Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Hiyo ni bei ya nauli walizopendekeza wao trc then latra watakusanya maoni ya wadau ili wacrosscheck pande zote kupata bei sahihi ya mlaji. Kama mlaji napendekeza nauli ya dar moro iwe 6000
Baba akipendekeza upikwe ugali maharage wewe kama mtoto kutengua ni utata.
 
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeitisha kikao cha wadau kujadili nauli za abiria wa treni ya njia ya Reli ya Kisasa--SGR ambapo Shirika la Reli Tanzania (TRC) linapendekeza Sh 59,494 na Sh71,392 kwa daraja la kwanza na la kati mtawalia kwa mtu mkubwa anaye safiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.

TRC imependekeza nauli ya Sh 24,794 na Sh 29,752 kwa daraja la kawaida na kati kwa mtu mkubwa anaye safiri kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.

Latra imesema inahitaji maoni ya wadau kabla ya kufikia uamuzi wa kuridia viwango vya nauli kwa huduma za treni hiyo. Mkutano huo umepangwa kufanyika Disemba 19, jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Anatorglo.

HII IMEKAAJE? MBONA KUSAFIRI KWA BASI NI BEI NDOGO KULIKO TRENI SASA?
 
serikali inafeligi hapa kwenye kutofautisha kati ya BIASHARA na HUDUMA!

ukieka bei kubwa kwenye usafiri si kwamba utazalisha faida mapema big noooo!

utazalisha mchwa kuongeza kula urefu wa kuzidi kamba zao
 
Nauli sio mbaya, muhimu waangalie muda wa kusafiri na ubora wa mabehewa, hasa kwa daraja la kawaida, SGR lazima iwe na ubora wa mabehewa na muda wa safari ili kuitofautisha na reli ya kawaida.
 
Dar - Moro 60mins mkuu.
Kwa nauli ya elfu 29 kama ni muda wa saa moja tu iko vizuri kuliko.kutumia karibu masaa saba kwa basi ma spidi limit barabarani kibao

Mabasi ya kwenda nyanda za juu kusini wajiandae kuwa na route za kuanzia morogoro kwenda mikoa hiyo sababu mtu akiua masaa sita ya barabara akishuka morogoro anapanda basi la kutoka Moro kwenda Iringa ,mbeya na Ruvuma anafika mapema tu

Treni hiyo iondoke mapema mfano saa 12 na nusu ifike morogoro saa moja na nusu watu wa mikoa ya nyanda za juu kusini wapande.mabasi yao kuanzia morogoro saa mbili yaondoke kwenda mikoani

Vivyo hivyo liwahi Dodoma wa mikoa ya kanda ya Ziwa wapandie mabasi Dodoma kwenda Kagera nk yawezekana kabisa watu wa kagera kufika siku hiyo hiyo bila kulala kahama

TRC wajipange kuhakikidha watu wana move faster kwa kushirikiana na wadau wa mabasi ya abiria

Ratiba zao wa consider hilo na Latra wajipange kupanga ratiba zao vizuri za mabasi ya Moro kwenda nyanda za juu kusini nk na Ya Dodoma kwenda kanda ya ziwa na kigoma nk

Treni ikimwaga mabasi yanapokea mbio yanakimbiza abiria
 
Baba akipendekeza upikwe ugali maharage wewe kama mtoto kutengua ni utata.
Uko sahihi ila hapa hatuongelei familia, hayo ni maslahi ya wananchi lazima serikali iangalie huku na huku
 
Nauli sio mbaya, muhimu waangalie muda wa kusafiri na ubora wa mabehewa, hasa kwa daraja la kawaida, SGR lazima iwe na ubora wa mabehewa na muda wa safari ili kuitofautisha na reli ya kawaida.
Mbona nauli ya ndege hiyo Mkuu
 
wezi huwaza kuiba hata akiwa Kanisani anawaza kuondoka na vyombo vya kanisa ili akatumie yeye peke yake
 
Tujue itatumia muda gani kufika doms kama ndio ile mwendo wa Kobe,,,bus tu hakuna na namna!
 
Sasa mkuu kama tunazungumzia kinachoendelea na sio jinsi ya kuweza kuboresha hatuna tofauti na wale mababu zetu waliosema wanadiscuss people au events na sio ideas...; Hakuna mtu ambae haoni kinachoendelea kwamba ndivyo sivyo.., ila hio kazi ya ku-report tunawaachia kina Pascal Mayalla wafanye kazi yao wengine sisi hapa tunaongelea mawazo / fikra zetu no matter kama zitafanyika au kutofanyika katika kizazi chetu
Naunga mkono hoja, hakuna SGR yoyote ya Africa itajilipa kwa kusafirisha abiria!, usafirishaji wa abiria ni service only, not for profit!, kiukweli nchi hii tuna mijitu mijinga sijapata kuona!. Nauli ya SGR lazima iwe ndogo kuliko nauli ya basi ili iwe incentive kuvutia watu kupanda SGR!. Haya mambo sisi wengine tuliyaona kitambo na tukashauri, Reli ya SGR: Je, Tujifunze kwa wenzetu Kenya kuepusha SGR yetu kuwa ‘A White Elephant’? Wenzetu yameshawakuta...

kwa vile sisi ni akina kajamb. nani, nobody listens!

P
 
Back
Top Bottom