Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!

Mkiamka ndotoni siku moja ndio mtajua hii furaha ya leo ni upepo tu utakaopita, watu wana mihemko sana.

Inashangaza sana kuona watu wanachanganywa akili na maneno tu, nasoma mpaka comment za viongozi wa upinzani naona wanaandika mambo ya kushangaza kabisa, never thought kama tuna wapinzani vichwa vyepesi namna hii.

Hawa wanachotaka ni kuendelea na mambo yao tu, wafanye biashara zao kwa amani baada ya kujichumia kupitia migongo ya "wapiga kura", yaani nasoma comments zote sijaona hata mmoja aliekumbuka Katiba Mpya leo, wote wanashangilia maneno ya mwenyekiti wa CCM, yaani kumbe wanaishi kwa kudra za mwenyekiti wa CCM! ajabu sana.

Niwakumbushe tu, hata Kikwete nae alikuwa na maneno matamu kama haya ya leo. Watanzania tusipoamka badala yake tuendelee kuvitegemea hivi "vyama vya upinzani" tumeliwa.
Hayo maneno ya Kigogo mkosaji umeya paste huku ndugu yangu.
Sio kila kitu kupinga miaka 6 ilikuwa ya machungu ,hao wapinzani unaoasema wana wanachama ,waliingizwa barabara wakaogopa kufa.
Kinachofurahisha watu ni kuona hata wana CCM hawakuwa na furaha pia.
 
Taifa limejawa na furaha kwa sababu ni taifa la majuha.Ni punguani peke yake ndiye anaweza kumsifia Mama au kufikiri kuwa Mama ana nia njema na Tanzania kwa sababu bado anaongoza nchi kwa kutumia zile zile sheria kandamizi za Magufuli.

Nchi huwa inaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa maneno matamu na ahadi za matumaini.Kuongoza nchi kwa maneno matamu na ahadi za matumaini wakati sheria ni mbovu na kandamizi hilo huwa ni changa la macho.Mama atakuwa na nia njema na Tanzania if and only if atafuta zile sheria kandamizi za Magufuli na kutunga sheria zinazoleta haki,usawa na ukuaji sahihi wa uchumi.
Mkiamka ndotoni siku moja ndio mtajua hii furaha ya leo ni upepo tu utakaopita, watu wana mihemko sana.

Inashangaza sana kuona watu wanachanganywa akili na maneno tu, nasoma mpaka comment za viongozi wa upinzani naona wanaandika mambo ya kushangaza kabisa, never thought kama tuna wapinzani vichwa vyepesi namna hii.

Hawa wanachotaka ni kuendelea na mambo yao tu, wafanye biashara zao kwa amani baada ya kujichumia kupitia migongo ya "wapiga kura", yaani nasoma comments zote sijaona hata mmoja aliekumbuka Katiba Mpya leo, wote wanashangilia maneno ya mwenyekiti wa CCM, yaani kumbe wanaishi kwa kudra za mwenyekiti wa CCM! ajabu sana.

Niwakumbushe tu, hata Kikwete nae alikuwa na maneno matamu kama haya ya leo. Watanzania tusipoamka badala yake tuendelee kuvitegemea hivi "vyama vya upinzani" tumeliwa.
Bora ya mama kuliko Jiwe Mara elfu, Mimi mwenyewe Nina furaha, tumpe mda
 
Bora huyu mama hata kama hatujamjua kuliko mtu ambaye tulishamjua anapenda tuishi kama mashetani. 🤣🤣🤣🍺🍺 Ilkua inabidi tutoke saa kumi na mbili join na saa mbili usiku tusharudi home. Maisha mafupi jmn tunajengea vizazi vijavyo sawa lakini na sisi tule kidogo jamn
Mungu amlaze sehemu anayostahili kuwepo huko alipo mavumbini.
 
Ndani ya siku 18 za Urais wa Samia Suluhu, nchi imejawa na FURAHA, siyo kwamba amepandisha mishahara HAPANA.
siyo kwamba ameajiri HAPANA
siyo kwamba anagawa pesa huko mitaani HAPANA
bali ni MATAMSHI yake tu kama Kiongozi Mkuu wa nchi yanaendelea kuliponya taifa bila sindano wala vidonge, kwenye utawala uliopita taifa liligawanyika vipande vipande, taifa liliumizwa na hata yeye alijua ndiyo maana ameanza kwa kuliponya taifa kwa maneno yake kabla ya vitendo.

Nadhani mama huyu hahitaji kuomba aombewe bali sisi kama taifa kwa imani zetu bila kujali kipato, nafasi/cheo, kanda, kabila ama jinsia tuanze kumwombea afya njema, hekima, busara na nidhamu asiingiwe na kiburi huko mbeleni.

Mafisadi pia mkae mbali na mama
Wanasiasa vigeugeu mkae mbali na mama huyu.
Viongozi wa dini vigeugeu mkae mbali na mama huyu.
Watendaji wa serikali vigeugeu mkae mbali na mama huyu.
Wajinga wajinga mkae mbali na mama huyu.
Waandishi wa habari vigeugeu mkae mbali na mama huyu.
Matapeli wala rushwa mkae mbali na mama huyu

Hatufurahi kupitiliza ila angalau ukikutana watanzia watano, watatu kama sio wanne wanalotabasamu utasikia mama ....oohh mama ni mtu na nusu .

Mungu Mbariki Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan
Mungu atubariki Watanzania
Mungu Ibariki Tanzania.
Ndugu yangu hakuna kinachouma Kama kodi za dhuluma. Wafanya biashara wamepitia maumivu mengi sana
 
1.Sheria ya Mitandao ya mwaka 2015.

2.Kanuni za Mawasiliano ya Kieletroniki na ya Posta (Maudhui ya Mtandaoni) zilizopitishwa mwaka 2018 zinamtaka kila anaemiliki blogu au tovuti kulipa ada ya leseni hadi shilingi za kitanzania milioni 2.1 (zaidi ya Dola za Marekani 900). Sheria hii pia inadhibiti maudhui ya mtandaoni na kuruhusu uchunguzi wa mitandao bila usimamizi wa mahakama.

3.Serikali ya Tanzania pia inadhibiti utafiti binafsi na upatikanaji wa taarifa za takwimu kwa umma kupitia sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, ambayo inawanyima wananchi vyanzo mbadala vya taarifa huru zilizothibitishwa. Wakati marekebisho ya sheria hii yaliyoletwa mwaka 2019 yameondoa dhima ya jinai kwa kuchapisha takwimu zisizo rasmi, mamlaka bado inadhibiti nani anayeweza kukusanya na kusambaza taarifa za takwimu na kuamua kipi ni sahihi au sio sahihi.

4.Januari 2019, Bunge lilifanya marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na kuweka vikwazo vingi zaidi vya haki ya uhuru wa kushiriki na kukusanyika kwa amani. Marekebisho haya yalimpa Msajili wa Vyama vya Siasa nguvu ya kufuta vyama vya siasa, kuitisha taarifa kutoka vyama vya siasa na kusimamisha wanachama. Pia ilianzisha hitaji la mashirika na watu binafsi kupata kibali kabla ya kutoa elimu ya uraia, jambo ambalo linazuia haki ya mwananchi kupata taarifa.
I think hivo vitarudishwa Tena bungeni ka hyo Sheria ya mitandao, kanuni za mawasiliano ya kielectronic ni ya kufutwa kabisa hata hyo ya msajil ni ya kufutwa kabisa
 
Mkiamka ndotoni siku moja ndio mtajua hii furaha ya leo ni upepo tu utakaopita, watu wana mihemko sana.

Inashangaza sana kuona watu wanachanganywa akili na maneno tu, nasoma mpaka comment za viongozi wa upinzani naona wanaandika mambo ya kushangaza kabisa, never thought kama tuna wapinzani vichwa vyepesi namna hii.

Hawa wanachotaka ni kuendelea na mambo yao tu, wafanye biashara zao kwa amani baada ya kujichumia kupitia migongo ya "wapiga kura", yaani nasoma comments zote sijaona hata mmoja aliekumbuka Katiba Mpya leo, wote wanashangilia maneno ya mwenyekiti wa CCM, yaani kumbe wanaishi kwa kudra za mwenyekiti wa CCM! ajabu sana.

Niwakumbushe tu, hata Kikwete nae alikuwa na maneno matamu kama haya ya leo. Watanzania tusipoamka badala yake tuendelee kuvitegemea hivi "vyama vya upinzani" tumeliwa.
Kwahiyo mkuu tumshauri mama kesho asubuhi akija aite vyombo vya habari na aseme ataleta katiba mpya???
 
Unavyosema maneno tu unakosea
1. Ameongelea sana kuongeza uwekezaji haya sio maneno tu ni mipango
2. Kachagua makamu mzuri
3. Kaanza kushughulikia Corona
4. Kushughulikia mambo ya muungano
5. Kuchagua waziri mpya wa mambo ya nje
6. Kutoa wanasiasa na kuweka wafanyakazi wenye uwezo mfano kubadili katibu mkuu wa nchi
7. Kubadilisha mifumo ili isitegemea watu tumeona Raisi kafariki! mifumo imara ni mizuri
8. Uhuru zaidi wa vyombo vya habari
9. Kupunguza uhasama na wapinzani
Hawa watu sijui wanataka wafanyiwe nini kwa kweli.

Hili taifa ni la maajabu sana.

Mama yetu kipenzi ameanza kushughulikia matatizo yetu tena katika namna inayoridhisha haswa ila bado tu.

Dah! Poleni viongozi wa Tanzania
 
Mama kaonyesha kutofurahishwa na mambo yalivyokuwa yanaendeshwa. Hilo ndilo la msingi na la awali kabisa.
Sheria huwezi amka na kuzifuta,ni mchakato.
Amin nakwambia Mh. Rais Samia anakwenda kufuta sheria zote za kionevu na kidhalimu.
Nia anayo.
Uwezo anao.
Yaani baadhi ya wenzetu sijui wana akili gani.

Wao wakiambiwa sheria ndogo tu kwamba wacha kunywa pombe basi hawatoweza kuamka asubuhi na kuacha, itabidi iwe ni mchakato kuacha hiyo pombe.

Ajabu wanataka mama akurupuke na kutafuta kila sheria hawajui kama ni mchakato
 
Taifa limejawa na furaha kwa sababu ni taifa la majuha.Ni punguani peke yake ndiye anaweza kumsifia Mama au kufikiri kuwa Mama ana nia njema na Tanzania kwa sababu bado anaongoza nchi kwa kutumia zile zile sheria kandamizi za Magufuli.

Nchi huwa inaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa maneno matamu na ahadi za matumaini.Kuongoza nchi kwa maneno matamu na ahadi za matumaini wakati sheria ni mbovu na kandamizi hilo huwa ni changa la macho.Mama atakuwa na nia njema na Tanzania if and only if atafuta zile sheria kandamizi za Magufuli na kutunga sheria zinazoleta haki,usawa na ukuaji sahihi wa uchumi.
Je ulitaka azibadikishe kwa usiku mmoja? Utaratibu ni kwamba hizi sheria lazima zipelekwe bungeni na kuzifutulia mbali. Nakubaliana na wewe sheria kandamizi zipo na haziitaji kuwepo kwenye jamii na dunia ya leo?
 
Taifa limejawa na furaha kwa sababu ni taifa la majuha.Ni punguani peke yake ndiye anaweza kumsifia Mama au kufikiri kuwa Mama ana nia njema na Tanzania kwa sababu bado anaongoza nchi kwa kutumia zile zile sheria kandamizi za Magufuli.

Nchi huwa inaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa maneno matamu na ahadi za matumaini.Kuongoza nchi kwa maneno matamu na ahadi za matumaini wakati sheria ni mbovu na kandamizi hilo huwa ni changa la macho.Mama atakuwa na nia njema na Tanzania if and only if atafuta zile sheria kandamizi za Magufuli na kutunga sheria zinazoleta haki,usawa na ukuaji sahihi wa uchumi.
Sasa ana wiki moja unaanza kumlaumu hivi
 
Unavyosema maneno tu unakosea
1. Ameongelea sana kuongeza uwekezaji haya sio maneno tu ni mipango
2. Kachagua makamu mzuri
3. Kaanza kushughulikia Corona
4. Kushughulikia mambo ya muungano
5. Kuchagua waziri mpya wa mambo ya nje
6. Kutoa wanasiasa na kuweka wafanyakazi wenye uwezo mfano kubadili katibu mkuu wa nchi
7. Kubadilisha mifumo ili isitegemea watu tumeona Raisi kafariki! mifumo imara ni mizuri
8. Uhuru zaidi wa vyombo vya habari
9. Kupunguza uhasama na wapinzani
ndio maana umeambiwa mnafiki
 
1.Sheria ya Mitandao ya mwaka 2015.

2.Kanuni za Mawasiliano ya Kieletroniki na ya Posta (Maudhui ya Mtandaoni) zilizopitishwa mwaka 2018 zinamtaka kila anaemiliki blogu au tovuti kulipa ada ya leseni hadi shilingi za kitanzania milioni 2.1 (zaidi ya Dola za Marekani 900). Sheria hii pia inadhibiti maudhui ya mtandaoni na kuruhusu uchunguzi wa mitandao bila usimamizi wa mahakama.

3.Serikali ya Tanzania pia inadhibiti utafiti binafsi na upatikanaji wa taarifa za takwimu kwa umma kupitia sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, ambayo inawanyima wananchi vyanzo mbadala vya taarifa huru zilizothibitishwa. Wakati marekebisho ya sheria hii yaliyoletwa mwaka 2019 yameondoa dhima ya jinai kwa kuchapisha takwimu zisizo rasmi, mamlaka bado inadhibiti nani anayeweza kukusanya na kusambaza taarifa za takwimu na kuamua kipi ni sahihi au sio sahihi.

4.Januari 2019, Bunge lilifanya marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na kuweka vikwazo vingi zaidi vya haki ya uhuru wa kushiriki na kukusanyika kwa amani. Marekebisho haya yalimpa Msajili wa Vyama vya Siasa nguvu ya kufuta vyama vya siasa, kuitisha taarifa kutoka vyama vya siasa na kusimamisha wanachama. Pia ilianzisha hitaji la mashirika na watu binafsi kupata kibali kabla ya kutoa elimu ya uraia, jambo ambalo linazuia haki ya mwananchi kupata taarifa.
Ni kweli usemayo ila tusemacho ni kwamba tuna imani na tumepata imani na Mama, alivyomsikivu haya atayafanyia kazi. Mama anatakiwa apewe muda na tusikatishane tamaa kwamba eti ni wale wale tu.

Ndani ya siku 18 mama amefanya tuliyokuwa tunayalilia for ages.

Sisi watanzania tunampenda na tuna imani na Mheshimiwa rais wetu kipenzi chetu, mama yetu Samia Suluhu Hassan
 
Ni kawaida wanasiasa kupumbaza wananchi kwa maneno matamu.Hata madikteta hufanya hivyo.Hata Hitler alipumbaza watu kwa maneno matamu sana hadi wananchi wakampa kibali cha kuwa waziri mkuu ila baadae aliwabadilikia.Nchi huongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa maneno matamu.Mimi nitamuamini Mama tu kama ataenda kufuta sheria zote kandamizi ambazo alitengeneza yeye pamoja na Magufuli.
Mkuu tunakupa ruhusa wewe usimuamini.

Tuachie Sisi watanzania tumuamini.
 
Unataka abadilishe sheria zilizosimikwa kwa miaka 6 ndani ya siku 18? Hapana tumpe muda, umemsikia akisema sheria/kanuni kandamizi, atafanya vizuri zaidi. Acha tufurahi hata kwa maneno tu maana mbali ya Mwendazake kuwa na matendo ya kikatili lakini pia alijaliwa maneno ya kifedhuli.
Yaani saa nyengine ndio maana rais Magufuli alikuwa akiwaambia hawa wabaki na mavi yao nyumbani.

Yaani mnafarijiwa na kupewa tumaini jipya huku mambo yakifanyika mdogo mdogo ila bado tu hawa walimwengu
 
Back
Top Bottom