NCCR Mageuzi yamsimamisha James Mbatia kufanya shughuli za Chama

Hakuna mtu ambaye amewahi kunajisi chama kama Magufuli.

Ebu fikiria, wagombea wa ubunge 75% waliopitishwa wajumbe, aliwakata majina yao, na kupachika ya kwake. Fikiria mahali kama Shinyanga, Masele aliyepata kura 360 za wajumbe, alikatwa jina lake, akampachika Katambi aliyepata kura 3. Wote kimya kabisa ndani ya CCM. Hakuna aliyejaribu hata kunyanyua pua kuhoji. Ukisikia udiktetamwingine wote ni uchwara, udikteta hasa, tazama matendo ya marehemu Magufuli. Ukinyanyua pua kuhoji tu, umeuawa, kutekwa au kupotezwa, ikiwa bahati yako nzuri sana unusurike kama Lisu au Mdude.
 
Alie zaidi ya Mbatia ni katiba ya chama chao, tofauti na chama fulani cha upinzani ambacho mwenyekiti ndo yupo juu zaidi ya katiba ya chama chake, ndo maana anaamua lolote atakalo dhidi ya chama na hakuna wa kumuuliza.

Tupe uzoefu wako wa mwenyekiti wa CCM, maana hapa nilipo nachekea kwenye shati.
 
Doh!!namuona mzee wa mama Tanzania Akiunga juhudi mkono
Huyo hawamuwezi! Akishirikiana na Marando, Selasini na nduguye Lamwai nk, walimng'oa Mrema na maguvu yake. Kisha, akaja kung'oka Marando, Selasini mwenyewe na kumwachia chama. Nina imani, hao waliotangaza mapinduzi, watang'oka wao!
 
hawa watu wanajitambua sio yule mbowe kigando kang'ang'ania cheo cha mwenyekiti ,safi nssr
 
DaaAAh wamemtimua
 
Katiba yenu inasema ukiwa rais outomatiki unakuwa m/kiti wa chama, chukua mfano kama mkishindwa uchaguzi mala tano mfululizo itakuwaje??
Nioneshe hicho kifungu cha katiba, kinachosema ukiwa raisi unakuwa outomatiki mwenyekiti wa chama. Na kama hauna basi kubali kuwa wewe ni chawa kama chawa wengine waliokubali kutumiwa kama daraja na wajanja wachache, kwa masilahi ya matumbo yao na familia zao.
 
Chadema kwani Mbowe ndio mwanzilishi?

Magufuli alipokuwa akiajisi Chama CCM ilimfanya nini? Au dawa ndio kumuwekea sumu na kusingizia moyo?
Hayo ya sumu unayajua ww. Ila huku muda wako ukifika utake usitake lazima upishe wengine. Hiyo ndio demokrasia ya kweli.
 
Kwani wewe haufahamu kuwa kila rais mpya wa ccm anakuwa m/kiti wa chama pia??
 
Kwani wewe haufahamu kuwa kila rais mpya wa ccm anakuwa m/kiti wa chama pia??
Unapojadiliana na mtu mwenye akili kama mimi unatakiwa utumie akili yako mwenyewe ili twende sawa, sio utumie akili uliyopandikizwa na mwenyekiti kwa masilahi yake na familia yake. Nimekuomba unioneshe kifungu cha katiba ya ccm kinachosema kuwa mtu akiwa raisi wa JMT anatakiwa pia awe mwenyekiti wa chama chao, umekosa kunionesha, badala yake unaendelea kubwabwaja bila evidence. Hilo ulilozungumzia hapa ni swala la mazoea wala halipo kwenye katiba ya chama. Kama ilivyokuwa imezoeleka mwanzo kwamba raisi wa JMT akitoka bara basi awamu inayofata atatoka zenji. Haya yalikuwa ni mazoea tu wala sio katiba ndio maana uliona utaratibu huo uligeuka mwaka 2005 baada ya kutoka hayati Mkapa bara akaingia Kikwete bara na Kikwete pia akamuachia hayati Magu ambae nae alikuwa m'bara. Kwahiyo swala la mazoea ambalo halipo kikatiba wenye chama wakiamua kupindua meza kama walivyopindua kwenye swala la uraisi wa bara na zenji hakuna atakaepingana nao.
 
Usiwe na matarajio makubwa sana na mtu kabla hujamwona kwenye hiyo nafasi.Heche unaweza kumwona mzuri kumbe nikwasababu hajakaa kwenye hiyo nafasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…