Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

Nimeishi na nchi moja huko ulaya na kufanya kazi taasisi moja hivi, Ilikuwa chakula tunakula kwa pamoja, Dah jioni chakula ni mikate hasa brown sosage na matunda mwanzoni sikuwaelewa aisee nilikuwa ikifika saa 6 usiku nakuwa na njaa balaa.

Kila jumapili jioni ilikuwa mnapangiwa zamu ya watu watatu kuandaa chakula cha jioni cha watu wote, hapa unaweza kupika chakula mtakachochagua nyinyi, siku hiyo tulipangiwa zamu ya kupika, nilipagwa mimi na jamaa wawili mmoja mtu Ghana na mwingine mbrazil, niliwashawishi tupike supu ya ng'ombe na tambi tule na mikate.

Duh ile supu wazungu waliigomea aisee, mjerumani mmoja na mke wake alisema kwao supu kama hii ni kwaajili ya Mbwa πŸ•, kwanini tuwapikie chakula cha mbwa πŸ•! tulimind sana

Hio siku sitaisahau maana walitususia supu yote aisee, tukaenda kuwapa mbwa πŸ•
 
Walionja kitu ulichokitoa au walishangaa tu??
 
Ahaaa dah duniani kuna Mambo,sasa hapo ugali wangekupiga nao
 
Mkate hutengenezwa zaidi kwa unga wa ngano, lakini hata huu ugali wetu wakati mwingine tunaita 'mkate' japo ugali hauliwi bila mboga. Sasa mboga nayo ni chakula kingine baki au ni kitu gani. Ni ajabu mtu kula mboga tu peke yake bila ugali au wali. Na pia ni ajabu mtu kula ugali peke yake bila mboga. Wali unaweza kula bila mboga ila kuna watu watakushangaa afadhali unywee na chai. Matumbo ya watu nayo yamezoezwa kulishwa aina fulani za vyakula ndio mtu anaona atashiba kisawasawa. Mkate? Kuna watu wakila mkate hawashibi hata kidogo bora wale wali kama hakuna ugali. Mikate inashibisha vizuri kama ikiliwa sambamba na vinyaji kama chai, maziwa, juisi na soda. Kutafuna mkate peke yake nako itashangaza
 
Wabongo chakula chetu kikuu ni UGALI. Chakula cha pili ni wali ikifuatiwa na ndizi, kuna nyongeza kama makande na viazi vitamu. Mboga kuu ni maharage na dagaa na za majani ni mchicha, matembele na kisamvu, nyama ni ufahari, kuna samaki nao wapo huliwa kwa ugali au wali. Chipsi ni chakula cha anasa tu wala si chakula cha kushiba. Mikate ni kwa kunyea na chai kama kifungua kinywa asubuhi. Siku moja Rambo aliingia hotelini huko kwao akaagiza saladi sahani imejaa akala, wabongo tukashangaa mlo huo wa Rambo
 
Slices 12!! Rey bhana hapo umetuuza,
Mimi nakula sana mkate na hata usiku huu nimetoka kula huo huo na Mayai mwanzo nilikula wali ukawa haushuki kabisa nikaachana nao nikapiga mkate wangu niko fresh kabisa,

Slices 2 tu hua sizidishi hapo.
Watu tunafukia mkate mzima kweli nyie ni species nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…