Nchimbi ni Shujaa wa Taifa au kajiuzulu kwasababu zake?

Nchimbi ni Shujaa wa Taifa au kajiuzulu kwasababu zake?

Baadhi ya raia kusema hawaitambui serikali ni suala la kifilosifia zaidi kuliko uhalisia. Katika nchi yoyote kiuhalisia hata watu wakipindua serikali kama Traore au Al-Sisi tayari wanakua ni serikali inayotawala na kutambulika kimataifa.
Ahaaa haya sawa

Njee ya mada : naomba
niambie kuhusu huyo mzee kwenye Avatar yako
 
Unless aje/apewe jukwaa/afanye press kuwaambia wananchi kuwa alipush mabadiliko kwa njia gani akiwa ndani ya chama ili sisi wananchi kupitia “watu wenye akili” tupime kuwa alikuwa pamoja na sisi.

Look at CDM + TAL wamepush mabadiliko sio tu kwa kusema no reform no election (Katiba mpya ni sasa)

Bali…

1. Wamewafikia wananchi kupitia mikutano ya hadhara kuwafundisha na kuwashawishi kuunga mkono mabadiliko

2.Walianzisha kampeni ya NRNE na ikawa msimamo wa chama. (sio jambo rahisi kuwashawishi watia nia wakubali wasishiriki uchaguzi sababu licha ya kwenda kutumikia wananchi ukishinda kuna financial gain kichama na kwa wao kama watu binafsi, uamuzi wa kuacha kugombea ni alama ya selfless.

3.Wamepush mabadiliko institutionally, Wameomba kuonana na Rais na kumpa ajenda zao, kama chama cha upinzani na wanachi halali wa nchi hii, Wao CCM wakaona suala la msingi ni kupiga nao picha ili kuonesha ushirikiano fake…. Wakati wenzao wameomba kuonana na kiongozi kupush ajenda ya mabadiliko as they should. Viongozi wa serikali ya CCM kwenye hili wameonesha unafiki wa hali ya juu, miaka na miaka Hii nchi ina wazee wanafiki sana, zamani nilikuwa sijui maana ya msemo “wapinzani wanapenda kuitwa kunywa chai ikulu na kupiga picha” kumbe kumsingi huwa wanapeleka agenda zao kimaandishi , hawa wanafiki huwaza picha tu ili wazitumie kisiasa.

Additionally wameomba kuonana na viongozi + Taasisi respectable kuwashawishi watumie ushawishi wao kuongea na Rais/uongozi nchi isiingie kwenye uchaguzi bila reforms kufanyika sio kwasababu wao CDM wamesema bali tume mbali mbali zilizoundwa toka miaka ya 90’s zilitoa hayo mapendekezo.

(Haya yote ameyasema TAL mahakamani Tarehe 24/08 akiwa chini ya kiapo kwahiyo hadanganyi)

Sasa na yeye bwana mkubwa siku akipata jukwaa alitumie kuwaeleza wananchi alichofanya…. kinyume na hapo tutaendelea kumuona ni walewale wamewahiana tu. GenZ + na sisi Millennials ni ngumu kutuimbisha nyimbo za ushujaa bila kutupa mzani.
✍️✍️
 
Nimesema hivyo kwa sababu kuna waliosema hawaitambui serikali iliyopo kwa maana haikuchaguliwa kisheria na wana nchi

Sasa ni kauliza kama serikali iliyopo haitambuliki inakuaje kusema makamu wa Rais kajiuzulu

Basi kama wanasema kajiuzulu ina maana wameikubali serikali iliyopo
ki kawaida chadema nadhani toka 2010 wao hua matokeo yakitoka wanasema hawaitambui serikali, hivyo kwenye hilo ni kawaida ya chadema ila kwenye utendaji serikali zilezile wasizozitambua wamekua wakifanya nazo kazi kama kawaida tu.
 
Mkuu mpaka hapo nadhani umeshanielewa kwa kiasi fulani sio?
 
You ask great questions!

1) Mimi ninakuwa na wasiwasi navyoona Watanzania wanavyompigia makofi Nchimbi kwa kusema endeleeni kuomba katiba mpya. Polepole alisema Nchimbi ni mwanamtandao na pia Nchimbi has been a notable member of CCM for longer than most of us have been alive — hatujui mambo aliyofanya humo ndani miaka nenda rudi.

Mimi hofu yangu kubwa ni wanamtandao wanatuchezea akili.

What if this is all a scheme ? Nchimbi ajiuzulu, wananchi wamuite shujaa, 2030 agombee uraisi kama mtu aliyesimamia haki = mtandao unabaki madarakani.

2) Kumcompare Nchimbi na Polepole ni kumuonea Polepole. Polepole hawakumvua uanachama, alitekwa… Nchimbi kafukuzwa na matarumbeta… Hawa watu wana mind games…

Vitu Polepole alivyoweka wazi kuhusu wanamtandao, CCM, na serikali — you cannot even begin to compare it with the few sentences Nchimbi uttered.

3) The constructed separation between SSH and Nchimbi. Mimi mwaka jana niliweka mpaka academic articles zinazoonyesha how female leaders are regularly used as scapegoats in corrupt government systems — maraisi wanawake wanaofungwa kwasababu ya ufisadi sio kuwa hawajaiba, wanatumika na the boys club kunawa dhambi zao na kuendelea na uhalifu wao. Mtandao lazima una Plan A, B, C… ili uendele kuishi.

Mkuu mpaka hapo nadhani umeshanielewa kwa kiasi fulani sio?
nimekupata sana mkuu, kama mtazamo wako ni huo nadhani wote tupo mzani mmoja labda kidogo sana tutofautiane angle ya kutizamia, ila kwa kua kwenye uzi huu nimeona mara kadhaa umeandika kwamba "hakuna kuremba muandiko" --- basi na mimi kwenye comment zile nilikua sirembi muandio dhidi ya chadema.

na kuchangia kiasi mada comment ya mdau hapo juu na wote wenye mlengo huo nawaunga mkono isipokua tu sehem ndogo sana polepole mimi namuona ni tapeli, mjanja mjanja .

Na suala la nchimbi kujiuzulu kwa sisi ambao hatuna habari za ndani wala sio watu wakuamini sna habari za ndani, case ya nchimbi inatuchanganya kiasi,
i. barua ile iliyopostiwa ya taarifa kwa umma ya nchimbi inaonekana imeandaliwa vyema sana karibu kila kitu kipo on point, mule anasema "amemuandikia rais kumjulisha kua ameamua kustaafu siasa ...... hivyo anajiuzulu" --- sio kuomba kustaafu , ni kumpa taarifa/notice kama ambavyo kihalali inapaswa, kujiuzulu hakuhitaji wewe uombe maana ni uamuzi binafsi

ii. barua/taarifa ya katibu mkuu kiongozi kutoka ikulu ikaja kusema jioni ile kwamba rais amepokea ombi la nchimbi kujiuzulu na kwamba ameridhia ombi hilo, japo hatujaona hiyo barua halisi ya nchimbi kweda kwa rais lakini kwa lugha iliyotumika kwenye taarifa kwa umma itakua ngumu kuamini kama kwenye barua rasmi "kaomba kujiuzulu" bali katoa taarifa ya kujiuzulu

kwa kupitia jambo hilo napata ukakasi kuamini kwamba ile taarifa kwa umma kaandikiwa maana iweje iwe ipo vizuri sana kushinda hata response kutoka ikulu.
 
Haya sawa usirembe muandiko 😆
na kuchangia kiasi mada comment ya mdau hapo juu na wote wenye mlengo huo nawaunga mkono isipokua tu sehem ndogo sana polepole mimi namuona ni tapeli, mjanja mjanja .
Kwanini unamuona kama mjanja mjanja mkuu fafanua hata kwa uchache
Na suala la nchimbi kujiuzulu kwa sisi ambao hatuna habari za ndani wala sio watu wakuamini sna habari za ndani, case ya nchimbi inatuchanganya kiasi,
i. barua ile iliyopostiwa ya taarifa kwa umma ya nchimbi inaonekana imeandaliwa vyema sana karibu kila kitu kipo on point, mule anasema "amemuandikia rais kumjulisha kua ameamua kustaafu siasa ...... hivyo anajiuzulu" --- sio kuomba kustaafu , ni kumpa taarifa/notice kama ambavyo kihalali inapaswa, kujiuzulu hakuhitaji wewe uombe maana ni uamuzi binafsi

ii. barua/taarifa ya katibu mkuu kiongozi kutoka ikulu ikaja kusema jioni ile kwamba rais amepokea ombi la nchimbi kujiuzulu na kwamba ameridhia ombi hilo, japo hatujaona hiyo barua halisi ya nchimbi kweda kwa rais lakini kwa lugha iliyotumika kwenye taarifa kwa umma itakua ngumu kuamini kama kwenye barua rasmi "kaomba kujiuzulu" bali katoa taarifa ya kujiuzulu

kwa kupitia jambo hilo napata ukakasi kuamini kwamba ile taarifa kwa umma kaandikiwa maana iweje iwe ipo vizuri sana kushinda hata response kutoka ikulu.
Shida ni kwamba mwenyewe hatoki hadharani kusema tunabaki na theory tu
 
Haya sawa usirembe muandiko 😆

Kwanini unamuona kama mjanja mjanja mkuu fafanua hata kwa uchache

Shida ni kwamba mwenyewe hatoki hadharani kusema tunabaki na theory tu
Mwanamkakati polepole ni mjanja mjanja na lengo lake kuu ni samia kukaa pembeni kwenye uchaguzi ule wa 2025, na laiti kama samia angekataa kugombea 2025 yote aliyoyasema asingeyasema --- ushahidi wa hilo ni maneno yake mwenyewe, pindi alipokua anasema mama asigombee lasivyo atasema makubwa na vijngozi wake watachukia
 
Alikuawa na tatizo nae binafsi au?
 
Back
Top Bottom