Uchaguzi 2020 Nawamegea siri: 'Bakuli la Lissu' lijazwe michango, linasaidia kuruka kiunzi kikuu mwaka huu

Porojo tupu, kwani hawakupewa ruzuku kwa ajili ya kampeni? Kila mtanzania anajua jinsi hii saccos ilivyo na matumizi mabovu ya rasilimali fedha. Wanaofaidi ni hao top layers tu wengine ndio imekula kwao mazima.
CAG huwa anakagua na hakuna hicho ulichokitaja hapa!
Muulizeni mashinji ambaye yuko huko kwenu na ndiye aliyekuwa anasaini fedha za chama awape siri!Ukiona kimya mjue hizo ni propaganda!
 
Kumbe hata CCM mnajua kua mmewatia umasikini wananchi?.
Kila mabadiliko yanahitaji gharama, hivyo sio mbaya kwa mwananchi kuchangia kwa aliyenacho, kama hana alazimishwi kuna njia nyingine ya kuchangia kiifikia ahadi ya maendeleo ya kweli
Na ile michango ya wabunge ipo wapi hadi mchangishe watu?
 
Hawa ni wahuni mkuu, wanadai wananchi wana halimbaya kiuchumi hapohapo wanawachangisha pesa sijui wanatuonaje Hawa watu.
 
Sisi wapenda Uhuru na demokrasia tumeshachanga na tutachangia tena
Mbona alipotoka Zanzibar ndugu Lissu aliongea na wanahabari, alilalamika hali ni mbaya sana kifedha? Kama mnachanga kweli hali ingekuwa hivyo?
 
Kwani ile michango waliokuwa wanakatwa wabunge kwa ajili ya uchaguzi iko wapi? Wananchi wana hali mbaya kwa nini muwachangishe?
Hiyo hali mbaya ya wananchi imeletwa na nani? CHADEMA au CCM inayokusanya Kodi! Iliyotawala miaka 60 sasa?
 
Kwani ile michango waliokuwa wanakatwa wabunge kwa ajili ya uchaguzi iko wapi? Wananchi wana hali mbaya kwa nini muwachangishe?
Muulize MEKO wenu ile RAMBIRAMBI ya WANA KAGERA ameifukia wapiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii?????????????
 
Hiyo hali mbaya ya wananchi imeletwa na nani? CHADEMA au CCM inayokusanya Kodi! Iliyotawala miaka 60 sasa?
Mgombea wenu anazunguka anasema wananchi wana hali mbaya. Sasa kwa nini anawachangisha hata pesa?
 
 
... TUONDOE WATAWALA WANAOFUGA UMASIKINI NA UNYONGE WETU ILI WAENDELEE KUTUTAWALA!
🤮🤮🤮🤮
 
Nalazimika tu kujibu ingawa umenijibu kishabiki kuliko kiuchambuzi.

Hata vile nijibu kwa ujumla kuwa uwe mkweli na jasiri kuwauliza viongozi wa CHADEMA matumizi ya fedha za chama (ruzuku, michango ya wabunge, ada za wanachama, misaada ya vyama rafiki vya nje, nk}.

Kuna tuhuma dhidi ya Mbowe zilizotolewa na viongozi waandamizi waliokihama chama, hazijajibiwa hadi muda huu. Labda una majibu tofauti na madai yako kuwa zimetumika kwa shughuli za chama. Au ndiyo hayo ya tuhuma? Km inadaiwa kuwa watumishi wengi wa chama hawalipwi mishahara/posho.

Uchaguzi Mkuu 2015, CHADEMA kilikuwa kimejiandaa kifedha kwa kampeni ikiwa ni pamoja na mabango, TShirt, chopa, nk. Iweje leo kishindwe kumudu gharama za kampeni huku kina vyanzo vya uhakika {ruzuku + michango ya wabunge)?

Kuna vyama vingi tu vinashiriki Uchaguzi Mkuu huu visivyokuwa na ruzuku wala mapato kama CHADEMA, havitembezi bakuli.

Nashauri wafuasi wa CHADEMA, humu JF, waache unafiki kama wana nia nzuri ya kutaka kiwe Chama Tawala, ili isije baadaye kunung'unika kuwa hawakujua. Kuna ushahidi usio na mashaka kuwa CHADEMA hakiendeshwi kama chama cha siasa. Dai hili linakinyima uhalali wa kupewa ridhaa na wananchi kuongoza nchi.

Bila kumung'unya maneno, naomba kwa Mwenyezi Mungu awajaze ujasiri Watanzania kukiadhibu vibaya sana CHADEMA kwenye sanduku la kura ili viongozi wake warudi mezani kujenga chama upya kama chama cha siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…