FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
- Thread starter
- #121
Ni kweli kabisa yaweza kupata ajali baada tu ya kufanyiwa ukaguzi lakini kinachopaswa kutazamwa ni sababu zipi au mazingira gani kitaalamu yaliyosababisha ajali hiyo kutokea.Kwan ndege baada yakufanyiwa ukaguzi haiwez pata ajali how kama ilikua ndege haina shida ila ni uzembe 2 wadereva
US na CANADA Kwanini Ndio Wawe Wao Tu Miongoni Mwamataifa Makubwa Yanayoshikilia Kama Ndege Iliripuliwa Na Iran Millitary Equipments !?
Unamalizaje kuwahusisha IRAN Wakat HataUchunguzi Haujakamilika
Mabaki ya Hizo Missile Zimeonekana Wapi ?!Finally
Nyie Ndio Mlopinga Habari Kutoka Vyanzo Vyandani Ya IRAN Ikiwemo Pars Today Kwamba Wameua Wanajeshi 200s Wa US
Ila Nyie Ndio Mnapingana Pia Na Vyombo Vyahabari Hvyo Hvyo Vya IRAN Kama Sababu Za Ajali Sio Missile Mnakwamia Wap !?
Habari zinazotolewa Na IRAN za UONGO Ila Zinazotolewa na Wengine Ndio Habari Kamili hehehe.....
Sent using Jamii Forums mobile app
Uthibitisho wa kimazingira na hata wa kitaalamu uliopo mpaka sasa unakataa kabisa kukubaliana na madai ya awali ya Iran kwamba lilikuwa ni tatizo la kiufundi.
1. Kukatika ghafla kwa mawasiliano. Kitaalamu jambo hilo linaleta mashaka kwamba kulikuwa na hitilafu ya ndani tu na si chanzo kutoka nje.
2. Hitilafu katika vifaa maalumu vya kutunzia kumbukumbu (Black boxes). Kitaalamu, inaleta wasiwasi kwamba ni matatizo tu ya kiufundi.
3. Ushahidi wa mabaki ya kombora linalotajwa kuhusika kuiangusha ndege hiyo, mabaki yamepatikana karibu na eneo ilipoanguka ndege hiyo. Picha zipo.
4. Ushahidi wa video wakati wa ajali yenyewe, wakati ndege ilipopigwa kwa kombora, kuwaka kwake moto, kuanguka na na kisha kulipuka.
Picha zimepigwa na video imerekodiwa katika mji wa Parand. Mji ambao upo karibu kabisa na uwanja wa ndege wa Tehran. Picha na video vyote viwili vina uthibitisho wa mazingira yanayofanana.
Unaweza kusafiri na kwenda eneo la tukio ukajionee mwenyewe.
Unasema kwamba naihusisha Iran wakati uchunguzi haujafanyika.
Lakini,
Kumbuka kuwa Iran ndiyo ilikuwa ya kwanza kabisa kutangulia mapema na kutuambia kwamba ni "tatizo la kiufundi" kabla hata ya huo unaoitwa "uchunguzi" kufanyika.