Nataka kufanya DNA test ya watoto wa kaka kupitia mimi je inawezekana?

Nataka kufanya DNA test ya watoto wa kaka kupitia mimi je inawezekana?

  1. Kwanza hapa hatuna uhakika kama marehemu aliwapima au hakuwapima hao watoto wakati wa uhai wake
  2. Sasa hivi mleta mada ndio responsible wa malezi ya hao watoto pamoja na Mama yao,so anao uamuzi wa kujiridhisha,isije ikawa anachukua majukumu ya mtu mwingine,
  3. Akisha jua kua hao watoto sio wa kwao,uamuzi utakua ni wake,aidha awapeleke wakalelewe na Baba yao au awalee kwa kujitolea tu huku akiwa na uhakika kua hao watoto sio damu yao
Ifike mahali watu wawe responsible kwa matendo yao na sio tu kutanguliza huruma tu,kwanza ingewekwa sheria kabisa,kabla ya mtoto kupewe Birth certificate ni lazima apimwe DNA ili huko mbeleni isije kutokea sintofahamu kama hii,kuna tofauti ya kumlea mtoto kwa kujitolea na kumlea mtoto huku ukijua kua ni damu yenu na kumbe sio damu yenu.
Mimi naunga mkono hoja yako.

Tufika mahali tuache ujanja ujanja kwenye Mambo Muhimu ya Kifamilia.

Israeli kokote unakozaa mtoto lazima apimwe DND kwanza kama ni Myahudi.

Kama hauko serious kwenye swala la familia utakuwa serious kwenye Nini?

Wahindi na Warabu wamejizatiti hakuna kuzaa hovyo hovyo na mtu mweusi kwa sababu watu weusi hawajali mstakabali wa Maisha yao.

Kwa Muhindi utaoa au kuolewa tu na yule ambaye familia imeridhia uwe unampenda au humpendi lazima utii Wazazi.

Na kwakweli tunaona wanafanikiwa sana kwenye maswala ya kifamilia na Uchumi Pia.
 
Mwaka jana nimefiwa na kaka yngu na ameacha watoto 4 watatu wako primary ila kuna jambo kidgo limenipa hofu kama inawezekana ili nijiridhishe.

Kifupi hawa watoto wote kwa sasa hivi mimi ndio mlezi wao kwa kila kitu, ni sehemu ya familia yangu na mama yao ilibidi tumbakishe nyumbani kwajili ya kusaidia ulezi sababu jamaa bado ni wadogo.

Nisiende mbali sana nataka kufanya DNA kwahawa watoto kupitia mimi au babu yao je! Inawezekana?
Acha kukimbia majukumu mkuu lea watoto wa bro

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Ila mtoa mada unafurahisha
Sasa unaomba ushauri ili usaidiwe lakini apo apo unasema Kuna stori nyuma ya pazia
Asa watu watakupaje ushauri ulio sahihi wakati kiini cha iyo stori yako hutaki kuisema apa
hapo inatakiwa aelezee hiyo sintofahamu yake imetokea wapi mpaka kufikia uamuzi huo. Sasa sijui sasa tutamshaurije wakati hatujui hata kiini cha story yake.
 
Mwaka jana nimefiwa na kaka yngu na ameacha watoto 4 watatu wako primary ila kuna jambo kidgo limenipa hofu kama inawezekana ili nijiridhishe.

Kifupi hawa watoto wote kwa sasa hivi mimi ndio mlezi wao kwa kila kitu, ni sehemu ya familia yangu na mama yao ilibidi tumbakishe nyumbani kwajili ya kusaidia ulezi sababu jamaa bado ni wadogo.

Nisiende mbali sana nataka kufanya DNA kwahawa watoto kupitia mimi au babu yao je! Inawezekana?
Kaka yako ndio alipaswa kuwapima DNA, Kama hakufanya hivyo walee kama mlivyoachiwa, Watoto ni zawadi pekee toka kwa MUNGU.
 
Uko sahihi katika hili...... lakini hoja yako inakinzana na mitazamo ya kiimani........

Unaanzaje kumuambia aliyekuja kumuangalia mwanae aliyezaliwa kuwa anatakiwa apimwe DNA kuthibitisha nasaba yake na mtoto....???

Majibu yoyote yatakavyokuwa lakini lazima yataacha nyufa kwenye mioyo ya wanandoa.......hakuna tena atakayemuamini mwenzie.....
Mwanzoni italeta madhara hayo uliyoyaeleza ila huko mbeleni wana ndoa watakaa kwenye mstari,sio leo hii mke anazaa na mwanaume mwingine halafu anambambikia mumewe,

Transition yeyote hua ngumu mwanzoni but mbeleni faida zake huonekana,ifike wakati hawa wanawake wanao bambikia wanaume watoto wawe responsible kwa upumbavu wao.
 
Ila #3 Baba kaishatangulia mbele
Lakini ni maamuzi ya mtu na mtu
Na ni ushauri mzuri kama umeshuku kwamba mke alikuwa mama huruma
Baba katangullia mbele ya haki ila jukumu la malezi ya watoto na Mama yao lipo kwa mtu ambae yupo hai,
Tukitanguliza huruma basi hili tatizo la wanaume kubambikiwa watoto halitokwisha,

Msaliti hua hasamehewi hata siku moja,hakuna huruma kwa msaliti,usiwaangalie hao watoto tu bali angalia na unyama wa huyo Mama kumbambikia watoto mume wake (Kama majibu ya DNA yatatoka kua sio watoto wake)
 
Ni taira huyu jamaa... mambo ya familia is very sensitive sio yakuingilia fargha za watu na kuhatarisha maisha ya watu na viumbe visivyo na hatia
Haya mambo yanahitaji ujasiri na umakini mkubwa sana, unaweza dhani unatatua tatizo kumbe ndo unaongeza tatizo zaidi...
 
Baba katangullia mbele ya haki ila jukumu la malezi ya watoto na Mama yao lipo kwa mtu ambae yupo hai,
Tukitanguliza huruma basi hili tatizo la wanaume kubambikiwa watoto halitokwisha,

Msaliti hua hasamehewi hata siku moja,hakuna huruma kwa msaliti,usiwaangalie hao watoto tu bali angalia na unyama wa huyo Mama kumbambikia watoto mume wake (Kama majibu ya DNA yatatoka kua sio watoto wake)
Kweli kabisa nimekuelewa, ila usaliti umezidi sana siku hizi sijui sababu ni nini
Enzi za mwalimu tulikuwa tunasikia kwa nadra sana na mtoto anajulikana kabisa ila Baba anaelea anaendelea na ndoa
Najua kuna kijana alizika Baba zake wawili (how)
Mmoja alipokulia kama baba mzazi akiishi nae na ndugu zake
Na mwingine aliechepuka na mama yake na kuzaliwa yeye
Lakini siku hizi unaona watoto wote sio wa hapo daa
Kweli kuna shida mahali
Dunia imeharibika sana
 
Kama umestuka mkuu fanya DNA test maana haiwezekani watoto wazaliwe wasifanane hata pua, macho, miguu, vidole, tembea, e.t.c na kaka yako.

Na ndo maana ya DNA(Vina saba) lazima kuwepo na Inherited traits. Sasa unakuta mtoto hufanani nae stuka.Achana na zilipendwa sijui huyu mtoto anafanana na ujombani, sijui ushangazini achana na hizo mambo unapigwaa...! Thats your blood lazima vitu achukue toka kwako..🤣

Hii tabia ya kubambikiwa watoto ipo sana unakuta unalea katoto kana tabia tofauti kabisa unaanza kujiuliza mbona kwenye ukoo wetu hakuna mtu mwenye tabia hizi.

Wakuu tulee damu Zetu. Mimi mwanamke akisema ooh niliteleza nisamehe huyu mtoto sio wako kwahiyo hapo unaweza kuamua kulea au kuachana maana kakuambia ukweli.

Lakini kubambikiwa hapana. Almanusura nibambikiwe 2 kids maana nikawa najiuliza mbona hawa watoto siwaelewi elewi na hawafanani na mtu yoyote kwenye ukoo wetu na sina ile real love kama yule wa kwanza ambaye nafanana nae mpaka kucha, tembea, cheka e.t.c. Ndo nikaanza kufatilia na kujua ukweli dakekii nilichokutana nacho alafu wanawake wengine wanakuchezea/ushirikina ili usije ukajua chochote.
Watchout wekeza nguvu kwenye Damu yako.
 
Kaka yako ndio alipaswa kuwapima DNA, Kama hakufanya hivyo walee kama mlivyoachiwa, Watoto ni zawadi pekee toka kwa MUNGU.
Aah wapi! Kuna vitu vingine unaweza kuja kujipa mzigo..mtoto pekee ninae ona ni zawadi toka kwa Mungu ni yule/wale uliyo ambiwa ukweli kwamba baba fulani hapa niliteleza huyu mmoja sio wako, sasa hapo ndo roho wa Mungu anaweza kukugusa na ukaamua kulea huku ukiwa na Inner peace.

Lakini hawa wa kubambikiwa huku mama mtu anapiga kimya na anawasiliana kisiri na baba mtoto huko na kuchukua hela za matumizi kabisa sio sahihi kabisa na wakati mwingine mbele ya safari umeshawekeza nguvu zako kumsomesha mtu bila kujua na mwisho wa siku umekorofishana na mama yake ndo sasa anaanza kufunguka ukweli kuwa huyo mtoto kwanza sio wako. Si hata Mauaji yanaweza tokea.? HOW DOES THAT FEEL?wewe kama wewe?

MUNGU USIMSINGIZIE, MUNGU ANAPENDA UKWELI SASA KAMA MAMA MTU HAJASEMA UKWELI WAKE MIAKA YOTE HIYO ALAFU UNASEMA ZAWADI TOKA KWA MUNGU, HUYO MUNGU NI WA WAPI?

NB; Zingatia neno "ukweli" lazima kuwe na maafikiano baina ya pande mbili ndo hapo roho wa Mungu anaweza kugusa na ukalea.
 
Ila mtoa mada unafurahisha
Sasa unaomba ushauri ili usaidiwe lakini apo apo unasema Kuna stori nyuma ya pazia
Asa watu watakupaje ushauri ulio sahihi wakati kiini cha iyo stori yako hutaki kuisema apa
Acheni umbea sema kama unajua
Akipima yeye kwa niaba ya ndugu yake inafaa? Basi mengine mwachieni mwenyewe
Akitaka atawashirikisha mumshauri
 
Mwaka jana nimefiwa na kaka yngu na ameacha watoto 4 watatu wako primary ila kuna jambo kidgo limenipa hofu kama inawezekana ili nijiridhishe.

Kifupi hawa watoto wote kwa sasa hivi mimi ndio mlezi wao kwa kila kitu, ni sehemu ya familia yangu na mama yao ilibidi tumbakishe nyumbani kwajili ya kusaidia ulezi sababu jamaa bado ni wadogo.

Nisiende mbali sana nataka kufanya DNA kwahawa watoto kupitia mimi au babu yao je! Inawezekana?
Mkuu awali ya vyote pima wewe na baba yako kama kweli kaka yako ni ndugu yenu, ndo huanze kushughurikia au dogo, hapo kwanza nyie kwa nyie mnaweza mkapotezana, fanya wakika kwanza wenu ndo uingize hao third party,.......mambo ya DNA sio ya kuchezea chezea tena Tanzania maabara haziko accurate utaumia bure na kuumiza watoto.
 
sasa hapo itakuwa majanga, manake huyo anamdhania ni kaka yake si ukute wala sio kaka yake wa damu, mama alipitako naye, unaenda pale unapima DNA inasoma negative kumbe ni negative kwasababu wewe sio kaka wa damu wa huyo bro, althogh watoto ni wa bro kiukweli.
 
Back
Top Bottom