Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Wakati mwingine watanzania tuwe na uwezo wa kujua kwamba kinachowekezwa kikiwa ni ghali, na huduma itakayotolewa nayo itakuwa ghali.

Uwekezaji uliofanywa kwenye SGR ni mkubwa mno kwa ivo ni lazima tukubaliane kwamba na huduma itakayotolewa itakuwa ni ghali pia.
 
Kwa mahesabu hayo kutoka Dar hadi Mwanza kwa SGR nauli itakuwa 500,000
Ni sawa tu. Maana tofauti kati ya treni ya Umeme na ndege ni mwendokasi na njia inayotumika. Maana wanaotakiwa kupanda hizo treni ni wale wenye haja ama sababu ya kwenda kwa kasi kuliko mabasi, Kama huna haraka hakuna sababu za kupanda treni hizo.
 
Hizo bei sio kubwa endapo muda utazingatiwa
Maaan kama una haraka n nzur sana sasa hzo naul znafkia za ndege?
Kwa umeme upi kwa kuendesha hayo mabehewa used kwa haraka angalau ndani ya lisaa hadi Moro?
 
😂😂😂sasa apo na haiendi kigoma apo waha wangejuta na bei
 
Hi project ya sgr haikufanyiwa feasibility study au upembuza ya sanifu, haiwezakani hiyo nauli izidi ya basi, wakati tulikua tunahitaji mbadala wa bei ya chini wa kutumia mabasi na maroli.
Imagine SGR ya Kenya nauli kutoka mombasa hadi Nairobi 600km ni sh 1000 ya Kenya sawa sawa na 19,000 ya Tz itakua je kutoka Dar - Moro 180km iwe shilling 34,000 kwa hiyo itakua na comparative advantage kwetu.
 
dhana potofu
 
They are willingly killing it before it stars. Sijajua lakin wametumia uhalisia wa wateja wao au walitumia mere papers. We must balance the papers and the reality of the fields
 
Achana na wanasiasa Gharama ya Umeme unaolipia inatokana na gharama za uzalishaji (au in our case gharama za kununua kutoka kwa madalali n.k.) sasa kama gharama ya uzalishaji itapungua common sense inakwambia nini ?

Tupende kuangalia tatizo lipo wapi na sio outcome zitakuwa vipi..., kama kila mwaka ukilima shamba kuna wezi wanakuja kuiba kabla haujavuna tatizo sio wewe kupanda / kulima tatizo ni hao wezi na jinsi ya kuwazuia wasikuibie..., Hence tatizo sio Bwawa kuisha na kuongeza double capacity ya sasa tatizo ni walamba asali
 
Wagogo wakisoma nauli ya Bahi naona wote watahamia Chadema safari hii
 
Unajua hii ni train ?; Unajua ni kiasi cha kuongezea behewa tu, kwahio hao watu hata mkitaka mkodi behewa kwa milioni tano ili msafiri peke yenu / peke yako nadhani its possible ?

Shida unaangalia mambo kwa mafungu na sio kwa ujumla..., hao masikini / wanyonge unaowaita huenda kwa kuweza kutoka moro na matenga yao ya nyanya kwa bei nafuu ikakusaidia wewe na familia yako kiafya kwa kupata chakula kwa bei nzuri zaidi na fresh zaidi ili uendelee kupanda train kwa kujinafasi..., Pia hio Train imefadhiliwa na kodi za hao hao pia so called wanyonge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…