Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Kiongozi,
Mungu akutangulie kwenye plan zako,
 
Mim nimeanza kufuga kuku mwez8 nimeanza na kuk 30 mixer na kanga target yangu mpka 2023 niwe angalau na kuku 1000
 
Kuna kitu mkuu unakosea sana, hakuna aliekataa mazingira ya kijijini kuwa hayako favourable Kwa ajili ya ufugaji wa kuku na hasa free range system....
Mkuu nilibahatika kuanza mradi wa kuku wa kienyeji katika eneo la eka 3 ila nilichukua sehemu ndogo ya eneo kwa kuanzia.

Walifika mpaka 100 na nilikuwa nawala ila siuzi
Mayai ni kugawa kwa familia tu

Nilikuwa na biashara zangu zingine kwa hiyo hapo nilikuwa napenda tu kuona wakizunguka kwenye machine za Unga

Chakula nilikuwa nawapa dagaa na virutubisho kwa kuchanganya ila nilikuja kusoma jamaa USA wanavyoweka rundo la mchnganyiko wa mboga na matunda pamoja na brown staff.

Hiyo ilinipunguzia sana kununua chakula kwani soko la mboga lipo karibu sana na Gari la kubeba lipo
Kazi ni kukusanya mabaki ya mboga na matunda na kubeba bure kutoka sokoni

Mradi niliufunga baada ya kuku kuingiliwa na ugonjwa ulioletwa na wasagaji wa mahindi na mradi ukafa ila sasa nataka kukaa mbali kidogo na kufanya mradi wa kibiashara zaidi na nitahitaji wataalamu wa kuwalipa vizuri

 
Kuvuka katika project kama hii utahitaji kuku wazazi wanaokaribia 260 mwaka wa kwanza
Wanaotaga mayai angalau 75%
Incubator yenye ufanisi usiopungua 85%
Vifo vya vifaranga/kkuku visizidi 7%
Ukuaji wa project usipungue 30% kwa mwaka....


Najaribu kufikiria jambo gumu kwa rahisi
 
Ana wazo zuri jamani.

Huwenda akaja kumudu kuku 2000.

Hatokuwa alipo lakini pia kuku wanataga mayai ambayo ni pesa kwenye kuku 2000 huwezi kosa kuku 300

wanaotaga kila siku hiyo yote ni pesa ambayo inasaidia uendeshaji

mtu anaweza kuwa na kuku hata milioni 1 achilia mbali hiyo laki moja
 
Ila mkuu kuwa na kuku mil 1 n Jambo linalowezekana k ila utekelezaji wake n balaa anahtaj kujitoa haswaa
Nikupe mfano mm hapa kwangu vjana wangu wanapassion ya ufugaji niliwanunulia kuku 10 jike 8!jogoo 2 asee wale kuku walianza.kutaga Kama mzaha Sasa hivi wanakuku 180 wa kienyeji ufugaj huu ulianza mwaka Jana mwez 1

Kiukwel wamekuwa msaada hapa nyumban

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hapo tunaongelea kampuni sasa ambapo una wafanyakazi hata elfu1 na mashamba hata kumi ya kuku lakini ukiwaza kwa udogo kwamba nyumba na ist ndiyo umeshapatia maisha basi kuku elfu mbili ni wengi sana kwako
 
Endelea kujifurahisha na kufurahisha wengine, ila kiuhalisia ni kwamba Huwezi kuwa na kuku laki moja

Unawajua kuku laki 1 au unawaskia tu? Hiyo mashine unayosema ipo ya kusaga haina uwezo wa kuhudumia kuku laki 1 Kwa siku...
[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…