Naunga mkono suala la kubinasifisha Bandari ya Dar es Salaam

Naunga mkono suala la kubinasifisha Bandari ya Dar es Salaam

Mleta mada uko sahihi. DP World ni kampuni yenye weledi usiotia shaka. Kwa wasioijua ni kuwa wao pia ndo wana mikataba kwenye bandari sita za USA. Je, USA wao ni wajinga? Hakuna namna tunaweza piga hatua kwa kuendekeza watanzania wenzetu wanaotupiga daily.
Kwa sheria za US Wala hao dp world hawawezi fanya ujinga. huku kwetu hesabu ni maumivu

Kaangalie pia Namibia kilichotokea kwa hap dp world unaowasifia
 
Wewe unamuona tundu lissu kama mtu safi, kalagha bhao, huwa Najaribu kuunda serekali ya chadema kifikra huwa nashindwa kujua itakuwaje?, mfano rais TL, Makamu wa rais yule with zanzibar, Waziri mkuu mbowe, Waziri biashara sugu, Mambo ya ndani lema, hivi mnadhani hapo patakuwa na nchi kweli?

..KATIBA nzuri yenye sheria kali itadhibiti wezi wa Ccm, Chadema, Act, etc.

..Trump alidhibitiwa na Katiba ya Marekani. Wangekuwa na Katiba legelege Trump angepora uchaguzi.
 
Ndio tupangishe ila siyo kwa miaka Mia duh

Muhimu mkataba uwekwe wazi.

Tuelezwe kwanini wameamua miaka Mia na sio labda mitano kwanza

Kwanini hakukuwa na ushindani wa makampuni tofauti.

Tunahakikisha vipi na wenyewe hawatupigi?
 
Kwa sheria za US Wala hao dp world hawawezi fanya ujinga. huku kwetu hesabu ni maumivu

Kaangalie pia Namibia kilichotokea kwa hap dp world unaowasifia
Point muhimu kwa USA, Europe hawezi sababu na wao wanasimamiwa na watu makini, wazalendo kwa mataifa yao na kila kitu kinawekwa na kipo wazi.

Hatua zote za kuwapa tenda, malengo, faida Kwa nchi, urefu wa mkataba, kwanini uwe mrefu hivyo vyote vingekuwa wazi. Añgalia hadi sasa huu mkataba hivi bado unafichwa, haujawekwa wazi.

Hapa Tanzania, Afrika wasimamizi wenyewe ndio hao hao wala rushwa wakuu, hawajali, ndio washirika wakubwa wa upigaji wa Mali za umma.

Nani atawasimamia na kuwawajibisha?
 
Ifike wakati Serikali iachane na kufanya biashara make huu ni ujamaa na ushakuwa proved haiwezekani zaidi ya upigaji.

Kwa taarifa zaidi soma hapa >> Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam

Mashirika ya umma kama Bandari, Tanesco, Maji, sijui Posta, TTCL, ATCL, na zinitakiwa kuingia sokoni kuuzwa.

Hiyo Bandari ya Dar kama ingejengwa ya Baganoyo na ya Bagamoyo ikawa ni private na ya Dar ikawa ni ya Serikali bila shaka meli zingehamia Bagamoyo na ya Dar ingekuwa kama TTCL now.

Tanesco angali utendaji wao, lazima wafuatwe offisini uwe unajuama na mfanya kazi mmoja wapo, na sio tu kufuatana na kuwapa rushwa juu, sasa ingekuwa inasimamiwa na watu weupe unazani kungekuwa na kufuatana offisini?

Angalia TTCL haijulikani kazi zao kwa sasa, hivi TTCL ilikuwa ni ya kushindwa hadi na wakina Haloteli? TTCL ilipaswa kuwa sawa na Vodacom, ila Kwa sababu ni Mali ya Umma hakuna anaye jali pale na imejaa wafanya kazi wengi kuliko ufanisi na hakuna anajali.

Mamlaka za maji zimejaa upigaji tupu, unafuatilia kuunganishiwa maji hadi unachoka na lazima uhonge la sivyo hutakaa uunganishiwe maji.

Kwani Bandari ikikodishwa hao wanao kodisha watakuja kuondoka nayo? Wataihamisha? Tuachane na ujamaaa
acha siasa kwenye mambo kama haya hivi miaka 100 unaielewa vizuri
 
Naona vitu kwa sasa wanapewa sekta binafsi kwa sirisiri bandari, mbuga kwa miaka 33, 100 nk.

Pia Kuna LNG na uwekezaji wa 40bn USD. Hii process inaendeshwa kwa usiri isije kuwa ni mikataba kama ya ACACIA

Kwanini kuna ugumu gani na kigugumuzi kuweka haya mambo wazi kama mkataba na Tanzania na Barrick Gold?
 
Hii story ya Namibia inaonekana ni kama 100% kilichotokea Namibia.

Soma hapo chini

"In 2019, DP World, a Dubai-owned port operator, under the aegis of Sultan Bin Sulayem, with support from the former Transport Executive Director, Willem Goeimann orchestrated a plan to gain control of the newly constructed N$4.2 billion Walvis Bay container terminal through a direct agreement for a period of 50 years.

DP World’s strategy included extending unwarranted generosity to several Namibian decision makers, some of whom were completely oblivious of their true intent; to avoid a competitive process that would most probably undercut their chances of controlling this strategic asset. To bypass Namibia’s procurement laws and justify a direct agreement, DP World’s agents pushed for a largely farcical Government-to-Government agreement between UAE and Namibia, which was a mere smokescreen, hiding DP World’s real motive. This deception was clearly manifested when they signed an MOU with Nara Namib to develop a Free Economic Zone in Walvis Bay.

It was considered dangerous and inimical to the interest of Namibian People but it seems no one made the effort to analyse it in detail.

For unscrupulous foreign opportunists all you need is the opportunity, an architect to draft the master plan, a local agent that knows how to manipulate the system, a few key officials and the unscrupulous foreign investor to exploit Namibia and deprive it of real economic development".

Naunga hoja mkuu serikali yetu kwenye mashirika Haina uwezo wa kuyaendesha wabinafsishe wabaki kukusanya Kodi tu huko naona kidogo wanajiweza lakini usimamizi ni mbovu kwakweli
Mbona Bandari ya Dar kila mwaka inapata faida mabilioni ya fedha ?
 
Hii Bandari iligeuzwa shamba la bibi la watu wachache kuchuma harafu wengine tunabakia kuwa Wapenzi watazamaji..

Naipongeza Serikali kuweka investor Cha msingi wakubaliane pesa Kwa mwaka Ili awatimue wale wezi na waliokuwa wanaleta inefficiency..

Iende Hadi kwenye sekta zingine mfano tuna Kampuni ya Ranchi ya Taifa hakuna wanachofanya ni upuuzi tuu.
Secta nyingine ifutate inazie pale yule bibi pale ikulu maana hataki kutumia hata 1/64 ya akila yake solution ni kubinafsisha tuanza na yeye kwanza
 
Mleta mada uko sahihi. DP World ni kampuni yenye weledi usiotia shaka. Kwa wasioijua ni kuwa wao pia ndo wana mikataba kwenye bandari sita za USA. Je, USA wao ni wajinga? Hakuna namna tunaweza piga hatua kwa kuendekeza watanzania wenzetu wanaotupiga daily.
Maktaba wa US.A na hapa kwa bibi unaweza kulinganisha reputation yao
 
Kuwaachia kila kitu wawekezaji maana yake tunakiri hatuwezi kujitawala, ni bora sasa tumrudishe mkoloni arudi kwasababu naamini kabisa, jinsi mambo yanavyoendelea serikalini kwa sasa, pia tunahitaji kuibinafsisha serikali yetu.

Hivyo sioni sababu kwanini tuendelee kuwaza kubinafsisha vitu vidogo dogo, wakati kule juu penye tatizo la msingi tunaendelea kupaacha kama palivyo, alaah, kumbe inawezekana hata vichwa vyetu pia vinatakiwa kubinafsishwa, kwasababu fikra zetu nazo ni mgando.
Kwani tunaweza kujitawala?
 
Ifike wakati Serikali iachane na kufanya biashara make huu ni ujamaa na ushakuwa proved haiwezekani zaidi ya upigaji.

Kwa taarifa zaidi soma hapa >> Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam

Mashirika ya umma kama Bandari, Tanesco, Maji, sijui Posta, TTCL, ATCL, na zinitakiwa kuingia sokoni kuuzwa.

Hiyo Bandari ya Dar kama ingejengwa ya Baganoyo na ya Bagamoyo ikawa ni private na ya Dar ikawa ni ya Serikali bila shaka meli zingehamia Bagamoyo na ya Dar ingekuwa kama TTCL now.

Tanesco angali utendaji wao, lazima wafuatwe offisini uwe unajuama na mfanya kazi mmoja wapo, na sio tu kufuatana na kuwapa rushwa juu, sasa ingekuwa inasimamiwa na watu weupe unazani kungekuwa na kufuatana offisini?

Angalia TTCL haijulikani kazi zao kwa sasa, hivi TTCL ilikuwa ni ya kushindwa hadi na wakina Haloteli? TTCL ilipaswa kuwa sawa na Vodacom, ila Kwa sababu ni Mali ya Umma hakuna anaye jali pale na imejaa wafanya kazi wengi kuliko ufanisi na hakuna anajali.

Mamlaka za maji zimejaa upigaji tupu, unafuatilia kuunganishiwa maji hadi unachoka na lazima uhonge la sivyo hutakaa uunganishiwe maji.

Kwani Bandari ikikodishwa hao wanao kodisha watakuja kuondoka nayo? Wataihamisha? Tuachane na ujamaaa
Hakuna nchi ambayo imebinafsisha kila kitu mzee bandari ni sehemu nyeti sana huwezi kumpa mtu binafsi aendeshe kuna mambo mengi ya kiusalama kwetu na nchi jirani ni sawa na kuzi privatelize airports haiwezekani zitakuwa ni highways za kupitishia magendo na silaha haramu .
YAANI TUMPE MCHINA NDIO ASIMAMIE BANDARI YETU LOL!!
 
Naungana na wewe serikali kufanya biashara ni kunufaisha watu wachache tu maana wizi ni asili ya watanzania ziwekwe terms nzuri kimkataba ambazo zitaipa pesa za uhakika serikali wawaachie wawekezaji.hata ufanisi utakuwepo sana na malalamiko yatapungua sana
Wanao nufaika ni wachache sana jamii kubwa inabakia masikini milele
 
Secta nyingine ifutate inazie pale yule bibi pale ikulu maana hataki kutumia hata 1/64 ya akila yake solution ni kubinafsisha tuanza na yeye kwanza
Wala hakuna shida hata yeye atabinafsishwa ,kikubwa Ufanisi uje

Kamatia hapo hapo Rais Hadi wanyooke Hawa nyumbu waligeuza Bandari shamba la bibi la kuvinia,ngoja Mwarabu aje awanyooshwe vizuri
 
Back
Top Bottom