Nchimbi ni Shujaa wa Taifa au kajiuzulu kwasababu zake?

Nchimbi ni Shujaa wa Taifa au kajiuzulu kwasababu zake?

Wewe ambae sio mpumbavu na hulaumu mpaka sasa hivi umefanya nini?

Nyerere ana mengi mazuri
Na ana mabaya pia ikiwemo la muungano ucwara
Asante kwa kuelewa.

Hilo ndio swali ambalo inatakiwa tujiulize badala ya kuanza kumlaumu nyerere ambaye amefanya mengi mazuri kwa namna aliyoona inafaa.

Sisi sasa tuboreshe zaidi panapohitajika.

Mimi, wewe na yule tujiulize tumefanya au tunafanya au tufanye nini ili kuhakikisha kunakuwa na mambo stahiki?
 
Wewe ambae sio mpumbavu na hulaumu mpaka sasa hivi umefanya nini?

Nyerere ana mengi mazuri
Na ana mabaya pia ikiwemo la muungano ucwara
Kama nyumba inamsingi mbovu ni lazima ibomolewe. Legacy ya huyu Mzee ni lazima tuibomoe tukiendelea kulinda bhasi tukubali damu ziendelee kumwagika.

Mzee alikua hapendi ukweli wa mawazo mbadala.

Mfano

-Tuntemeke Sanga
-Mzee Kambona
-Marehemu Bibi titi
-Mzee Jumbe

Hao ni mifano ya watu walioonja rungu lake baada ya kuleta mawazo mbadala.
 
Wa Tanzania 🇹🇿 hili swala la Nchimbi lililosimamisha nchi tafsiri yake imekaaje?

Kuna maswali najiuliza hapa Naomba ku share nanyi

Hawa wafuasi waliojitokeza kumsifia Nchimbi na kumuona shujaa ni wana CCM wenyewe au ni wanachama wa vyama vingine?

Je, nani anajua Nchimbi amejiuzulu kwa maslahi binafsi au kwa maslahi ya taifa?

Na kama amejiuzulu kwa maslahi binafsi, bado anafaa kuonekana shujaa?

Na kama ni kwa maslahi ya taifa zima je ni mambo gani aliyofanya mpaka tuseme huyu kajiuzulu kwa maslahi ya taifa?
Kama yapo share hapa!

Jambo lingine, hili swala la Nchimbi kujiuzulu kwa nini linasherehekewa na upinzani wakati huo huo upinzani unasema hautambui serikali iliyopo?

Inawezekaje je kusherekea mtu kujiuzulu nafasi ambayo wewe huitambui?
Hii imekaaje?

Na kama tunasema kujiuzulu kwake ni jambo kubwa na la kupongezwa basi tunapaswa pia kujiuliza:

Ni nini hasa alichokifanya mpaka kuondoka kwake kuwe jambo la kusherehekea?

Tusije tukawa tunasherekea mtu kwa sababu tu ameondoka kwenye nafasi, bila kuangalia sababu ya kuondoka kwake na impact yake kwa taifa

Karibuni kwa maoni Kosoa, ila weka FACT

Na pia shauri nini kifanyike

Maswali ni mengi, wewe chagua kipande chako, weka maoni yako

ShesRise_1 🤚
Kukubali katiba mpya ambayo CCM wameisema kwenye ilani ya uchaguzi,wamenyuti, Yeye kapaza sauti!
 
Asante kwa kuelewa.

Hilo ndio swali ambalo inatakiwa tujiulize badala ya kuanza kumlaumu nyerere ambaye amefanya mengi mazuri kwa namna aliyoona inafaa.

Sisi sasa tuboreshe zaidi panapohitajika.

Mimi, wewe na yule tujiulize tumefanya au tunafanya au tufanye nini ili kuhakikisha kunakuwa na mambo stahiki?
Asante pia kunielewa
Nikuulize
Kwa namna unavyoona sisi watanzania
Tutaweza kusahihisha baadhi ya makosa yaliyofanywa na kina Nyerere
Kwa unafiki tulionao?
 
Hakika ShesRise_1 nakutoa kwenye Gen Z nakutunuku U millennium you're good in thinking and very right upstairs.

Kuhusu huyo Mzee ndie alitufikisha hapa.
Ukiona umefikishwa mahali na ukaendelea kubaki hapo manaake wewe ndiye umekubali na umependa uwe hapo.

Alikutoa huko akakufikisha hapo, yeye maono na jukumu lake lishaisha na ashasepa zake, sasa kutoka hapo sisi/wewe mwenyewe upambanie kwenda unapotaka kufika

Itakuwa ngumu kutatua matatizo yetu kama kila nyakati tutakuwa tunatafuta wa kumtupia lawama.
 
Asante kwa kuelewa.

Hilo ndio swali ambalo inatakiwa tujiulize badala ya kuanza kumlaumu nyerere ambaye amefanya mengi mazuri kwa namna aliyoona inafaa.

Sisi sasa tuboreshe zaidi panapohitajika.

Mimi, wewe na yule tujiulize tumefanya au tunafanya au tufanye nini ili kuhakikisha kunakuwa na mambo stahiki?
Mkuu unahoja lakini hoja zako hazina misingi.

Hoja zako zinakosa misingi pale ambapo unataka tumuongelee Nyerere kwa mazuri tuu.

Nyerere ndio muasisi wa hii nchi pia matatizo tuliyonayo Leo asilimia kubwa yametokana/yameanzishwa na Nyerere mwenyew.

Pia hatuwezi kutatua tatizo bila kujua chanzo Cha tatizo Sasa hapo ndio tunaona madhaifu ya Nyerere.

Vijana Leo wamekua tegemezi kwasababu ya sera za Nyerere na ujamaa wake, Wakati tunapata uhuru nchi hii ilikua ya kibepari yeye akaleta ujamaa, akaisomesha hiyo mizee Bure matokeo yake imekuja kuifilisi nchi haitaki kustaafu.
 
Hakika ShesRise_1 nakutoa kwenye Gen Z nakutunuku U millennium you're good in thinking and very right upstairs.

Kuhusu huyo Mzee ndie alitufikisha hapa.

1. Alifeli kuendesha nchi na bado hakukubali kwamba amefeli mwisho alisababisha zao la mkonge kufa kifo Cha kawaida kabisa.

2. Alisababisha shilingi ikashuka thamani against Dola mpaka Leo shilingi imeshindwa kujipambania.

3. Yeye ndio alianzisha maswala ya UHAINI, KUWEKANA VIZUIZINI, PAMOJA NA KUTEKANA.

4. Huyo Mzee ndie alianzisha mfumo wa vyama vingi vya kiini macho, alikubali kuanzisha mfumo wa vyama vingi lakini alivitoa meno. Mwishowe tukaona mauaji ya Zanzibar hasa Pemba na mengine mwaka jana. Hii ni mbegu aliipanda huyo Mzee

5. Huyo Mzee alijua kwamba katiba tuliyonayo ni mbovu na hata yeye mwenyew alishawahi kukiri Hilo lakini hakuchukua jukumu lolote kurekebisha Hilo.

6. Huyo Mzee ndie alijipa cheo Cha rais kuwa mwenyekiti wa chama ili aweze kucontrol matokeo yake ndio haya kichaa kapewa rungu na anapiga yeyote.

Kama mzizi wa fitna alianzisha huyo mnaesema ni baba wa Taifa.
Hakuna haja ya kulemba mwandiko ipo hivyo
Sawa alikua na mazuri yake
Lakini maamzi na misingi iliyowekwa kipindi taifa linajengwa yamechangia kwa kiasi kikubwa kufika hapa tulipo

Kuthibisha haya ni madai ya sasa ya katiba mpya
 
Nyerere ndio muasisi wa hii nchi pia matatizo tuliyonayo Leo asilimia kubwa yametokana/yameanzishwa na Nyerere mwenyew.

Pia hatuwezi kutatua tatizo bila kujua chanzo Cha tatizo Sasa hapo ndio tunaona madhaifu ya Nyerere.
Tuchukue haya uliyoandika kwamba yote ni sahihi na sawa tumeona kwamba matatizo yote kayaleta yeye.

Yanaondokaje sasa maana yeye alishakufa na katuachia/katuacha.

Tuendelee kumlaumu hadi mwaka 2100 au njia ya kuchomoka ni ipi? Hilo ndilo la msingi kwa sasa.
 
Ukiona umefikishwa mahali na ukaendelea kubaki hapo manaake wewe ndiye umekubali na umependa uwe hapo.

Alikutoa huko akakufikisha hapo, yeye maono na jukumu lake lishaisha na ashasepa zake, sasa kutoka hapo sisi/wewe mwenyewe upambanie kwenda unapotaka kufika

Itakuwa ngumu kutatua matatizo yetu kama kila nyakati tutakuwa tunatafuta wa kumtupia lawama.
Kaka hapa hatupiwi mtu lawama
Ila ukweli upo hivyo
Hii nchi makosa yalifanyika kipindi hicho
Ndiyo sababu tunalialia leo

Hata hivyo dawa sio kuwatowa mdarakani CCM
Hilo siyo suruhisho

Suruhisho ni katiba mpya bora
 
Kama nyumba inamsingi mbovu ni lazima ibomolewe. Legacy ya huyu Mzee ni lazima tuibomoe tukiendelea kulinda bhasi tukubali damu ziendelee kumwagika.

Mzee alikua hapendi ukweli wa mawazo mbadala.

Mfano

-Tuntemeke Sanga
-Mzee Kambona
-Marehemu Bibi titi
-Mzee Jumbe

Hao ni mifano ya watu walioonja rungu lake baada ya kuleta mawazo mbadala.
Kasheshe !
Haya mambo ya kunyamanzishana ni ya karne
 
Ukiona umefikishwa mahali na ukaendelea kubaki hapo manaake wewe ndiye umekubali na umependa uwe hapo.

Alikutoa huko akakufikisha hapo, yeye maono na jukumu lake lishaisha na ashasepa zake, sasa kutoka hapo sisi/wewe mwenyewe upambanie kwenda unapotaka kufika

Itakuwa ngumu kutatua matatizo yetu kama kila nyakati tutakuwa tunatafuta wa kumtupia lawama.
Mkuu kama nchi ipo kwenye mkwamo wa kisiasa na kiuchumi na tuliowapa dhamana ndio wanafanya maigizo ya kujiuzulu na maigizo mengine yapo mahakamani kwa kesi za uongo. Je! Tufanye Nini kama nchi ili kutoka hapa tulipo?
 
Kasheshe !
Haya mambo ya kunyamanzishana ni ya karne
Na huyo Mzee ndio muasisi wa haya mambo ya hovyo, sijui aliirithi hiyo tabia kwa wakoloni? Hata sielewi lakini simlaumu sana baada ya kusoma Uzi alianzisha mtoto wake Poppy Hatonn kwamba Mzee alikua haoni mbali/future.
Ni mvivu mpka kufanya kazi 🤣🤣
Hapana kwenye kazi Sina utani kabisa😂😂😂, watoto wetu watakula Nini? Mchanga sio chakula.
 
Kaka hapa hatupiwi mtu lawama
Ila ukweli upo hivyo
Hii nchi makosa yalifanyika kipindi hicho
Ndiyo sababu tunalialia leo

Hata hivyo dawa sio kuwatowa mdarakani CCM
Hilo siyo suruhisho

Suruhisho ni katiba mpya bora
Katiba mpya ndio CCM hawaitaki.

Kumbuka bunge la Mzee Sitta na yeye ndio aliharibu mchakato wa kupata katiba mpya wakatengeneza katiba wanayoijua wao halafu wakaitupilia mbali🤣🤣🤣🤣.
Hii nchi ukiwa serious sana utakufa kwa pressure.

Nakumbuka baada ya kumaliza ule upumbavu wao wa katiba walipoipitisha walikata na mauno kabisa😂😂👐🙌 bunge likawa kama uwanja wa kanga moko kumwaga burudani na katiba mpya ikaishia hapo.
 
Katiba mpya ndio CCM hawaitaki.

Kumbuka bunge la Mzee Sitta na yeye ndio aliharibu mchakato wa kupata katiba mpya wakatengeneza katiba wanayoijua wao halafu wakaitupilia mbali🤣🤣🤣🤣.
Hii nchi ukiwa serious sana utakufa kwa pressure.
Ngoja niombe visa kwa trampuuu nikaoshe vizee vya kizungu

Mambo yenu nawaachia
 
Nimesema hivyo kwa sababu kuna waliosema hawaitambui serikali iliyopo kwa maana haikuchaguliwa kisheria na wana nchi

Sasa ni kauliza kama serikali iliyopo haitambuliki inakuaje kusema makamu wa Rais kajiuzulu

Basi kama wanasema kajiuzulu ina maana wameikubali serikali iliyopo
Baadhi ya raia kusema hawaitambui serikali ni suala la kifilosifia zaidi kuliko uhalisia. Katika nchi yoyote kiuhalisia hata watu wakipindua serikali kama Traore au Al-Sisi tayari wanakua ni serikali inayotawala na kutambulika kimataifa.
 
Back
Top Bottom