Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!

Unataka abadilishe sheria zilizosimikwa kwa miaka 6 ndani ya siku 18? Hapana tumpe muda, umemsikia akisema sheria/kanuni kandamizi, atafanya vizuri zaidi. Acha tufurahi hata kwa maneno tu maana mbali ya Mwendazake kuwa na matendo ya kikatili lakini pia alijaliwa maneno ya kifedhuli.
 
Afanye system restore kuanzia January 2016
 
Amina
 
Sijasema kuwa nataka abadilishe sheria zilizosimikwa ndani ya miaka 6 kwa siku 18 ila nashangaa sana leo hakutoa hata ahadi ya kuzifuta sheria hizo achilia mbali kugusia kuwa zipo.

Ni kawaida wanasiasa kupumbaza wananchi kwa maneno matamu.Hata madikteta hufanya hivyo.Hata Hitler alipumbaza watu kwa maneno matamu sana hadi wananchi wakampa kibali cha kuwa waziri mkuu ila baadae aliwabadilikia.Nchi huongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa maneno matamu.

Mimi nitamuamini Mama tu kama ataenda kufuta sheria zote kandamizi ambazo alitengeneza yeye pamoja na Magufuli.Maneno yake matamu siyo lolote wala siyo chochote kwangu.Chenye faida kwangu ni akafute zile sheria mbovu ambazo alizitengeneza yeye na Magufuli na nchi iongozwe kwa sheria zenye kutoa haki na usawa.
 
Amen!
 
Kweli nimeamini shingo huwa ina akili sna kuliko kichwa. Haya wazee wa miguvu bila kutumia akili, mmezoea kula ugali mkubwa alafu unaenda kunyanyua gunia la pamba wakati wenzio wanaenda kunyanyua gunia la mchanga.
 

 
Sheria zitafwata ila kiongozi mkuu wa nchi neno lake ni faraja na pengine linaweza ku neutrialise sheria...tumeona kipindi cha JPM alikuwa ananguvu yakuikanyaga katiba na sheria hata Kama zimeandikwa kwene makaratasi...mm naamini raisi wa nchi neno lake Lina ukuu sana
 
Niliongelea general content sikupenda kutaja kimoja kimoja kwa sababu tayari alichofanya kwa wakati mfupi amejitahid kuturejesha tunapotaka kwenda.
 
Raisi hata miezi hana sasa unataka kila kitu afanye kwa muda mmoja aliokaa Kama raisi mm sioni ubaya wa watu kushangilia, watu wametoka kwene utawala uliokua unatoa maneno ya kibane na ukandamizi sasa kwann wasifurah kufarijiwa walau kwa maneno na huyu alieingia, kila Jambo ni hatua awez fanya kwa siku moja yte...ninaimani huyu mama atakuwa kiongozi mzuri tukiacha u ccm sijui u chadema Kuna watu hawana vyama wat we need ni kiongozi mzur tu awe anatoka pande yyte ile ila awe mzuri
 
Tumpatie muda mama,sio rahis kufanya hayo kwa muda wa siku 18 kumbuka kuna Bunge la bajeti linaendelea ,so kufanya reformation ya hayo yote inahitaji muda pia.
Lakini angalau kuna mwanga tunaona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…