Nawaza ingekuwa Rais Samia ndio kasaini Mkataba wa SGR...

Tena Mungu mkubwa sana, Kikwete tayari ile mikataba, SGR ilikuwa kishawapa China, Bwawa kishawapa Brazil, bandari ya bagamoyo alishawapa China na Oman, jamaaa alipoingia tu akaipiga chini yote.
Kumbe ndo maana this time mkastuka kumlinda mwarabu wenu mkaamua kuingia mkataba ambao hautapigwa chini aingie Rais gani au hata jina la nchi libadilike..
Msilinde uswahiba wenu at the expense ya nchi yetu.
 
Nauliza, kinachopingwa bandarini ni nini kama siyo dini?
Siku moja moja uwe unatumia muda kufikiri nje ya dini na utumie muda huo kufikiri juu ya uTanzania wako.

Huu ulevi wa dini unakuwa ni ugonjwa sasa.
 
Yaani Dr Slaa angetembea uchi just to make sure kila mtu anaona alivyochukizwa.....Pengo angetoa waraka kama wote
Kwa hiyo wa SgR ni sawa na huu wa milele?😂😂😂😂😂😂😂
 
Shost
Hao waarabu wamepewa kuendesha hiyo miradi au wanajenga na kuviacha viendeshwe nasi wenyewe?
 
Huyu nae sijui tumuiteje, unafananisha vitu hata havifanani.

Halafu naona JPM anazidi kuwa benchmark ya mafanikio ya utawala wenu, kila mnachofanya mtalinganisha na mwamba.
 
Kila nikiona sura ya mama au kusikia sauti yake napata mchanganyiko wa hisia mbali mbali mbaya sana, hasira, ghadhabu, uchungu, kichefu chefu eti al!!
Usijali, siku dp world ikianza kazi utazaa!!
 
Kila nikiona sura ya mama au kusikia sauti yake napata mchanganyiko wa hisia mbali mbali mbaya sana, hasira, ghadhabu, uchungu, kichefu chefu eti al!!
Upo kama mimi mzee: mi nipo hapa unguja kila sehemu wamebandika mapicha yake, natamani kuyachana yote
 
Kwani mama Samia kauza nini?

Hamjaona changa la Macho la Makinikia? Au huelewi kilichofanyika?
FaizaFoxy, ungejenga hoja kwa kutumia vifungu vya huo mkataba, mimi ningekuelewa na kuendeleza mjadala, lakini unaishia katika kulaumu tu.

Kama siyo kuuza, unaelewaje kifungu kifuatacho:
KIFUNGU CHA 7:VIBALI VYA MRADI
3. Iwapo vibali vikisha tolewa kwa mradi wowote havitoweza, kubatilishwa, kubadilishwa, kurekebishwa, au kushindwa kuhuishwa au kuongezwa na Serikali ya Tanzania au mamlaka husika ya serikali au wakala bila ya mashauriano ya awali na PCFC inayowakilisha Serikali ya Dubai ikiwa ubatilishaji kama huo, mabadiliko, urekebishaji au kushindwa kuhuisha au kuongezwa kunaweza kuwa na athari mbaya kwa Miradi (au yoyote kati ya hizo).


Kumbuka PCFC ni kampuni inayomilikiwa na Emirate ya Dubai na ikimiliki DPW (100%). Kwa maana hiyo DPW inaingia Tanzania kama balozi kumiliki Bandari na maeneo mengine yaliyoainishwa kwenye huo mkataba batiri. Kwa msingi huo itakuwa vigumu kuvunja mkataba nayo ila kwa njia ya kidiplomasia au mlolongo mrefu kwenye mahakama za UK (Kifungu cha 20 cha huo mkataba batili) kati ya Tanzania dhidi ya Dubai na siyo DPW.

Vifungu vifuatavyo vinakidhi hoja yangu ya kumilikisha bandari na maeneo mengine kwa Emirate ya Dubai, kampuni ya DPW ikiwa balozi mwakilishi. Nanukuu:

KIFUNGU I: UFAFANUZI NA TAFSIRI
“DPW” au “DP World” inamaanisha DP World MEA Ports FZE, kampuni inayomilikiwa na serikali ambayo inamilikiwa kikamilifu na PCFC ambayo inamilikiwa kikamilifu na Emirate ya Dubai,... ambayo itaanzisha Kampuni moja au zaidi za Miradi nchini Tanzania kwa madhumuni ya kutekeleza Shughuli za Mradi.

KIFUNGU CHA 2: LENGO LA MKATABA
1. Madhumuni ya Mkataba huu ni kuweka mfumo wa kisheria wa maeneo ya ushirikiano kwa ajili ya maendeleo, uboreshaji, usimamizi na uendeshaji wa bandari za bahari na maziwa, kanda maalum za kiuchumi, hifadhi za usafirishaji, korido za kibiashara na miundombinu mingine ya kimkakati ya bandari nchini Tanzania.


Vfungu vichache hivyo vya huo mkataba batili, ni dhahiri kuwa hakuna shaka Tanzania inawekwa kwenye utawala wa Emirate ya Dubai. Ili hilo lisitokoe mkataba wa IGA uwe wa ushirikiano tu na DPW iwekeze nchini kwa Sheria, Taratibu na Kanuni zetu, kama ilivyowekeza kwingineko duniani.
 
Wakati mwingine uzi wako unaweza kuivua nguo akili yako.
 
We Bibi mmepata sehemu ya kujificha. Mwendazake haja scramble kuuza wanyama ama kuhamishia vilemba kwenye mbuga. Kufanya kazi na hii serikali no sawa kufanya na mwendawazimu
 
Bwana yule alikuwa hasemi ukweli
 
 

Attachments

  • B76822CB-E8E2-4088-8411-E5AA5510704B.jpeg
    58.4 KB · Views: 3
  • 6EDC7B14-A93F-4E68-8620-26A64FDD4180.jpeg
    62 KB · Views: 2
  • 81871876-5CB1-434D-9E5C-1E228DD650AA.jpeg
    55.5 KB · Views: 2
  • E19279F6-BA45-4EA5-9860-D3816D9F1FD4.jpeg
    71.8 KB · Views: 2
Mkiambiwa

kwamba nyinyi akili ni ndogo zaidi mnaongozwa na udini mnakasirika!

SGR, Alipewa mturuki ni Mwislamu
JKNHSP, walipewa Wamisiri Ni Islamic

Uliona tatizo lolote kwa wakristo?
Nyani ona kund*lo please liko hapo nyuma hebu pindisha shingo hapo kidogo.
 
Namshangaa faiza leo kaja na hoja ya udini, mim na ugalatia wangu nimemkosoa jiwe mwanzo mwisho na mpaka naingia kaburini sitokubaliana na aina ya utawala wa jiwe
Yeye kwakuwa anamtetea Samia kwakuwa ni muislamu mwenzake, anataka kupotosha kuwa ni vita vya wakristo dhidi ya rais muislamu. Lakini kiukweli dhalimu ndio tulimpa vitasa vya hatari kuliko Samia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…