Ghiti Milimo
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 4,748
- 7,061
Wa kwanza kujinyonga, atakuwa johnthebaptistWajumbe wa mkutano mkuu chadema wana mpango wa kumuongezea Mbowe miaka mitano tena, hadi mjinyonge.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wa kwanza kujinyonga, atakuwa johnthebaptistWajumbe wa mkutano mkuu chadema wana mpango wa kumuongezea Mbowe miaka mitano tena, hadi mjinyonge.
Hakuna mtu ambaye amewahi kunajisi chama kama Magufuli.Bora huko nccr viongozi wapo huru kumuhukumu mwenyekiti wa chama. Upande wa pili mwenyekiti huwa haguswi hata pale anapotoa boko mchana kweupe. Na anapojitokeza wa kujaribu kufuata sheria za chama dhidi ya kiongozi wa chama basi anakiona cha mtema kuni. RIP Chacha Wangwe.
Alie zaidi ya Mbatia ni katiba ya chama chao, tofauti na chama fulani cha upinzani ambacho mwenyekiti ndo yupo juu zaidi ya katiba ya chama chake, ndo maana anaamua lolote atakalo dhidi ya chama na hakuna wa kumuuliza.
Huyo hawamuwezi! Akishirikiana na Marando, Selasini na nduguye Lamwai nk, walimng'oa Mrema na maguvu yake. Kisha, akaja kung'oka Marando, Selasini mwenyewe na kumwachia chama. Nina imani, hao waliotangaza mapinduzi, watang'oka wao!Doh!!namuona mzee wa mama Tanzania Akiunga juhudi mkono
DaaAAh wamemtimuaHalmashauri Kuu ya Chama cha NCCR Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wake, James Mbatia kufanya shughuli zote kisiasa za chama hicho mpaka pale atakapoitwa kwenye mkutano mkuu kujieleza.
View attachment 2232853
=======
Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia na makamu Mwenyekiti Bara, Angelina Mtahiwa kutojihusisha na shuhhuli zozote za chama hadi mkutano Mkuu utakapoitishwa ili wajieleze kuhusiana na tuhuma inazowakubali.
Uwamuzi huo umefanyika leo Jumamosi Mei 21, 2022 kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kugombanisha viongozi na kulazimisha kujiuzulu.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mwenyekiti wa azimio hilo, Joseph Selasini amesema pamoja na kusimamishwa kwa viongozi hao pia wamelivunja Baraza la Wadhamini la NCCR na kuteua wajumbe wapya ambao watasajiliwa kwa mujibu wa taratibu zitakazowekwa.
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza amesema walipokea barua kutoka NCCR-Mageuzi kuwa kuna mabadiliko ya wajumbe wa bodi ya wadhamini.
Amesema pamoja na mabadiliko hayo kulikuwa na ajenda nyingine ambayo ni kusimamishwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Bara kutokana na maazimio hayo wanasubiri barua rasmi ili kutoa taarifa.
"Tuna orodha yetu tutaenda kuangalia kama mlivyoona wajumbe wapo na akidi imetimia hivyo tunangoja barua rasmi kisha tutaenda kupitia na katiba yao," amesema Nyahoza.
Pia soma > Mgogoro NCCR Mageuzi: Timu Mbatia wachukua ofisi, wasema umefanyika uhaini ndani ya chama,
Nioneshe hicho kifungu cha katiba, kinachosema ukiwa raisi unakuwa outomatiki mwenyekiti wa chama. Na kama hauna basi kubali kuwa wewe ni chawa kama chawa wengine waliokubali kutumiwa kama daraja na wajanja wachache, kwa masilahi ya matumbo yao na familia zao.Katiba yenu inasema ukiwa rais outomatiki unakuwa m/kiti wa chama, chukua mfano kama mkishindwa uchaguzi mala tano mfululizo itakuwaje??
Mbona chawa unajishtukia na wakati sikukitaja chama chako.Pole. Naona CHADEMA inakutesa sana.
Hayo ya sumu unayajua ww. Ila huku muda wako ukifika utake usitake lazima upishe wengine. Hiyo ndio demokrasia ya kweli.Chadema kwani Mbowe ndio mwanzilishi?
Magufuli alipokuwa akiajisi Chama CCM ilimfanya nini? Au dawa ndio kumuwekea sumu na kusingizia moyo?
Selasini alishindwa CHADEMA ameweza NCCR, Kosa la Mbatia ni msimamo thabiti juu ya KATIBA mpya ingawa kikazi wote ni undercover.
Kwani wewe haufahamu kuwa kila rais mpya wa ccm anakuwa m/kiti wa chama pia??Nioneshe hicho kifungu cha katiba, kinachosema ukiwa raisi unakuwa outomatiki mwenyekiti wa chama. Na kama hauna basi kubali kuwa wewe ni chawa kama chawa wengine waliokubali kutumiwa kama daraja na wajanja wachache, kwa masilahi ya matumbo yao na familia zao.
Hakuna chama kinavumilia uasi na uhaini, hata Zitto na Kitila Mkumbo wanafahamu hilo.Pale chadema ukitaka kufanya jaribio kama hilo unaweza jikuta unafanana na Chacha Wangwe.
Kwa hiyo akikengeuka kama yule kichaa kung'olewa haiwezekani?Hayo ya sumu unayajua ww. Ila huku muda wako ukifika utake usitake lazima upishe wengine. Hiyo ndio demokrasia ya kweli.
Unapojadiliana na mtu mwenye akili kama mimi unatakiwa utumie akili yako mwenyewe ili twende sawa, sio utumie akili uliyopandikizwa na mwenyekiti kwa masilahi yake na familia yake. Nimekuomba unioneshe kifungu cha katiba ya ccm kinachosema kuwa mtu akiwa raisi wa JMT anatakiwa pia awe mwenyekiti wa chama chao, umekosa kunionesha, badala yake unaendelea kubwabwaja bila evidence. Hilo ulilozungumzia hapa ni swala la mazoea wala halipo kwenye katiba ya chama. Kama ilivyokuwa imezoeleka mwanzo kwamba raisi wa JMT akitoka bara basi awamu inayofata atatoka zenji. Haya yalikuwa ni mazoea tu wala sio katiba ndio maana uliona utaratibu huo uligeuka mwaka 2005 baada ya kutoka hayati Mkapa bara akaingia Kikwete bara na Kikwete pia akamuachia hayati Magu ambae nae alikuwa m'bara. Kwahiyo swala la mazoea ambalo halipo kikatiba wenye chama wakiamua kupindua meza kama walivyopindua kwenye swala la uraisi wa bara na zenji hakuna atakaepingana nao.Kwani wewe haufahamu kuwa kila rais mpya wa ccm anakuwa m/kiti wa chama pia??
Usiwe na matarajio makubwa sana na mtu kabla hujamwona kwenye hiyo nafasi.Heche unaweza kumwona mzuri kumbe nikwasababu hajakaa kwenye hiyo nafasi.Mbowe amefanya kazi nzuri sana kwa miaka mingi ila sasa anapoendelea kukaa madarakani kwa miaka mingi wengi tunamchoka.
Suala la maslahi yake kifedha yupo vizuri sana kupata ndani ya chama mkuu, hili linajulikana.
Chama sasa apewe kijana wa kazi John Heche ili ccm wapotezwe kabisa.
Wenye Chama ndio hao wakina Joseph SelasinNilijua chama cha kwake