Nazeeka kwa kasi ya ajabu mno. Nifanye nini?

Inawezekana mkuu ukawa huna hekima ndiyo maana unaogopa uzee! Laiti ungekuwa na hekima ungefurahia maana watu wangekuwa wanakufuata kutaka ushauri! Mara nyingi mtu anayeng'ang'ania kuonekana kijana ni watu wa kupenda kichepuko!
 
Kuna miaka miwiwili ya nyuma tulienda mahali kufanya mkutano Wa Injili na wakati wamaombezi akaletwa mama mmoja kuombewa
Sasa sisi tuliona ni mama mtu mzima ila waliomleta wanasema ni binti aisee ilitushangaza sana kwakweli

Tukaanza maombezi pale yaani alipandisha mapepo ya hatari ili baada ya kuyamuru yamtoke Kwa jina La yesu

Na yakatii kumtoka gafla uso wake ulirudisha nuru yake na sasa akatazamika kama binti na kesho yake anakaja tena aise haikuwa rahisi kukubali ni yule mama Wa Jana wa miaka 45+ maana alikuwa ni binti Wa miaka 26 mzuri kweli kweli

Na ndipo tukapata kisa kwamba kunamtu alimkataa kuolewa nae ndio mambo yalivyoanza kumbadilikia

Hivyo kama umejaribu mazoezi na kubadili menyu yako ya msosi na bado unaona kuna kitu sio chakawaida basi chukua hatua dunia inamengi sana hii
 
Fanya mazoezi, Tembea au kimbia x 3 kwa wiki angalau jumla 15km

Piga push up, squart, jumping jack, stretching

Pata jua la asubuhi kwa ajili ya Vitamin D

Pata supu ya kongoro japo mara 4 kwa wiki

Pata usingizi wa kutosha katika mazingira yenye ubaridi

Punguza stress

Practice Pranic yoga kwa ajili ya kuupa mwili oxygen ya kutosha, Google pranic yoga by Swami Ramdev
 

Mazoezi na matunda . Usingizi wa kutosha. Basi umemaliza uzee utausikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…