Ndege ya Ukraine ilitunguliwa kwa kombora

Ndege ya Ukraine ilitunguliwa kwa kombora

Waziri mkuu wa canada Justin Trudeau amezungumza na wanahabari na kuweka wazi kuna ushahidi wa video ambao unaonesha kuwa ndege ya UKraine Boeng 737 PS752 iliyoanguka Iran ilitunguliwa na makomboro ya Wairan na watu 176 kufariki dunia.

Canada ni moja ya nchi iliyopoteza watu wengi 63 ukiacha Ukraine watu 11,Sweden 10,4 Waafghastan,Wajerumani watatu na Waingireza watatu.

Ameungwa Mkono na Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson na kusema wanafanya kazi na Canada kwa ukaribu ili kuweza kuchunguza mambo kiuwazi zaidi kuhusu makombora ya Iran yaliyotungua ndege.

Ijapokuwa Iran sasa hawana cha kuhofia lakini video hii kama ikiongeza ushawishi na kuaminika basi watakuwa wamejifunga wenyewe kwa bao la mkono kwani Wairani wengi wameteketea katika tukio hili ambalo kw atasfri yake ni mauji yasiyo na hatia

Mdahalo umekuwa mkubwa wengine wakisema makombora hayo kutungua ndege hiyo ni makosa yaliyofanywa na jeshi la Iran na haikuwa lengo lao kwani watu waliokufa wengi ni wairan 82
Imani kubwa Irani wapo makini sana kwenye usalama walijua taarifa zote kuhusu abiria waliomo ndani,Inawezekana wakati wanafanya mashambulizi katika kambi za jeshi za marekani Iraq wakakosea hesabu zao.

Wengine wanasema walishambulia kwa kusudi huenda walipata taarifa za kintelejesia dakika za mwisho kuwa kuna watu muhimu wa watesi wao Marekani kuwamaliza haraka ni kuwatia msumari wa moto moyoni.

chini hapo kuna video
 

Attachments

  • dddd.jpg
    dddd.jpg
    84.2 KB · Views: 1
  • Trudeau and Johnson say they have intelligence Iran shot down Ukrainian airliner.mp4
    2.5 MB
‘....Mchakato wa Iran, ... tutaishirikisha kwa ukaribu zaid NATO...’- Trump
 
Kwan ndege baada yakufanyiwa ukaguzi haiwez pata ajali how kama ilikua ndege haina shida ila ni uzembe 2 wadereva

US na CANADA Kwanini Ndio Wawe Wao Tu Miongoni Mwamataifa Makubwa Yanayoshikilia Kama Ndege Iliripuliwa Na Iran Millitary Equipments !?

Unamalizaje kuwahusisha IRAN Wakat HataUchunguzi Haujakamilika
Mabaki ya Hizo Missile Zimeonekana Wapi ?!
Kabla hatujasema kuwa ni propaganda za Marekani kwanza tuyazingatie mambo yafuatayo;

Ndege ya Ukraine ilikuwa na miaka tatu tu, na ilikuwa imefanyiwa ukaguzi wa kiusalama hivi karibuni (siku mbili kabla ya ajali). Ni hitilafu za namna gani zilizopelekea kuwaka moto kwa ndege hiyo na kisha kulipuka? Isitoshe mawasiliano yalikatika ghafla, jambo linalozua maswali mengi ya kiufundi kuhusu hiyo hitilafu unayoisema.

Kuna ushahidi wa picha za mabaki ya kombora hilo pamoja na video inayoonekana kuonesha jinsi ndege hiyo ilivyotunguliwa na kombora. Video pamoja na picha nimekwisha post humu.

Kitendo cha Ubalozi wa Ukraine nchini Iran kuonekana kufuta taarifa ya hapo awali iliyokataa kuhusisha ajali hiyo na tukio la kigaidi ama shambulio la roketi, kinaleta maswali mengi na mpaka sasa tayari nchi kama Canada pamoja na Ukraine yenyewe inakubali kuwa kuna uwezekano wa ndege hiyo kutunguliwa.
Finally
Nyie Ndio Mlopinga Habari Kutoka Vyanzo Vyandani Ya IRAN Ikiwemo Pars Today Kwamba Wameua Wanajeshi 200s Wa US

Ila Nyie Ndio Mnapingana Pia Na Vyombo Vyahabari Hvyo Hvyo Vya IRAN Kama Sababu Za Ajali Sio Missile Mnakwamia Wap !?


Habari zinazotolewa Na IRAN za UONGO Ila Zinazotolewa na Wengine Ndio Habari Kamili hehehe.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuuwa mamilioni ya watu Iraq, Vietnam, Syria, Japan, Somalia, kuweit nk, kutuletea ukimwi, ndoa za jinsia moja, ushoga, kuiba malighafi za watu kwa nguvu, uchafu wote huu ni yy ngurue
WWI na WWII wakati zinatukia Marekani alikuwa na nguvu gani ya kijeshi?
.
Toka ashike usukani yeye ni vita gani kubwa imetokea?
Mshukuruni sana nyie mjahidini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuuwa mamilioni ya watu Iraq, Vietnam, Syria, Japan, Somalia, kuweit nk, kutuletea ukimwi, ndoa za jinsia moja, ushoga, kuiba malighafi za watu kwa nguvu, uchafu wote huu ni yy ngurue

Sent using Jamii Forums mobile app
Wairaq waliuana wao kwa wao au mmarekani alienda akaanza kuwaua?
Vietnam huko ni ujinga wao.
Syria vita bado inaendelea nenda kafungue kesi yako dhidi yao kama wanaua au wako pale kurejesha amani
.
Mrusi anatungua hadi miskiti watu wanaswali huko Syria anaua raia kimakosa alafu unaitaja America lmao!
Somalia America anaua au Alshabab ndio yanaua?
Haya si yamelipua kenya juzi tu hapa
.
Japan waliutaka mchezo wenyewe, huoni sasa hivi wamekuwa kama kaka na dada hadi military base za US ndani
Iran naye anautaka.
Ukimwi mmarekani aliuletaje Struggle nipe darasa?
.
Ndoa za jinsia moja ndio ushoga huohuo hii kitu ipo toka zama za kale chukua Biblia soma habari za Sodoma na Gomora.
Kuiba malighafi anaiba malighafi gani?
.
ALAFU ACHA DHARAU KWA NGURUWE (KITIMOTO) NYAMA TAMU DUNIA NZIMA 😋
 
Kuuwa mamilioni ya watu Iraq, Vietnam, Syria, Japan, Somalia, kuweit nk, kutuletea ukimwi, ndoa za jinsia moja, ushoga, kuiba malighafi za watu kwa nguvu, uchafu wote huu ni yy ngurue

Sent using Jamii Forums mobile app
Mauaji mbona hata hapa bongo yapo! Albino, vikongwe, wasiojulikana, ujambazi, nk. Wale wanaouwawa na marekani ni kama jinsi majambazi yanavyouwawa na polisi, je kuna shida jambazi kuuwawa likijaribu kupambana na polisi?! Kuhusu mauaji kukoma dunia hii hilo sahau.
Yote kwa yote dunia iko salama sana kiganjani mwa marekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cme-on bro, A u serious, mbona unaongea kimas-hara
Mauaji mbona hata hapa bongo yapo! Albino, vikongwe, wasiojulikana, ujambazi, nk. Wale wanaouwawa na marekani ni kama jinsi majambazi yanavyouwawa na polisi, je kuna shida jambazi kuuwawa likijaribu kupambana na polisi?! Kuhusu mauaji kukoma dunia hii hilo sahau.
Yote kwa yote dunia iko salama sana kiganjani mwa marekani.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom