Jambo la msingi kuelewa ni kwamba, Biblia kama wakati ule unasoma hautakuwa na usaidizi wa Roho Mtakatifu, au wakati ule unapolitumia Neno/Unapolituma kama hautakuwa umeokoka (kama hauna Mungu moyoni), ni kitabu cha kawaida tu na hakuna matunda yeyote. hii ndio sababu hata leo hii unaweza kumwita padre aliyesoma miaka 7 anaijua Biblia yote, ila ukimwambia kemea hili pepo litoke kwa huyu mtu, hawezi, wakati amesoma mistari Yesu alituagiza "pozeni wagonjwa fufueni wafu takaseni wenye ukoma toeni pepo".
hata Jina la Yesu, kama wewe haujaokoka, manake hauna Mungu moyoni hivyo mamlaka ya Mungu haipo moyoni mwako, halifanyi chochote, hata kama Biblia inasema "kwa Jina langu mtatoa pepo, mtaweka mikono juu ya wagonjwa nao watapata afya".
kwa hiyo, nawaasa, kuna faida katika kuokoka. Okokeni, siku ya wokovu ni sasa, wala sio kesho au baadaye, ni sasa. Neno la Mungu ndiye Mungu mwenyewe, linafanya kazi kwa wale tu wenye Mungu moyoni. hata mahubiri, yakihubiriwa na mtu ambaye hajaokoka, mfano, hao wanaocopy mahubiri ya wengine na kuweka semina na kupiga pesa, hata uhubiri vipi, hayawezi kubadilisha moyo wa mtu kwasababu hakuna Mungu ndani yake, anayeokoa ni Mungu, anayebadilisha ni MUngu anayeponya ni Mungu, kila kitu ni Mungu, sisi tunatumiwa tu kama vyombo, hivyo ukiona MUngu hajakutumia jua wewe sio wake, ukiona unafanya chohchote na hakuna uwepo wa Mungu jua umeenda peke yako na hakuna matunda, hata yakiwepo ujue ni maigizo ya adui wala sio Mungu, Mungu hawezi kuwepo hapo.
kuna kisanga kimoja, MATENDO 19:13 - 16, Imeandikwa:
13 Baadhi ya Wayahudi waliokuwa wakienda huku na huko wakiwatoa watu pepo wachafu wali jaribu nao kutumia jina la Yesu kutoa pepo, wakisema, βNakuamuru kwa jina la Yesu, anayehubiriwa na Paulo.β 14 Palikuwa na wana saba wa kuhani mkuu aliyeitwa Skeva ambao walikuwa wakifanya hivi. 15 Lakini pepo mchafu akawajibu, βYesu namfahamu na Paulo pia namfahamu; lakini ninyi ni nani?β 16 Yule mtu aliyekuwa na pepo mchafu akawarukia akawashambulia vikali, wakatoka ndani ya ile nyumba mbio wakiwa uchi na wenye majeraha.
kwanini pepo hakuwatii hawa? kwasababu kinachomtimua shetani sio jina la kawaida hili linaandikwa, ni Mamlaka ya Kimungu ndani ya Jina la Yesu ambayo haipo mdomoni, ipo ndani ya mtu, moyoni. Yesu anasema katika kitabu cha Ufunuo
Ufu 3:20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
ukimpa Yesu maisha yako, hata kaa kwenye makaratasi, katekisimo, liturgia au chochote, anaingia moyoni mwako, atakaa ndani yako, nawe utakuwa chombo tu yote anafanya yeye. miili yetu ni hekalu. tu. hivyo ninyi msiookoka, ni nafasi yenu sasa Mungu ameapa, okokeni leo, mpate sio tu uzima wa milele, bali ili muwe na mamlaka dhidi ya shetani na wafuasi wake wote.