Nusu na nusu zikiungana inakua kitu kizima (weka tabia zako aweke zake mtengeneze ukamilifu na hii ndio maana halisi ya mahusiano).
And let's talk positively now...
Iko hivi, usichokijua ni kwamba watu hutofautiana kisifa kwahiyo unavyohama kutoka kwenye mahusiano ya zamani kwenda mapya inatakiwa sifa za yale ya zamani uachane nazo kabisa ili uweze kuanza upya.
Na unapoanza upya lazima utakutana na mapungufu tu, na kwenye hayo mapungufu yapo ambayo yanaweza kubadilika kwa haraka lakini yapo mengine ambayo yanahitaji muda kubadilika (kwahiyo ni wewe sasa kupima kama yanavumilika kwako au hayavumiliki kwa maana mwisho wa siku mapenzi ni maisha na ili uweze kufurahia lazima uwe comfortable).
Lakini pia mwanamume yeyote mwenye ndoto kubwa na anaechukua hatua thabiti kuzifikia ndoto zake usitegemee atakuwa anapatikana Kila wakati (tunapambania kombe na always tupo na vipaombele vyetu, kwahiyo ukiweka kwenye mzani mapenzi na pesa utagundua mapenzi yapo tu, usipoyapata ujanani utayapata, but vipi kuhusu pesa?).
Kwahiyo wanamume ambao wapo available Kila wakati ni wale ambao tayari walishatimiza ndoto zao au ni wale ambao hawana mishe za kufanya au ni wale ambao wamesharidhika na walichonacho au ni wale ambao wanakujaza ili wapate wanachotaka na wakishapata wanarudi kwenye default mode yao au ni low value man (so ukiona mpenzi wako yuko available sana inatakiwa ukae kitaalamu kidogo).
Lakini pia unapaswa ujiulize ya kwamba wanawake wanapenda sana kupewa attention so huo muda wa kubebishana ambao anakupa wewe hadi kukufanya uhisi furaha yako iko mikononi mwake anaouwezo wa kuwapa wanawake wengine kama wewe na wakajihisi kama unavyojihisi.
Ila mwanamume ambae Hana huo muda ni ngumu sana kudate na Kila mwanamke kwa maana wengi wanakua ni high value men.
NB:
Wadada wengi ambao wanasifiwa mara kwa mara kwamba wao ni wazuri au wale wadada ambao wako vizuri kiuchumi au wale wadada ambao wako na vyeo makazini au wale wadada ambao wako karibu sana na baba zao huwa wako na tabia ya aina hiyo.