Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Utaipata kwa bei hio sababu ya Connections ulizonazo au negotiations skills mkuu?Hujakosea mkuu, ila tu gari ambayo wewe unainunua kwa milion 30 mie naweza kuipata kwa milion 20.
Mafuta yana faida ila kwa mtaji wa roli moja au mawili usijaribu.Mafuta ni risk na short zikitokea wakati wa kushusha ni hasara ya transporter, bei za tela za tenki zipo juu.
Ukitaka upate ahueni kama una gari chache kubali kufanya joint venture na kampuni kubwa zenye tenda ili na wewe uingize gari zako na kupata mafuta ya kupeleka nje(Transit)
Kama unavutiwa kusafirisha mafuta upate tenda za ndani(local) kwenye sheli za mikoani za watu binafsi ambayo hawana gari.
Ushauri huu auweke moyoniNunua mende ya mchanga.. Iweke Dar.. Nadhani kipande ni laki tatu kwa siku.. Usisahau kukatia bima kubwa.. Tafuta gari iliyo chini ya kilomita laki saba.View attachment 1484231
Ipo na gharama zake zipo chini ya millionSi unaweza kufunga security camera ya kisiri ambayo ipo linked na simu unaona live kama gari ina mzigo au la? Ni wazo tu sijawahi kuona lakini naamini kuna technolojia hii.
Mfano: Amazon product ASIN B07CL3M4BY
Haswaa mkuu!Utaipata kwa bei hio sababu ya Connections ulizonazo au negotiations skills mkuu?
Hiyo ni bei ya Cement mwanza au gharama ya kubeba mfuko mmoja wa cement mpaka mwanza?
Horse ndio nini?Kuna kampuni kama sikosei ni Overland walikuwa wakitoka Zambia kama wanarudi tupu basi gari moja itabeba horse za gari 2, na nyingine itabeba tela za gari 2.
Horse ndio nini?
Nimesikia brigedia general aliyeopoa Scania la Mama mto Wami anasema engine na Cabin vimepotea, chasis na horse vimepatikana. Horse ni nini? Thanks.
Horse au Tractor Unit ni kichwa cha roli kinachotumika kuvuta tela la mzigo.
Cabin ni sehemu ya kuendeshea na dereva kupata kupumzika au kulala.
Hiyo chini ni Horse ya Scania yenye Day Cabin. Cabin hii haina kitanda cha kulala.
Haiwezi kuwa bei ya kubebea, ni bei ya kuuziaHiyo ni bei ya Cement mwanza au gharama ya kubeba mfuko mmoja wa cement mpaka mwanza?
Maelezo ya Offshore yako sahihi 100%Horse haiwezi kuwa ndio tractor unit au kichwa kinachovuta trela kama unavyodai kwa sababu:
Mkuu wa kamandi za wahandisi wa kijeshi kikosi cha NYUMBU PROJECT, aliyeagizwa na Mkuu wa Majeshi ya Wananchi kwenda kuopoa Scania la Mama wa mto Wami, Brigedia Generali Mhandisi Mwandamizi Hashim Yusuph Komba, amesema wamefanikiwa kuokoa CHASIS na HORSE lakini ENGINE na CABIN vimezolewa na mto, havikupatikana!
Na Cabin ndimo mule mbele anamolala dereva, na ndio kichwa..
KICHWA cha Scania kimepotea.
HORSE imepatikana.
Kwa hiyo KICHWA sio HORSE.
HORSE ni nini ???
maelezo ya Offshore yako sahihi 100%
huenda mkuu wa kamandi za uhandisi alipitiwa tu kidogo japokuwa tamko lake halibadili ukweli juu ya maana ya horse!Horse haiwezi kuwa ndio tractor unit au kichwa kinachovuta trela kama unavyodai kwa sababu:
Mkuu wa kamandi za wahandisi wa kijeshi kikosi cha NYUMBU PROJECT, aliyeagizwa na Mkuu wa Majeshi ya Wananchi kwenda kuopoa Scania la Mama wa mto Wami, Brigedia Generali Mhandisi Mwandamizi Hashim Yusuph Komba, amesema wamefanikiwa kuokoa CHASIS na HORSE lakini ENGINE na CABIN vimezolewa na mto, havikupatikana!
Na Cabin ndimo mule mbele anamolala dereva, na ndio kichwa..
KICHWA cha Scania kimepotea.
HORSE imepatikana.
Kwa hiyo KICHWA sio HORSE.
HORSE ni nini ???
Kwanini asibebe mkaa????????????Wakuu,
Niseme machache.
Marehemu Rugemalila Mutahaba aliwai kusema maneno haya, naomba kumnukuu" Ukifanya biashara na haikupi changamoto basi hiyo biashara haina faida achana nayo"
Akaenda mbali tena, Mjasiriamali wa kweli ni yule anayebadilika badilika huwez kukomaa na biashara ya aina moja tu kwa wakati wote, Mwisho wa nukuu.
Hii biashara ina changamoto zake lakini ina pesa, sehemu yeyote yenye changamoto pesa inapatikana hapo.
Scania 113M ni horse nzuri lakini ina mapungufu yake, hii gari haitumii umeme mwingi na ulaji wake wa diseal ni mkubwa, lakini pia haina Kitanda.
Kwa mfano trip ya Dar -Lubumbashi, halafu Lubumbashi - Dar hiyo gari inatumia diseal lita 2400 na muda mwingine mpaka 2500 wakati scania 114L, 124L inakula lita 2200.
Kwa ushauri wangu, unaweza kuanza na scania 114L yenye horse power 380 cabin ndogo. Au ukishindwa sana basi chukua DAF XF 95 manual, (camis engine)
View attachment 1484869
View attachment 1484870
Kama nilivyosema awali, Dereva ndiye mtu muhimu sana atakaye kutoa hapo ulipo mpaka sehemu uliyopanga wewe kufika. Tatizo kubwa kwenye hii biashara wamiliki wengi wanamchukulia dereva kama barmaid.
Dereva mzuri unampataje? Madereva wazuri siku zote wanaibwa kutoka kwenye makampuni mengine.
Tengeneza mofolojia ya kazi yako vizuri, kwa mfano kuna kampuni X inamlipa dereva mileage ya kwenda Lubumbashi na kurudi dar TSHS 1milion
Kiaje? Dereva anapewa shs 500k kwenda Lubumbashi na anavyoingia Mgodini kupakia copper unampatia dola 100, akirudi dar unampa shs 300k kama return mileage. Sasa dereva kama huyo kwanini asiheshimu kazi na kutunza gari lako vizuri..!
Kwenye hii kazi reporting ni muhimu sana, mwenye mzigo wake anataka kujua gari iko wapi na imelala wapi? Sasa ili uweze kwendana na hii ari huna budi kutengeneza Kanuni ambayo itakuwa kama katiba ya kazi ofisini kwako.
Dereva aanze safari saa moja asubuhi na ikifika saa kumi na mbili jioni apaki gari atafute guest alale na atume ujumbe kwako kukupa report. ( Kuwa mkali sana kwa dereva anayepuuzia hili)
Madhara ya kutembeza gari usiku ni makubwa sana na yanaweza kukufilisi kabisa na ukajuta kwanini uliingia kwenye hii biashara ya magari kama wanavyoelezea wadau hapo juu.
Breakdown, jitahidi sana kuepuka hitilafu za njiani, funga spare za uhakika ambazo utaweza zipata sub-scania au kwenye maduka mengine ambayo yako vizuri.
Na unapopata breakdown najua kichwa kinawaka moto na pressure inakuwa juu, jitahidi sana kujicontrol, pokea simu ya agent aliyekupakilisha mzigo au mteja mwenyewe mwambie ukweli na umpe uhakika wa usalama wa mzigo wake na uhakika wa kutoka hapo ulipo nasa.
Kutokupokea simu za hao watu kutakuharibia sana na siku nyingine utashindwa aminiwa na ukizingatia ndiyo kwanza unaanza.
Kwenye hii biashara tuna utatu mtakatifu, ambao ni Dereva, Agent / Wakala wa mizigo na Fundi wako wa gari, Hawa watu ishi nao vizuri, kuwa nao karibu kushindwa mchepuko wako.
Chonde chonde usiruhusu lori lako kubeba mkaa, (kama ni kagunia kamoja basi akamwagie maji ndiyo akabebe)
Rate za mizigo sokoni huwa zinabadilika kutoka na ari ilivyo kwa wakati huo na kabla ya kumpatia agent nyaraka zako za gari basi jiridhishe kwa kufanya utafiti kidogo wa bei maana nao ni watafutaji kama wewe.
Shukrani sana!
Muwe na jumapili njema iliyobarikiwa