Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Mafuta yana faida ila kwa mtaji wa roli moja au mawili usijaribu.Mafuta ni risk na short zikitokea wakati wa kushusha ni hasara ya transporter, bei za tela za tenki zipo juu.

Ukitaka upate ahueni kama una gari chache kubali kufanya joint venture na kampuni kubwa zenye tenda ili na wewe uingize gari zako na kupata mafuta ya kupeleka nje(Transit)

Kama unavutiwa kusafirisha mafuta upate tenda za ndani(local) kwenye sheli za mikoani za watu binafsi ambayo hawana gari.
 
Thanks[emoji120]
 
Sio muandishi mzuri bali naomba nichangie kidogo kwa uzoefu niliopata baada ya kuamua kuingia kwenye hiyo biashara 2011 to 2015.
1. Nilisajili kampuni na kupata investor Exemption TIC, unapata break kubwa ya kodi na zoezi likaanza.

2. Tuliagiza gari 4 na tela 4 Daf XF 3 flatbed trailer na 124 moja yenye tela ya tiper. 124 ilikuja single excel ikaongezwa hapa bongo kwa gharama ya 5M kila kitu.

3. Kazi ikaanza mwaka wa kwanza ulikuwa sio mbaya kazi zilikuwepo na madereva wa mwanzo walikuwa wanajielewa ikawa angalau si haba dola zilikaa mkononi. Shida ikaanza baada ya kuondoka kurudi ninapoishi nje ya Tanzania hapo madereva na wasimamizi ikaanza shughuli nzito madereva wakaondoka na kuanza na madereva vishoka hali ikawa tete nikaamua kuuza Daf zote nikabaki na 124 tipper nikatafuta kampuni ya ujenzi nikaingia now mkataba wa kazi na kuacha majukumu kwa mtu wa kusimamia hiyo tu.
My point.
Gari ya kuanza nayo kama unataka kusogea tafuta 124L haitakuangusha kama utaihudumia vizuri, unawezanunua single excel ukaongeza excel bongo maana kununua single ni bei chini na zipo nyingi europe.
Pia kama unataka kuingia kwenye hii biashara ni kweli pesa ipo sana ila unahitajika kujitoa kwenye hiyo biashara 120% hakikisha gari imepakia mzigo bandarini usimuamini agent, Ukiweza safiri mpaka nchi za jirani kutana na ma agent na jenga nao ukaribu na muaminiane sana.
Dereva makini ndio mtaji na mafanikio yako ,kama ukipata dereva mzuri basi mtunze na muhudumie kama nyumba ndogo yako sababu utapata return kwake ya kuhudumia chombo kinachompa mazuri yote unayompa.
Mwisho Nasisitiza hili. Muda wako wote ujitoe kwenye hiyo kazi na uwepo wako ndio mafanikio yako.
Mimi ilinishinda kutokuwepo sehemu ya tukio ila kwa biashara ni nzuri sana ,ingawa sasa hivi kidogo ina misukosuko ya hapa na pale lakini muda utapita itarudi kama zamani.
Nipo njia kuirudia 2026 kunapo uhai.
Asanteni.
 
Biashara magari labda uwe dereva mwenyewe, hakuna watu hatari kama Madereva. Watakufilisi.

Kama alivyopata hasara yule Mama wa roli moja lililotumbukia mto Wami.
Ni uzembe wa dereva kuto kuhakiki mfumo wa Upepo ktk hilo lori.

Kama alikuwa na mtaji mdogo ndo keshafirisika hapo.
Madereva afadhali na ugonjwa wa Corona.
 
Kwa local naomba nikusahihishe route ya Dar-Mza ni $43 to $47 per ton unless uwe inabeba mizigo ya international company ndio unaweza kupata $70..... Which is also rare for the owner of single truck.
 
Kuna kampuni kama sikosei ni Overland walikuwa wakitoka Zambia kama wanarudi tupu basi gari moja itabeba horse za gari 2, na nyingine itabeba tela za gari 2.
Horse ndio nini?

Nimesikia brigedia general aliyeopoa Scania la Mama mto Wami anasema engine na Cabin vimepotea, chasis na horse vimepatikana. Horse ni nini? Thanks.
 
Horse ndio nini?

Nimesikia brigedia general aliyeopoa Scania la Mama mto Wami anasema engine na Cabin vimepotea, chasis na horse vimepatikana. Horse ni nini? Thanks.

Horse au Tractor Unit ni kichwa cha roli kinachotumika kuvuta tela la mzigo.
Cabin ni sehemu ya kuendeshea na dereva kupata kupumzika au kulala.
Hiyo chini ni Horse ya Scania yenye Day Cabin. Cabin hii haina kitanda cha kulala.
 

Attachments

  • images (2).jpeg
    20.2 KB · Views: 29
  • images (2).jpeg
    20.2 KB · Views: 29
Horse au Tractor Unit ni kichwa cha roli kinachotumika kuvuta tela la mzigo.
Cabin ni sehemu ya kuendeshea na dereva kupata kupumzika au kulala.
Hiyo chini ni Horse ya Scania yenye Day Cabin. Cabin hii haina kitanda cha kulala.

Horse haiwezi kuwa ndio tractor unit au kichwa kinachovuta trela kama unavyodai kwa sababu:

Mkuu wa kamandi za wahandisi wa kijeshi kikosi cha NYUMBU PROJECT, aliyeagizwa na Mkuu wa Majeshi ya Wananchi kwenda kuopoa Scania la Mama wa mto Wami, Brigedia Generali Mhandisi Mwandamizi Hashim Yusuph Komba, amesema wamefanikiwa kuokoa CHASIS na HORSE lakini ENGINE na CABIN vimezolewa na mto, havikupatikana!

Na Cabin ndimo mule mbele anamolala dereva, na ndio kichwa..

KICHWA cha Scania kimepotea.
HORSE imepatikana.
Kwa hiyo KICHWA sio HORSE.

HORSE ni nini ???


 
Maelezo ya Offshore yako sahihi 100%
 
huenda mkuu wa kamandi za uhandisi alipitiwa tu kidogo japokuwa tamko lake halibadili ukweli juu ya maana ya horse!

Horse ni combination ya cabin na complete chassis mahususi kwa ajili ya kuvuta semi trailer/interlink(tela zisizo na ekseli mbele).

Sent from my SM-J105H using JamiiForums mobile app
 
Kwanini asibebe mkaa????????????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…