sehemu ya familia yangu na mama yao ilibidi tumbakishe nyumbani kwajili ya kusaidia ulezi sababu jamaa bado ni wadogo.

Nisiende mbali sana nataka kufanya DNA kwahawa watoto kupitia mimi au babu yao je! Inawezekana?
Kama umeamua kuwalea lea tu ndugu.
Mambo ya DNA ya nini?
Unajua maridhiano yao na kaka yako marehemu?
Kitanda hakizai haramu
 
Back
Top Bottom