DR NCHIMBI; RAIS NA CCM HATUHUSIKI NA UTEKAJI
Hotuba ya leo Septemba 13, 2024 ya Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Nchimbi ni ya kihistoria. Amezungumza vitu vigumu kwa lugha rahisi kuonesha 4R za Rais Dkt Samia bado zipo hai sana.
Hotuba yake imebainisha mambo 10 ambayo pasina shaka Rais Dkt Samia na Chama tawala, CCM kama Taasisi mbili zinazoongoza nchi hadi sasa, zinaamini kwa VITENDO:-
1) Umoja, mshikamano na upendo wetu sote bila kujali tofauti zetu za vyama ndio nguzo ya taifa.
2) Utekaji na uuaji wa raia si siasa, ilani wala mwongozo wa Rais Dkt Samia wala CCM.
3) Watekaji na wauaji wa raia ni mtu ama kikundi cha watu wabaya WANAOWEZA kutoka CCM na ama upinzani.
4) Lengo kuu la Watekaji na wauaji ni kumgombanisha na kumfitinisha Rais Dkt Samia na Chama chake, CCM na wananchi, hivyo kwa vyovyote vile hawana baraka za Rais Dkt Samia na baraka za CCM kama chama tawala.
5) Wajibu wa kuwadhibiti Watekaji na wauaji wa raia si wa Rais na CCM pekee bali pia ni wajibu wa Upinzani, makundi yote nchini na wananchi wote.
6) Serikali haijashindwa kuchunguza matukio ya Utekaji na uuaji raia kufika kiwango cha kukaribisha wachunguzi kutoka nje ya nchi itusaidie, hivyo endapo Serikali itahitaji msaada huo, CCM itaunga mkono.
7) Kosa la mtumishi au kikundi cha watumishi wasiye waadilifu na waaminifu wa chombo cha ulinzi na Usalama sio kosa la vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama.
8) Kuhamasishwa kuwa na ugomvi na kutoamini vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kosa la watumishi wachache wa kada hii ya Ulinzi na usalama ni kujikosea na kujihatarishia maisha yetu wenyewe wananchi. Ni sawa tu na kukosewa na daktari mmoja na kutaka kuwachukia madaktari wote nchini wasituhudumie huku tuna wagonjwa kila uchwao.
9) Kauli za kuchonganisha, kutishia na kufitinisha baina ya Serikali, CCM na vyama Vingine vya siasa na wananchi zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa CCM na Serikali yake sio msimamo wa Rais wala CCM. CCM na Serikali ya Rais Dkt Samia ipo makini, haivumilii na huwa inawachukulia hatua za kinidhamu viongozi hao kwa mujibu wa taratibu za Chama na Serikali.
10) Samia Must Go haivumiliki wala haimstahili Rais wetu mchapa kazi, mpenda utu, haki na uhuru Dkt Samia kwani kwa muda mfupi ametuletea maendeleo yasiyomithimika, na cheo alichonacho hajajipa yeye mwenyewe bali katiba ndio imempa na kama kuondoka ataondoka kwa mujibu wa katiba na sio vinginevyo.
Ahsante Katibu Mkuu makini sana, Dr. Nchimbi.
Watanzania tuendelee kudumisha 4R( Reconciliation (Maridhiano), Resilience (Ustahimilivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga upya) za Rais wetu Dkt Samia tuendelee kujenga taifa letu lenye usawa, umoja na upendo, tusiunge mkono migogoro na maandamano ya kutuletea uvunjifu wa amani na utulivu tukalipoteza taifa letu adhimu hususani nyakati hizi za kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu ambapo watu waovu dhidi ya taifa letu wamejaa tele.
KAZI IENDELEE, na KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI‼️
Suphian Juma Nkuwi,
Simu; +255717027973