Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata km still Kuna watu Wana hela na hawapendi watt wengisio kila mtu ana shida. mfano CEO wa NMB ana watoto watano. kwenye ndoa yake
Kuna wanaume wamejipata kiuchumi kila kitu kuanzia kwao tu walipozaliwa kuna makampuni.. sasa huyo nae akioa aogope kupata watoto wengi kisa shida
Habari wadau.
Ukweli maisha ya kisasa sio rafiki kabisa kwa dada zangu ama wanawake wote.
Wanawake wana biological age tofauti na wanaume.
Dada zangu wanamaliza elimu mapema wakiwa ealy 20s tu wameshamaliza masomo. Hapo wapo hot. Sura nzuri. Mayai ya uzazi yapo vizuri ukigusa tu mimba. Waoaji hawaonekani sababu kipindi hicho dada zangu wanakuwa hawana kipato cha kueleweka. Mwanamke Kuolewa mpaka awe na maisha ama kipato kizuri nowdays. Ama huyo dada atoke familia bora mambo safi ndio anaolewa haraka.
Dada zangu wanabaki wanasuburia huku umri unaenda mayai ya uzazi nayo yanazeeeka. Maana hawana hela ya ku ya freeze kama wazungu.
Dada zangu hao hao wakifika 30s kidogo kipato kimesimama simama. Ndio wanaume waoaji wanaibuka na kutaka kuwaoa. Dada zangu hawana hiyana wanaolewa.
Shida kwenye ndoa sasa wanaenda kukutana na lawama kwamba hawazai ama wakijitahidi wanazaa mtoto mmoja tu.
Mwanaume kama unataka familia watoto wengi kwa nini usimuoe dada yangu toka amemaliza chuo wakati yupo early 20s...
Hapo ungemchoka mwenyewe mpaka anafika 30s angekuwa ameshakuzalia watoto hata watatu. Na angekuzalia wengine in her 30s sababu uzazi umeshafunguka mapema kuendelea kuzaa sio ishu kwake
Kumuoa umechelewa mwenyewe halafu unampa lawama kwamba hazai watoto unaotaka.
Wanaume mjifunze wanawake wana biological clock.
Kama tunapenda watuzalie familia kubwa Tuwaoe mapema wakati mayai yao yana nguvu ealy 20s
View attachment 2890512
View attachment 2890483
View attachment 2890561
Point. Komando Jide bado mbiichiiMiaka 20 kwa elimu ya bongi bado sana.. Akimaliza chuo yupo 23 tuseme kwanza yale mapenzi ya chuo mengi hayapelekei ndoa ni utapeli na uongo..
Msomi akimaliza anarudi home au anabaki town kusaka mishe sana sana ajira ili atumie ujuzi wake aliosoma.
Ndoa na kupata mtoto ni jambo zuri ila kila mtu atapafa kwa mda ,mwanamke hachakai kwa umri wala kushindwa kuzaa akiwa mtu mzimq...Clock ya mwanamke inategemea katumika vip mwanamke aliyeanza mapenzi mapema hapo kati kafanya mambo ya hovyo inawezekana katoa mimba mfano kuna moja ya msanii wa bongi hap ndio ulikuwa mtindo wake...
Mwanamke miaka 30's anazaa tena yupo kweny nafasi kubwa ya kupata watoto mapacha ...
Hao unaowasemea hapa,ni wale waliosoma bila shida km za kufeli, kurudia rudia,au kuunga unga ambao Wala sio wengi kulinganisha na Hawa wengine,umti huo wengi Bado snTanzania wanawake wasomi tukipima kwa wale waliofika chuo kikuu. huwa wanahitimu shahada yao wakiwa na miaka 23.
shule ya msingi wanaanza na miaka 7 na wanamaliza msingi na miaka 13 ( tena hao kayumba, wale wa english medium la kwanza wanaanza mapema zaidi na miaka mitano ama sita )
form one wanaanza na miaka 14 na wanamaliza o level na miaka 18
form 5 wanaanza na miaka 18 na wanamaliza na miaka 19
chuo wanaanza na miaka 20 na wanamaliza na miaka 23 wale wa kozi ndefu kama udaktari ndio wanamaliza na 24 ama 25.
umri ni factor kubwa sana ya uzazi kwa mwanamke. utafiti wa kisayansi umethibitisha hilo
View attachment 2890519
Hata km still Kuna watu Wana hela na hawapendi watt wengi
Aah huku bwana watu wanazaa tu bila hayo mamboteknolojia zimekuja sababu kuu ni kulinda mayai ya mwanamke yasipoteze ubora maana wanajua umri unavyoenda yanapoteza quality yake. nchi zilizoendelea wanawake wasiotaka kuzaa mapema sababu ya career zao huwa wana freeze mayai yao kipindi wakiwa na umri mdogo. mfano binti wa miaka 25 akifreeze mayai yake . siku akifika miaka 40 anataka kuzaa anatumia mayai yake yale yale aliyoyafreeze akiwa na miaka 25.
View attachment 2890527
Unajua haya maisha bwana acha tukae kimya tu.Risk factors, kinachoongelewa sio ukomo wa kuzaa coz hata 40s wanazaa, wengine hadi 50s. Ila complications zinaongezeka kadri umri unavyosonga. Kama kuna chances ya kupata watoto ukiwa 20s na 30s ni vyema sana, unapunguza risks za mimba.
Hii mada haileweki, hapa unaongelea wanaopenda kulelewa ama? Yaani Mimi na akili na nguvu zangu nisubiri mwanamke apate hela ndio nimuoe? Huo ujinga siwezi fanya.
Sio wote mkuukwa wanaume akiwa na hela nyingi ama mali nyingi lazima atapenda kuwa na watoto wengi. maana wanaume tunaendeleza ukoo. watoto ndio msingi wa ukoo kuendelea.
ndoa bila watoto mwanaume anajiona kama hajakamilika
Aah huku bwana watu wanazaa tu bila hayo mambo
Watu Wana 50 Bado Wana breed🤣
Usiogope mkuu we ongea tu, ila ni vema kupata watoto ukiwa bado mdogo, complications zinakuwa sio nyingi. Lakini pia usiwe na pressure as kila jambo na wakati wake.Unajua haya maisha bwana acha tukae kimya tu.
Watu wajue safari ya maisha haifanani!
Kwakweli nasema hivi tusipangiane maishaVivaaa katibu
Nasemaje kuolewa sio kipaumbele chetu
Tutazaa tukitaka, furaha ya moyo ndo kila kitu..!!
Hatupo kwenye mashindano ya uzazi na ndoa