Naumaliza mwaka Kwa machungu ya kuachana na mwanaume wangu niliyempenda sana

Hapa ndio penye pwenti ya msingi haya tuambie kwenye hizi harakati ulimwambia unataka kumpiga kiasi gani? Maana hapa ndio wanaponyoooshwa wengi kigezo cha ndoa mtu anatandika na mkeka wa shida zake mfululizo siku hizi vijana wameamka ukimleta shida zako analala mbele yeye sio kituo cha watoto yatima yaani akuoe kwa kukuonea huruma?
 
Duh, pole sana, piga moyo konde, unaweza kuishi bila yeye, kitakachokutesa ni mazoea tu, ukiweka mazingira mazuri(sio kilevi wala kuanzisha mahusiano kwa kukurupuka) basi utaishi vizuri na kwa amani, yeye sio oxygen yako, yeye sio wa kwanza na hawezi kuwa wa mwisho. Mpaka hapo hana thamani ya kuitwa mumeo, umeumbwa uenjoy sio kuteseka.
Asieijua thamani yako, hana haki ya kupata chozi lako.
 
Kibaya zaidi maumivu hayo yy hajui kama unayapata. Angalia kulia na kushoto kisha vuka barabara uende ng`ambo
 
Aibu nishaipata sababu mahusiano yetu yalikua open Sana
Aibu ya kuvunjika mahusiano ndio kitu gani?

Sikiliza binti, huyo bwana angekuwa amejitambulisha na kukulipia mahari hiyo ndiyo ingekuwa aibu, siyo hii unayoiongelea hapa.

Hayo yalikuwa mahusiano ya kawaida, kinachokuumiza ni malengo na upendo ambao unasema ulikuwa nao juu yake, usijiongezee vitu vya kukuumiza moyo.

Lakini, kosa lako lilikuwa kutuma ujumbe wa kuvunja mahusiano, ungekaa kimya ungeondoka na ushindi mkubwa maana pengine alipatwa na matatizo wewe kwa kukurupuka kwako umevuruga mambo.

Pengine anaweza kurudi, msikilize sababu zake na lazima hili lililotokea uliweke kama taa nyekundu, kama hana sababu za msingi inabidi uyape fikra ya upili hayo mahusiano yenu. Na asiporudi songa mbele, achana na mambo ya kujidhuru ni ukatili kwako na wapendwa wako.

Pole.
 
Umeandika ujumbe mreeefuuu utafikiri na wewe unaufuata
 
achana nae jitahidi na wewe usimtafute

kula vizuri jipende na jipe furaha mwenyewe siku yaja utapata anaejali hisia zako πŸ™‚β€β†”οΈπŸ™‚β€β†”οΈ
Lini sasa wakati sahv ana miaka 32 πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Yeye ndo alipropose ndoa Wala Sio mimi
Alipropose wewe ukaja na yako ya ili unioe fanya hivi na vile na vile, kaaangalia kaona hapa naingia kwenye dushu hili ngoja nilale mbele hapa naenda kupigwa, demand zenu kabla ya ndoa ziwe na akili sio mna-demand vitu sio vijana wanaingia mitini na wanaofanya hivyo ni wale wenye akili pekee mazombi wanakubali kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…