Uchaguzi 2020 Nawashauri CHADEMA wamtulize kwa sasa Tundu Lissu aache kufanya mashambulizi makali kwa Rais Magufuli


Endeleeni kulialia, subiri tuwatembezee kipondo cha bila huruma.
 
Lisu ajikite kutuambia atakayoyafanya, kila mtu anajua strength na weakness za Magufuli hivyo tumechoka kuzisikia.

Ni wakati muafaka sasa upinzani hasa Lisu kuanza kutumegea mikakati waliyo nayo katika kutuvusha kutoka hapa tulipo kwenda pazuri zaidi.

Tumechoka kila siku kusimuliwa blunder za Magufuli
 
Hizo tirioni tulizokopa watanzania wanatakiwa waambiwe zinazidi kipato chetu kwa ukubwa gani,lakini pia waambie kuwa hiyo pesa ni zaidi ya budget yetu ya mwaka mzima,kwamba Kama nchi ingekuwa ni familia basi baba ameamua kutofanya kazi za kuingiza kipato amekalia tu kukopa,watanzania waangalie asije akawauza
 
Chuja chuja ya ubunge isiyo ya kibinadamu inayekwenda kufanywa na CCM huko Dodoma unayo manufaa makubwa kwa chadema hususani kwa wale walioshinda kisha wakakatwa kwa report za uonevu zilizosukwa na wabaya wao
 

Muda wa kampeni bado, unataka aanze kuinad ilani ya chadema ili mkaweke pingamizi kuwa ameanza kampeni kabla ya wakati.
 
Usiwe na haraka subiria kampeni zianze utasikia vingi ambavyo vitakuduwaza kama siyo kukushangaza, ukumbuke mtukufu alizuia mikutano ya siasa kinyume cha Sheria kwa miaka 5 mengi mabaya madhambi yote vitaanikwa live
 
Muda wa kampeni bado, unataka aanze kuinad ilani ya chadema ili mkaweke pingamizi kuwa ameanza kampeni kabla ya wakati.
Hizi habari za kumsema sema rais kila mara majukwaani ni nini kama sio kampeni ?
 
Yeye anatoa Rushwa kwa kununua kuku kupanua barabara akiwa anakula mahindi ya kuchoma, unataka amseme nani wakati huyo ndiye mpinzani wake namba moja
Kwa mtazamo naona inamfanya Lisu aonekane ana personal hatred na Magufuli
 
Nanukuu: Eti umejenga mabwawa je kwani kulikuwa hakuna mabwawa yaliyoyowai kujengwa uko nyuma?
 
TL ni kama mwalimu, anaongea lugha rahisi sana hata wasio na elimu wanaelewa, kitu kizuri sana hiki kwasababu kuna umbumbumbu unatakiwa ufutwe vichwani mwa wananchi wa kawaida. Education and Information are crucial, go TL.
 
Hayati Kingunge alitoa angalizo

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kwani hiyo ndiyo ilani ya uchaguzi ya CHADEMA?? Hivi kwa akili yako unadhani watanzani ni wajinga kiasi gani kumchagua huyo mropokaji?

Kwani kampeni zimeanza hadi aanze kunadi ilani ya uchaguzi tulia hiyo imetengewa siku 60
 
Tatizo la Magufuli ni kama ifuatavyo

1. Anaogopa mfumo wa utawala kupitia taasisi... anataka yeye ndio awe taasisi na aamua anavyo taka.. Ndio maana wengi wanasema mambo mengi anayo yafanya hayatadumu labda madaraja tuu.. lakini issue na madini na mikataba tayari zimemshinda kwa sababu kwanza bado ni siri..

2. Diplomasia ana ikwepa kitu ambacho atakwamba kwa sababu dunia ina wenyewe cha msingi cheza kwa akili.

3. Anaongelea zaidi vitu kuliko sera na utawala bora.
 
Kwani kura unaenda kupiga wewe peke yako na ukoo wako?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…