Nyerere, Nyerere, Nyerere!
Ulikuwa mbele mmno ya muda, hatukukuelewa, hatukuelewi na bila shaka hatutakuja kukuelewa.
Ulisema, maadui wakubwa wa taifa hili ni ujinga, maradhi na umaskini. Kwa wanaoweza kufuatilia video hii, haya maneno yako wazi!.
Na kwangu mimi,hapa nakiona kitu kimoja cha muhimu. UJINGA. Maskini mwerevu hawezi kujidhalilisha kiasi hiki kwa kugombea bagia, andazi nk
HIvi sio huyu mbunge amvaye miezi michache nyuma alitoa hoja ya kutaka kila Bodaboda achangie 1000 kwa ajili ya ujenzi wa barabara?
Hapa Nyerere anarudi, alisema" mtu mwenye akili akikueleza jambo la kipumbavu na wewe ukakubali, amekudharau" kwa kitendo hiki cha kugawa bagia na wananchi kugombea, amewadharau!
Na hii ndio ilivyo kwa taifa letu hivi sasa maadui wale watatu aliowataja Nyerere sasa wamekuwa mazimwi baada ya kustawishwa kwa rutuba na maji ya kutosha. Naogopa tulipo na tunakokwenda.