Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Nimefikisha kuku 2000 mpaka sasa. Japo nilipata changamoto hapo kati, ila safari ndo imeiva hivi sasa. Nimetenga tray 10 kila siku za kuhudumia kuku wote. Mpaka ndoto yangu itimie.

Karibu tule vijogoo vya kuchoma na mayai ya kuchemsha kwa mama mkuu
allah akutangulie wasichokijua ni kuwa mpka kufika hiyo idadi hao kuku watakuwa wanajihudumia wenyewe.
 
umempa ukweli mchungu kulisha kuku laki1 kisa kuna mashine ya kukoboa karibu kijana analeta masikhara uyu
Mashine ya kusaga haiwezi kulisha hao kuku nafahamu. Ila hatua nilifikia saizi, nina soko la mayai kila siku tray 10 sawa na sh 120, 000

Nayaona matumaini japo sehemu ya kufugia inaelekea ukingoni. Hesabu niliyonayo ni kuuza uzao wa kuku 1500 yaani kila baada ya miezi 4 natoa kuku 12, 000 sawa na mil 150.

Biashara inaanza mwaka huu mwishoni
 
upo wapi mkuu nije kupata shamba darasa
 
hongera sana
 
Mimi siamini kwenye kufeli huwa naamini kwenye kujifunza. Pia nafahamu kuwa kila kitu hakipo kwaajili ya kila mtu. Nilikua na malengo ya kufikisha kuku laki moja lakini nimeamua kuishia kwenye kuku 2000.

Pia huwa siogopi kuzifuata ndoto kubwa. Kadri ninavyozidi kusogea na mradi wangu, ndivyo ninavyozidi kuyaelewa mengi sana kuhusu ufugaji wa kuku wa kienyeji.

Nilipofikia sasa, mdondo sio ugonjwa wa kutisha kwangu maana nina tiba kabisa
 
Soko ni kubwa sana la kuku wa kienyeji. Kinachofanya lisionekane, ni uhaba wa wafugaji wa kuku hawa. Ila wanatafutwa sana
 
Ulichokisema ni kweli kabisa. Hatua niliyofikia saizi, kwakweli nafurahi mwenyewe. Maana sioni mlima wa kuwalisha. Nauza mayai yao wenyewe maana soko ni zuri alafu nanunua mahitaji. Nakua busy sana maana kila kitu nafanya mwenyewe.

Naiona nuru mbele yangu
 
Simamia kwenye chanjo kuna ugonjwa unaitwa mdondo huo ukipita bandani kama kuku wako hawajachanjwa wanapukutisha banda nzima.
Mdondo sio tishio tena kwangu maana nina dawa ya kutibu kabisa. Hata ndui haifui dafu. Nimejifunza mengi kwa muda mchache sana nilioishi na kuku
 
Raha ya hawa kuku wa kienyeji hawako complicated sana kuanzia kula, na nature yao kwa ujumla. Inanipa urahisi maana hata dawaza magonjwa hatarishi, hivi sasa nazifahamu
 
Nimecheka sana.Vijana wanatoka shule wakiwa na motivated na mitandao.Mwambie ajaribu kuku 100 kwanza,ndiyo ataelewa Somo ni kwa nini watu hatufugi Kuku wa kienyeji kwa idadi ya broiler
Nitafika tu hata kwa mbinde
 
Hongera sana mkuu, wewe ni mfano wa kuigwa, uliamua kusimamia ndoto zako pamoja na changamoto ulizopata humu kutoka kwetu sie wachangiaji

Ata kwa hao 2000 sio haba ni wengi sana mkuu, ukilinganisha na Idadi uliyoanza nayo ya kuku 15, hivo unastahili hongera za dhati kabisa

Kama hutojali mkuu, tunaomba ushee nasi picha za kuku zako ili uzidi Ku inspire kundi kubwa la vijana ambao wanaamini kufuga ni kazi ngumu sana

utakuwa umetusaidia sana ukishea picha ili tuone Aina ya mabanda ambayo unafugia, system unayotumia kulelea vifaranga wako na vingine ambavyo utaona inafaa

Bila kusahau kutujuza ndugu zako hiyo dawa ya Mdondo uliyosema ushaijua, maana wengine tunaskiaga kuwa Mdondo hauna dawa, utawaokoa sana wafugaji wenzio mkuu
 
Hongera sana mkuu.
Kwa jamii ya wafugaji tukiona mtu mwenye ndoto kama zako huwa tunafurahi sanaaaaa.

Yan hapo najiona kama ndo mm vile nafuga kuku chotara katika kale ka pori kanguu.

Mungu akutangulie na akuepushe na kila baya katika ndoto hiyo,ukapate kufanikiwa zaid na zaid
 
kuku wa kienyeji wa umri wa miezi 4 ana thamani ye Elfu 15. Mbuzi wa Miezi 4 ana Thamani ya 80k. Kupanga ni kuchagua!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…