Nataka nikusanye kiasi cha million 25, nitumie mbinu gani?

Unataka kusave kwa muda gani? Kama unataka kusave kwa miaka 10. Fanya hivi. Nenda UTT, fungua akaunti ya mfuko wa Ukwasi (Liquid Fund). Weka TZS 100,000 kila mwezi, hakikisha hutoi. Wana riba ya 13%. Save kwa miaka 10. Baada ya miaka 10 utakua na TZS 24,400,000.

Ambapo ungeamua tu kusave kwenye saving account ya bank, baada ya miaka kumi ungepata TZS 12,000,000. Ambapo pia ingekatwa kiasi kidogo kwa kukutunzia pesa yako.

Kazi Kwako
 
Matarajio ni miaka mitatu au minne
 
Then kwa hoja yako hii ni upi uwezekano wa kupata pesa nyingi ya pamoja kuanzia 20M maana ukikisanya ki laki 9 unasema iwekezwe hujui kuna tofauti za malengo.
 
A stock is the memory of the history of changing flows within the system.
Stocks change over time through the actions of a flow. Flows are filling and draining, births and deaths, purchases and sales, growth and decay,
deposits and withdrawals, successes and failures. A stock, then, is the present memory of the history of changing flows within the system.

Donella H Meadows
Think in Systems
 
Hii situation yako iko clear kabisa—tatizo siyo kipato, tatizo ni mfumo wa kusave na namna unavyolinda hiyo pesa.
Kwanza tukubaliane ukweli mmoja: kwa kipato cha 500k–800k, kufikisha 25M inawezekana, lakini siyo haraka bila discipline kali au kuongeza kipato.
Hesabu ya moja kwa moja: Ukisave 200k kwa mwezi → utahitaji zaidi ya miaka 10
Ukisave 300k kwa mwezi → kama miaka 7
Ukisave 400k kwa mwezi → kama miaka 5
Ukisave 500k kwa mwezi → kama miaka 4
Sasa tatizo lililokukwamisha kwenye kikoba siyo kikoba, ni haya mambo mawili:
Hukuweka emergency fund, hivyo shida ilipotokea ukaingia kwenye akiba
Pesa ilikuwa rahisi kuifikia, ukaanza “kukopa” mwenyewe
Ukishindwa kudhibiti haya mawili, hata ukipata mshahara mkubwa bado utashindwa kusave.
Sasa hii ndiyo njia sahihi ya kufanya:
Anza kwa kugawanya kipato chako vizuri. Kwa hali yako:
50% matumizi
30% savings
20% akiba ya dharura (emergency fund)
Usijilazimishe kuanza juu sana. Anza hata na 200k–300k kwa mwezi lakini uwe consistent.
Hatua ya pili, tengeneza emergency fund kwanza. Hii ni muhimu kuliko hata hiyo 25M. Lengo liwe angalau miezi 3 ya matumizi yako. Kama unatumia 300k kwa mwezi, basi uwe na kama 900k–1M pembeni. Hii itakuzuia kuvunja savings kila shida ikitokea.
Hatua ya tatu, linda pesa yako. Usirudie kosa la kikoba. Tafuta sehemu ambayo si rahisi kutoa pesa:
Fixed deposit ya benki
SACCO yenye masharti magumu ya kutoa
Akaunti tofauti ambayo huna access ya haraka
Lazima kuwe na ugumu fulani kuitoa hiyo pesa.
Hatua ya nne, jifunze ku-save kwanza kabla ya kutumia. Mshahara ukiingia, toa pesa ya savings immediately. Usisubiri kubakiza, kwa sababu ukweli ni kwamba hutobakiza kitu.
Hatua ya tano (hii ndiyo shortcut pekee halali): ongeza kipato. Kwa kipato chako cha sasa, safari ya 25M itakuwa ndefu. Ukipata side hustle au skill inayoongeza income, hapo ndipo utapunguza muda kwa kiasi kikubwa.
Mwisho kabisa, saving pekee haitoshi kwa muda mrefu. Ukishajenga nidhamu ya kusave, anza kufikiria uwekezaji kama mifuko ya uwekezaji, bonds au biashara ndogo ili pesa ianze kukua.
Kwa kifupi: Save 200k–300k kila mwezi bila kukosa
Tengeneza emergency fund kwanza
Weka pesa sehemu ambayo si rahisi kuifikia
Toa savings mara tu mshahara unapoingia
Tafuta njia ya kuongeza kipato
Ukifanya hivi kwa nidhamu, 25M utaifikia. Ukirudia mfumo wa zamani, utarudia matokeo yale yale.

RMK,
Independent stock analyst.
WhatsApp:+255 737 450 640
Dar es Salaam.
 
Salama mkuu? Sijui kama umeshapata ufumbuzi. Ila hicho kiasi cha pesa naweza kukupa assurance kua unakipata ndani ya mwaka huu mmoja. Kabla ya december, kama kweli unakihitaji.
Ila kabla hatujafika mbali naomba kufahamu,
1. Biashara unayofanya
2. Eneo au mkoa uliopo

Hivyo ndio vitu vya msingi zaidi.

Kipato chako cha mwezi ni mtaji mzuri sana, na kuipata 25M ni Hesabu tu.
 
Nahitaji mbinu ya kufikia malengo mkuu sio lazima iwe mwaka mmoja binafsi nimejiwekea walau miaka 3-4
 
Lakini kwa sisi tuliosoma Finance tunasema Loan is cheap source of funds/ capital
Hii iko sahihi sana ila kwasisi wafanya biashara wadogo wadogo kupata loan kwa dhamana ya biashara ni ngumu labda kausha damu ukakauke kau
 
Ela yakula unataka kuisave ?? Upo serious kweli? Unaupendo wa dhati kwa familia Yako??
Faida ya 800k baada ya kutoa cost zote sio hela ya kula mkuu hiyo ni faida ambapo hela ya kula tushaitoa kwenye cost kule na kurudisha mtaji mahali pake
 
Kama unafamilia, miaka 3 - 4 sijui kama utafanikiwa, kwa sababu kuna mambo yatabadilika(mfumo unaoishi saivi na utakaoishi pindi unapotengeneza hiyo 25m utakua tofauti). Maana mpaka umekuja hapa kuna vitu umeona vinabana, moja wapo ni familia). Sasa hapo kama unaweza, ungesogeza muda mbele kidogo, miaka 6 - 7 ivi. Alafu pia shirikisha familia yako(mke, na watoto kama ikiwezekana).
 
Maamuzi magumu hayahitaji kikao. Chukua watoto peleka kwa bibi yao, mke mwambie atafute kazi afanye(ila sio kudanga) awe anapata elfu tanotano. We unaweka laki 6, jan 2030 unamkwanja wa kutosha. Ukishindwa hapo itakubidi uue ndugu zako tu.

"Maisha ni ushindi"
 
Hadi sasa nimeweza kukusanya jumla 2.1mil safari bado mbichi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…